WATUMISHI WAPYA BUGANDO WAPATIWA MAFUNZO
..
Watumishi wapya 118 wa kada mbalimbali wameanza utumishi wao Bugando kwa kupatiwa mafunzo ya siku tatu yanayolenga kuwaandaa kuwa tayari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga amewakaribisha na kuwapongeza kwa kupata fursa hiyo ya ajira na kuwataka kutumia vyema mafunzo haya;
"Nimefurahi kukutana nanyi, ni nafasi nzuri sana na adhimu mmeipata, Napenda kuishukuru Serikali yetu ya Tanzania chini ya Ofisi ya Rais, menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora kwa kutupatia watumishi, mnapokuja mnaongeza timu na mtaongeza ufanisi wa utoaji huduma na mtasadia uborehsaji wa huduma, niwapongeze na kuwashukuru wawezeshaji wa mafunzo haya muhimu na niwahimize mtumie vizuri mafunzo haya , suala la mawasiliano mazuri ni muhimu kwani maneno mazuri yanaleta faraja kubwa kwa Mgonjwa, kufata mila na desturi za Bugando kwa kujiepusha na rushwa, wizi, mavazi yasiyofaa na mengine, myashike vizuri na kuyazingatia kwa vitendo" amesema Sr. Dkt. Massenga.
Mafunzo haya ya siku tatu kwa Watumishi wapya 118 yameanza leo Disemba 01, 2025 na yamejikita katika kuhakikisha Mgonjwa anahudumiwa kwa huruma na upendo, huduma nzuri kwa wateja, mawasiliano mazuri, ushirikiano, kufanya kazi bila msongo wa mawazo na mengine yanayotolewa na ofisi ya utumishi Bugando chini ya mratibu Bw. Lufingo Mwaipopo.
BMC SACCOS LTD YAFANYA MKUTANO WAKE MKUU WA MWAKA
..
Chama cha Ushirika cha Wafanyakazi wa Bugando, chuo cha CUHAS na MWACHAS kimefanya mkutano wake mkuu wa mwaka (Mkutano wa 21) leo Novemba 29, 2025, ili kujadili maendeleo ya chama walipotoka, walipo na matarajio ya Chama kwa miaka ijayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya BMC SACCOS LTD Bw. Martin Masunga amesema,chama hiki kina wanachama 552 sasa tangu kuanza kwake mwaka 2004, chama hiki kimekuwa msaada mkubwa wa kuwainua Wanachama wake kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu, kutoa elimu ya matumizi ya fedha na fursa nyingine nyingi ambazo zimewainua Wanachama wake na chama kuzidi kukua kwa Wanachama wapya na ustawi wa kiuchumi.
Mgeni rasmi wa mkutano huu na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga amewapongeza BMC SACCOS LTD na kusema; "Hongereni sana kwa hatua kubwa mliyopiga, ripoti zenu zinaonesha maendeleo mbalimbali kwa Wanachama ikiwemo kuwawezesha ada za masomo kwao binafsi, watoto na jamaa, kujenga nyumba za kuishi, usafiri na mengine mnafanya vyema, niwashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao umekuwepo na viongozi, na kwa kutokana na umuhimu wa Chama hiki, nipende kuwahimiza Wanachama kuwa waaminifu kwa kutimiza wajibu wao na kuhamasisha wengine kujiunga kupata fursa zinazopatikana SACCOS "
BMC SACCOS LTD katika mkutano wake wa 21 umehudhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo Maafisa Ushirika wa Mkoa na pia limefanyika zoezi la kupokea Wanachama wapya, tathmini ya mapato na matumizi pamoja na kutoa taarifa za mfuko wa Chama.
MWADETA YASHIRIKIANA NA BUGANDO KUTOA MAFUNZO MAALUM YA KUHUDUMIA WATOTO WENYE KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI KWA WATAALAM WA AFYA MKOA WA MWANZA
..
Leo Novemba 27, 2025 MWADETA (Mwanangu Development Tanzania ) na Hospitali ya Bugando wameshirikiana kutoa mafunzo maalum nadharia na vitendo kwa Wataalam wa vituo vya afya kutoka Mkoa Mwanza Wilaya ya Nyamagana , Misungwi, Ilemela na Magu. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wataalam wa afya namna nzuri ya kuwahudumia watoto wenye kichwa kikubwa (hydrocephalus) na mgongo wazi (spina bifida).
Akizungumza katika mafunzo mgeni rasmii Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amewashukuru MWADETA na wakufunzi kutoka hospitali ya Bugando, kuwezesha mafunzo haya, “naamini mtafundishwa namna mbalimbali za kuweza kuwahudumia watoto wenye mgongo wazi na vichwa vikubwa namna ya kutatua changamoto ili kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa wagonjwa.”
Dkt. Leba amesisitiza umuhimu wa kuwahudumia watoto hao kwa ufanisi ili kuboresha maisha yao na kuwapa nafasi ya kuishi maisha ya kawaida. Lengo la mafunzo hayo ni kuboresha huduma za afya kwa watoto wenye changamoto hizo mkoani Mwanza, na kuwapa wataalam ujuzi na mbinu za kisasa za kuwahudumia wagonjwa hao.
MAHAFALI YA 18 YA CHUO KIKUU CHA KIKATOLIKI CHA SAYANSI YA AFYA (CUHAS-BUGANDO)
..
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Sr. Dr. Alicia. Massenga mapema hii leo tarehe 22.Novemba, 2025 ameshiriki Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi ya Afya ( Cuhas - Bugando)
WATAALAM WA KUTOA DAWA ZA USINGIZI NA GANZI SALAMA NCHINI WAPEWA MAFUNZO BUGANDO.
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefungua rasmi mafunzo ya siku tatu kwa Wataalam 18 wa kutoa dawa za usingizi na ganzi salama kutoka vituo na Hospitali mbalimbali nchini yakilenga kuboresha huduma hiyo haswa kwa wajawazito wakati wa kujifungua kwa upasuaji.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Wataalam Bingwa na Bingwa Bobezi wa Usingizi na ganzi salama wa Bugando na Chuo Kikuu cha CUHAS, kwaajili ya kuongeza ujuzi na utaalam katika kumhudumia mama mjamzito wakati wa kujifungia kwani usingizi na ganzi salama ni hatua za awali muhimu katika upasuaji.
BUGANDO YAUNGANA NA DUNIA KUADHIMISHA WIKI YA UPIMAJI WA HOMA YA INI.
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jijini Mwanza imeungana na Dunia kuadhimisha wiki ya upimaji wa homa ya in duniani inayofanyika Novemba 18 hadi 24 Kila mwaka. Katika maadhimisho haya, Bugando imetoa huduma ya uchunguzi, upimaji na elimu namna ya kujikinga na ugonjwa huo kwa wanafunzi wa chuo cha CUHAS na MWACHAS.
Mkuu Wa Idara ya Afya jamii na Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani Dkt. Glory Manyangu amesema homa ya Ini ni miongoni mwa ugonjwa unaoathiri watu wengi bila kujua, hivyo kuwahi kupima mapema ni muhimu, hivyo tumepanga huduma hii kuwafikia Watu 200 wakiwemo wanafunzi na watumishi pamoja na watu ambao hawajapata chanjo.
Pia Dkt. Glory amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupima, kupata ushauri na kupata njia sahihi ya kujilinda dhidi ya maambukizi.
BUGANDO YATOA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA UGONJWA WA KISUKARI
..
Ikiwa lengo la kampeni ya siku ya kisukari duniani 2025 lilivyojikita katika kuzingatia kisukari mahali pa kazi, Hospitali ya Bugando leo Novemba 17,2025 imeendelea kutekeleza kampeni hiyo kwa kutoa huduma za uchunguzi wa ugonjwa wa kisukari kwa watumishi wa kampuni ya Serengeti Breweries - Mwanza huku madhumuni yakiwa ni kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa kisukari, kuhimiza upimaji wa mapema ili kuweza kuboresha Afya ya jamii kwa ujumla.
Akizungumza katika upimaji huo Bi. Rolinda Samson kiyumbi Site operation Manager wa Serengeti Breweries, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kuwafikia watumishi wa Serengeti Breweries kwa njia ya huduma na kuomba mashirikiano hayo yawe endelevu kwani yana manufaa kwa pande zote mbili na kuahidi kwamba wako tayari kushirikiana na Hospitali ya Bugando.
ABBOTT FUND TANZANIA YAKABIDHI BUGANDO MRADI WA JENGO LA KITUO CHA MAFUNZO KWA VITENDO TIBA ZA DHARURA NA AJALI.
..
Katika hatua za Awali, Taasisi ya Abbot Fund kwa kushirikiana na Wizara ya Afya nchini imekabidhi mradi wa jengo la kituo cha mafunzo kwa vitendo tiba za dharura na ajali (Emergency Medicine Training Hub, Lake Zone)
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Jacqueline Kidunda akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bugando, ameishukuru Abbott na Wizara ya Afya kwa kituo hiki muhimu ambacho kitasadia wakazi wa Kanda ya ziwa kwani kitapelekea wataalamu wa Idara ya dharura na Wanafunzi kupata mafunzo muhimu Kwa vitendo na kuleta matokeo chanya zaidi katika kuwahudumia wagonjwa.
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma za dharura Dkt. Ally Akrab amesema watatumia vyema kituo hicho kwa kuhakikisha wataalam wanapata ujuzi maalumu kwa vitendo na kuwa kituo muhimu cha mafunzo kwa wataalam wa huduma za dharura kutoka vituo vingine kufika Bugando kupata mafunzo hayo.
Aidha, Dkt. Raya Mussa ambaye ni Meneja mradi wa huduma za dharura Abbott amesema waliona kuna haja ya kuwa na kituo hiki, kwani kitasaidia mafunzo na ujuzi maalum kwa wataalam wa Idara za dharura nchini hivyo kupitia kituo hiiki,Hospitali ya Bugando ikiwa kama mlezi itasadia kuongeza huduma bora za dharura Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
BUGANDO YAPOKEA VIFAA VYA KISASA VYA UPASUAJI WA MISHIPA YA FAHAMU, UTI WA MGONGO NA UBONGO KUTOKA UJERUMANI .
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando imepokea vifaa maalum vya kisasa kwa ajili ya upasuaji wa uti wa mgongo, ubongo na mishipa ya fahamu. Vifaa hivyo vimewasilishwa kupitia kambi maalum ya kitabibu iliyoanza rasmi Oktoba 27, 2025, kwa ushirikiano kati ya wataalamu wa Bugando na madaktari bingwa kutoka Chuo Kikuu cha Augsburg na Chuo Kikuu cha Lausitz-Carl Thiem vya Ujerumani. Kambi hiyo, inayotarajiwa kumalizika Oktoba 31, 2025, inalenga kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo sugu ya mfumo wa fahamu yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu na matumizi ya teknolojia za kisasa.
Akizungumza katika kambi hiyo, Dkt. Sr. Alicia Massenga Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Bugando amesema, “katika kambi hii, Hospitali ya Bugando imepokea vifaa vinne vya kisasa vyenye uwezo wa kipekee katika utambuzi na matibabu ya magonjwa ya mfumo wa fahamu, ambavyo ni: CONVIVO, NEURO NAVIGATION, INTRA BEAM 600, na NEURO MONITORING.” na kushukuru kwa vifaa hivyo ambavyo vitakuwa vya msaada kwa matibabu ya upasuaji kwa watanzania.
Naye Dkt. Gerald Mayaya, daktari bingwa bobezi wa upasuaji wa mishipa ya fahamu Bugando, “Tunatarajia kuona wagonjwa wapatao 100, na kati yao takriban 20 watanyiwa upasuaji pia vifaa hivyo vitasaidia katika kubaini (detect) tatizo la uvimbe kwenye ubongo au uti wa mgongo wakati wa upasuaji, na kutoa majibu ya uchunguzi papo hapo huku upasuaji ukiendelea, kurahisisha upasuaji kwa urahisi zaidi, kupunguza muda wa matibabu na kuongeza ufanisi wa tiba na pia kuzuia madhara kwenye mfumo wa fahamu na kuongeza usalama wa mgonjwa.”
Kupitia kambi hiyo, Hospitali ya Bugando inatarajia kuongeza ujuzi wa madaktari wake, kuboresha huduma za kibingwa kwa wagonjwa wa ubongo na uti wa mgongo, na mishipa ya fahamu, sambamba na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimataifa kati ya Tanzania na Ujerumani katika sekta ya afya
RMO MWANZA AFANYA ZIARA YA TATHMINI YA MREJESHO NA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA HUDUMA BUGANDO.
..
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba pamoja na timu ya Afya mkoa, leo Oktoba 22, 2025 wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wakilenga kufanya tathmini ya mrejesho wa usimamizi shirikishi wa huduma kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania.
Akizungumza katika ziara hiyo Dkt. Jesca Lebba ameipongeza Hospitali ya Bugando kwa ushirikiano wao wanaoendelea kuuonesha katika kutoa huduma Kwa Wananchi lakini pia ujuzi na maarifa kwa wataalamu wengine wakiwemo wataalamu wa Hospitali na vituo vilivyomo chini ya Bugando. Pia, amesisitiza suala la mawasiliano kwa watoa huduma na hasa kwa wagonjwa wa dharura na wagonjwa wa rufaa ili kuweza kutoa huduma sahihi na kwa wakati sahihi kwa mgonjwa ambapo ameahidi kufanya kazi kwa kushirikiana na Hospitali pamoja na timu ya usimamizi wa huduma za Afya za halmashauri (CHMT).
Aidha, Kaimu mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dkt. Samson Kichiba akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Sr. Dkt. Alicia Massenga amemshukuru Dkt. Lebba kwa ziara hii yenye manufaa makubwa na kuahidi kwamba, Bugando ipo tayari kufanya kazi kwa kushirikiana pamoja na timu ya mkoa ili kuhakikisha huduma za Afya zinapatikana hata katika vituo vidogo vya afya.
Timu hii ilipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali ikiwemo maabara, labour, NICU, pamoja na famasi.
MAFUNZO YA HUDUMA ZA DHARURA KWA WATOTO YATOLEWA BUGANDO
..
Hospitali ya Bugando kwa kushirikiana na Wataalam kutoka Hospitali ya Boston ya nchini Marekani, inaendesha mafunzo ya siku tatu ya huduma za dharura kwa Madaktari na Wauguzi 44 wa Idara ya Wagonjwa mahututi (ICU) na Idara ya watoto yakilenga kuongeza matokeo chanya zaidi ya kumhudumia Mgonjwa.
Mafunzo haya yamefunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga ambapo amewakaribisha wageni kutoka Hospitali ya Boston nchini Marekani, akiwemo Rebecca John's(Muuguzi Bingwa wa Watoto), Dkt. Jacky Marrinam(Daktari wa ICU) na Karyan Palombe (Muuguzi wa ICU) kwa ushirikiano wao chanya kupitia mafunzo haya muhimu.
"Mafunzo haya ni muhimu sana, tunapopata wataalam hawa kutoka Boston wanaokuja hapa kutupa ujuzi na uwezo zaidi, ni vyema washiriki wote tuyazingatie naamini tutapata matokeo bora zaidi katika kazi yetu, hata wale ambao hawapo hapa kutokana na majukumu mkawape elimu hii kwani matokeo yanasema sisi ni nani kupitia huduma tunayotoa. Nawashukuru timu kutoka Boston kwa ushirikiano huu ambao ni muhimu siyo kwetu tu Bugando bali hadi kwa Wagonjwa wetu" amesema Sr. Dkt. Alicia Massenga, Mkurugenzi Mkuu Bugando.
Naye Mkuu wa Idara ya ICU Bugando Dkt. Debora Madyedye amesema mafunzo haya yatasadia kuongeza ufanisi katika utendaji wao kwani yatagusa nyanja zote muhimu kwa kushirikisha Madaktari na Wauguzi wa Idara kadhaa ambazo zinashirikiana kuhudumia Mgonjwa wa dharura na kuomba mafunzo yawe endelevu zaidi.
COSECSA NA OPERATION SMILE WAFANYA ZIARA BUGANDO KWA LENGO LA KUBORESHA HUDUMA ZA UPASUAJI SANIFU.
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, mapema leo Oktoba 17, 2025, imepokea wageni kutoka COSECSA (College of Surgeons of East, Central and Southern Africa) pamoja na Shirika la Operation Smile, kwa lengo la kuimarisha ubora wa huduma za upasuaji, mafunzo ya kitabibu, na utafiti katika idara ya upasuaji sanifu (Plastic and Reconstructive Surgery).
COSECSA ni taasisi ya kitaaluma inayotoa mafunzo ya juu ya upasuaji kwa madaktari katika nchi 14 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na nyinginezo. Ushirikiano huu unalenga kuinua viwango vya huduma za afya kwa kutoa elimu endelevu na fursa za kitaaluma kwa wataalamu wa upasuaji.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bugando, Dkt. Samson Kichiba, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, akiwa amemuwakilisha Mkurugenzi mkuu, amewashukuru wageni hao kwa kufika Bugando na kwa mchango wao katika kuboresha huduma za upasuaji.
“Sisi kama Hospitali ya Bugando tuko tayari kufanya kazi pamoja nanyi kwani mashirikiano haya yana tija kwa taasisi lakini pia kwa wagonjwa tunaowahudumia,” amesema Dkt. Kichiba.
Kwa upande wake, Prof. Lorry Akoko, Mkurugenzi wa COSECSA Tanzania, amewahimiza watoa huduma za upasuaji sanifu kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa huduma hizi, na kuwahamasisha wataalamu chipukizi kujikita katika fani ya upasuaji rekebishi (Reconstructive Surgery) kwa maendeleo ya sekta ya afya nchini.
Ziara hii ni ishara ya dhamira ya pamoja ya taasisi za afya za kikanda na kimataifa katika kuboresha huduma za upasuaji kwa jamii ya Afrika Mashariki na Kati.
WATUMISHI WA HOSPITALI YA BUGANDO WAKUMBUSHWA WAJIBU NA HAKI.
..
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga leo Oktoba 1, 2025 ameendesha kikao na makundi ya kada mbalimbali lengo likiwa ni kuboresha na kuimarisha huduma zitolewazo na Hospitali kwa Wananchi.
Sr. Dkt. Massenga amezungumza na kuwasikiliza Madaktari (madaktari wakazi-residents na registrars) pamoja na wauguzi ambapo amewashukuru kwa michango na ushirikiano wanaozidi kuuonesha katika kazi na amewataka Watumishi wote kuzingatia taratibu na kanuni za kazi wawapo kazini kwani utumishi umejikita katika kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa na Watanzania kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Watumishi wamekumbushwa matumizi ya lugha nzuri kwa wagonjwa pamoja na suala la uaminifu na uadilifu kazini.
Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani leo Septemba 29, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
..
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga amesema 20% ya watoto wanaozaliwa Bugando wanazaliwa na changamoto ya moyo na nusu yao wanahitaji upasuaji.
Sr. Dkt. Massenga amesema kwamba “hii ni kutokana na uelewa mdogo jambo ambalo hupelekea wagonjwa kufika Hospitali wakiwa wamechelewa hivyo tunapendekeza uwepo wa utoaji wa mafunzo endelevu na upimaji wa moyo katika vituo vya afya ili kupunguza changamoto ya wagonjwa kufika wakiwa wamechelewa”.
"Kila Pigo la Moyo ni Maisha, lilinde usilipoteze.”
RC MTANDA AHIMIZA WANANCHI KUBADILI MTINDO WA MAISHA ILI KULINDA AFYA YA MIOYO YAO.
..
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameyasema haya wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo Septemba 29, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, na kuwahasa wananchi kubadili mtindo wa maisha na kuzingatia lishe bora na kuepuka magonjwa ya moyo.
Akizungumza Katika maadhimisho hayo Mhe. Mtanda amesisitiza kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ikiwemo maradhi ya moyo yamekuwa chanzo kikuu cha vifo nchini na duniani kote, hali inayohitaji hatua za haraka.
Aidha, Mhe. Mtanda amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara na kutambua hali ya moyo wao mapema kabla ya kuathirika zaidi.
"Tusiishi kwa mazoea ya kwenda hospitali tu pale tunapougua, magonjwa ya moyo yanaweza kuzuilika iwapo tutajenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara na kuchukua hatua mapema," amesema Mhe. Mtanda.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Jesca Lebba amewaasa wananchi kuepuka maisha bwete kwa kufanya mazoezi, kuzingatia elimu lishe zinazotolewa na Wataalam ili kuepukana na Magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakikua kwa kasi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga amesema 20% ya watoto wanaozaliwa Bugando wanazaliwa na changamoto ya moyo na nusu yao wanahitaji upasuaji.
Sr. Dkt. Massenga amesema kwamba “hii ni kutokana na uelewa mdogo jambo ambalo hupelekea wagonjwa kufika Hospitali wakiwa wamechelewa hivyo tunapendekeza uwepo wa utoaji wa mafunzo endelevu na upimaji wa moyo katika vituo vya afya ili kupunguza changamoto ya wagonjwa kufika wakiwa wamechelewa”.
Maadhimisho haya yalianza na matembezi ya hisani yanayohamasisha kulinda afya za moyo, uchunguzi wa moyo ambapo maadhimisho haya yamekuwa na kaulimbiu "Kila Pigo la Moyo ni Maisha, lilinde usilipoteze.”
MAFUNZO YA ELIMU YA UZAZI NA USIMAMIZI WA MATIBABU YA UZAZI YATOLEWA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA WA BUGANDO NA CUHAS.
..
Hospitali ya rufaa ya kanda Bugando kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya (CUHAS) wanaendesha Mafunzo kuhusu Elimu ya Uzazi na usimamizi wa Tiba, kwa wataalamu wa idara ya uzazi na vizazi wa Bugando na CUHAS.
Mafunzo haya yameanza rasmi Septemba 29, 2025 na yanategemewa kukamilika Oktoba 3,2025 yakitolewa na Dkt. Hugo Soto, mjumbe Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Afya ya Uzazi (RHRI) ,Chile. Yakiwa yameshirikisha idadi ya wanafunzi (49) kutoka nchi nane tofauti barani Afrika na yanatazamiwa kuwa na manufaa makubwa kwa watoa huduma wa kizazi na vizazi katika lengo wa kuimarisha huduma hizo kwa Watanzania.
Akiongea Katika uzinduzi wa Mafunzo hayo, Dkt. Samson Kichiba kaimu mkurugenzi wa Upasuaji Bugando akiwa amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bugando Sr. Dkt.Alicia Massenga amesema " Mafunzo haya ni ya msimu wa pili kwani mafunzo ya awali yalifanyika Novemba 2024 ambayo pia yalilenga kuwafikia watoa huduma hivyo niwaombe washiriki wote muitumie nafasi hii vyema kwa lengo la kuongeza ujuzi na weledi katika maeneo yetu ya kazi".
BUGANDO YATOA HUDUMA ZA AFYA KWA JESHI LA POLISI MWANZA NA FAMILIA ZAO.
..
Katika kuendelea kukabiliana na changamoto za homa ya ini pamoja na saratani ya mlango wa kizazi, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha huduma ya chanjo ya homa ya ini pamoja na uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi, kwa jeshi la polisi Mwanza pamoja na familia zao zoezi lililofanyika katika kituo cha Polisi cha Mabatini Mwanza.
Huduma hii imetolewa leo Septemba 24, 2025 ikiwa na madhumuni ya kutoa chanjo ya homa ya ini pamoja na uchunguzi wa awali wa viashiria vya saratani ya mlango wa kizazi ambapo huduma hizi zimeambatana na kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu bobezi wa Afya.
Aidha, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Aloyce W. Nyantora ambaye ni mwakilishi wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ameishukuru na kuipongeza Hospitali ya Bugando kwa kuendelea kutoa huduma nzuri kwa Watanzania kwani huduma hizi ni muhimu na kusema " ili tuweze kufanya kazi kwa weledi na umahiri lazima tuwe na Afya njema hivyo niwapongeze tena na niwaombe tuendelee kufanya kazi kwa ushirikiano ili tuweze kuwa na taifa lenye afya bora"
SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI (IAEA) LATEMBELEA BUGANDO KATIKA KUENDELEA KUKABILIANA NA UGONJWA WA SARATANI.
..
Katika kukabiliana na changamoto za ugonjwa wa Saratani, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata wasaa wa kutembelewa na wataalamu kutoka shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki Duniani (IAEA),kutathmini utayari wa Tanzania kukabiliana na ugonjwa wa saratani.
Wageni hawa wamepata fursa ya kutembelea Hospitali mbalimbali zinazitoa huduma za saratani ikiwemo Hospitali ya Bugando na kuonana na wataalamu na kujadiliana namna ya kudhibiti ugonjwa wa saratani pamoja na ukusanyaji wa taarifa zinazohusu huduma za saratani na afya kwa ujumla.
DEVELOPING PEDIATRIC UNITS’ ANTIBIOGRAMS
..
Workshop and launching of the Antimicrobial Stewardship (AMS) project through pediatric-specific Antibiogram (ABG) development and implementation, along with a weekly prospective audit and feedback mechanism at the University Hospital Bugando Medical Centre for the Catholic University of Health and Allied Health Sciences today, 23-9-2025.
The ABG project is led by Dr. Neema Kayange in collaboration with the BMC-AMS team, BMC staff, and CUHAS, working in the departments of Pediatrics, Laboratory, Pharmacy, Pediatric Oncology, IPC, and the Stanford Centre for Innovation in Global Health at Stanford University USA.
This workshop was opened by Dr. Bahati Wajanga, Director of Medical Services at BMC, representing the Director General, and closed by Prof. Peter Rambau, Deputy Vice Chancellor of Academic and Research Affairs at CUHAS, representing the CUHAS Vice Chancellor.
MAFUNZO YA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI YAHITIMISHWA RASMI BUGANDO
..
Hii leo Septemba 18 Septemba, 2025 Hospitali ya Bugando imehitimisha mafunzo kutoka kwa wataalamu wabobezi wa tathmini na ufuatiliaji kutoka wizara ya Afya, mafunzo yaliyoanza tarehe 01 Sepetemba, 2025 ambapo yamelenga kusadia upimaji wa utendaji kazi katika kuelekea maono ya 2050( Vision 2050).
Akihitimisha mafunzo hayo, Dkt. Bahati Wajanga, akiwa amemkaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga, amewashukuru wataalam pamoja na washiriki na kusema;
"Mafunzo haya tuliyopata ni msingi mkubwa sana yasiishie hapa, ni lazima tuyafanyie kazi ili tuweze kujua wapi tumetoka, tulipo na tunakoelekea katika kupima matokeo ya kile tunachokifanya. Wizara wametupa mafunzo haya na wote tunaona kazi kubwa iliyo mbele yetu kuandaa mpango kazi mpya ambao utaendana na hili, tuendelee na ushirikiano na uwajibikaji ili kuhakikisha jambo hili linaenda kwa kasi katika kufikia malengo ya Taasisi"
Moja ya Wawezeshaji wa mafunzo Dkt. Edrew Hamis, Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Wizara ya Afya amepongeza uongozi wa Bugando kwa kuona umuhimu wa mafunzo haya na ushirikiano mkubwa waliopata na kusema wanategemea utekelezaji uwe wa hali ya juu ili Bugando ikawe mfano na kituo cha kujifunza kwa Taasisi nyingine.
Mafunzo haya yametolewa na Bw. Kilwanila H. Kiiza (Mkuu na mfuatiliaji upimaji wa utendaji), akiwa ameambatana na DKt.Endrew Hamis (Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Mwandamizi na Bw.Evaristus Makota (Mshauri Mwandamizi na Mkufunzi wa Ufuatiliaji na Tathmini) katika kuhakikisha Bugando inaanzisha kitengo U&T (Mfumo wa ufuatiliaji na Tathmini).
HUDUMA ZA MOYO KWA WATOTO ZAENDELEA KUIMARISHWA BUGANDO.
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ikishirikiana na Hospitali ya watoto Lurie- Chicago, Marekani kupitia idara ya watoto kitengo cha magonjwa ya moyo inaendesha mafunzo kwa wataalamu wa afya wa ngazi mbalimbali kujengeana ujuzi na uwezo katika masuala mazima ya kugundua changamoto za magonjwa ya moyo kwa watoto.
"Ugunduzi huu wa magonjwa ya moyo kwa watoto wachanga utawakinga watoto wengi na madhara makubwa ya kupata matatizo ya moyo ya kudumu", amesema hayo Dkt.Julieth Kabirigi ambaye ni daktari bingwa bobezi kwa magonjwa ya moyo kwa watoto.
Naye Dkt. Colleen Fant, mratibu wa programu ya magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Hospitali ya watoto Lurie nchini Marekani amesema mafunzo haya yataongeza uwezo mkubwa kwa madaktari na wanafunzi kwani watoto wengi wataweza kupata msaada wa kitabibu mapema na kuepusha watoto kusafiri umbali mrefu kupata msaada wa matibabu hayo.
Hata hivyo, Dkt.Shivan Patel Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali ya Lurie, Chacago- Marekani amesema,changamoto ya ugonjwa wa moyo kwa watoto inakua kwa kasi, hivyo ameshauri wazazi kutoamini katika mila potofu badala yake kuwahi Hospitali kupata matibabu sahihi na kuokoa maisha ya watoto.
WANAWAKE 30 WANUFAIKA KATIKA KAMBI YA UCHUNGUZI NA UPASUAJI KWA NJIA YA MATUNDU MADOGO BUGANDO.
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha kambi ya wiki mbili kufanya uchunguzi na upasuaji kwa njia ya matundu madogo (Laparoscopy and Hysteroscopy) wa changamoto ya uzazi na maradhi mengine ya Wanawake wakishirikiana na Madaktari Bingwa kutoka nchini Marekani, chini ya ufadhili wa Shirika la Americares.
Akizungumza katika kambi hii Dkt. Fr. Paul Ngayomela, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi wa Hospitali ya Bugando amesema aina hii ya upasuaji inasadia kupona haraka tofauti na njia ya awali ya kupasua tumbo;
"Upasuaji huu umekua msaada mkubwa, kupitia matundu madogo tunatumia Kamera maalumu kuona ndani ya tumbo na ndani ya mfuko wa uzazi kuweza kutibu, kufanya upasuaji wa vimbe ndani ya mfuko wa uzazi, mimba zinazotungwa nje ya mfuko wa uzazi na changamoto nyingine za uzazi ambazo kwa kweli anayefanyiwa upasuaji huu anaweza kuruhusiwa hata baada ya siku moja, kupona haraka na kuendelea na shughuli za uzalishaji"
Dkt. Fr. Ngayomela ameongeza kuwa kambi hii imesaidia Wanawake 30 ambao wamefanyiwa upasuaji lakini tangu ianze huduma hii Bugando mwaka 2022, Wanawake zaidi ya 200 wamenufaika nayo na kuwasihi Wanawake wenye changamoto ya Uzazi na maradhi mengine ya Wanawake kufika Bugando kupata huduma hii ya upasuaji kwa njia ya matundu madogo ambayo inamsadia Mgonjwa kupona haraka na kuepukana na makovu makubwa kama angefanyiwa upasuaji wa kuchana tumbo.
BUGANDO, MENDING KIDS,& COSECSA KUANZISHA PROGRAMU YA UPASUAJI BOBEZI WA WATOTO KWA MATATIZO YA PUA, KOO NA MASIKIO.
..
Hii leo Septemba 16, 2025 Hospitali ya Bugando kupitia Madaktari wa Idara ya Pua, Masikio na Koo - ENT (Pediatric ENT Fellowship) imeendesha kikao kazi kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Chuo kikuu cha Mbarara Uganda, Mending Kids kutoka Calfornia Marekani na mwakilishi wa COSECSA ( College of Surgeons of East, Central and Southern Africa)
nchini pamoja na Chuo Kikuu cha CUHAS kujadili kuhusu kuanzisha programu ya udaktari wa upasuaji bobezi wa watoto - ENT chini ya Chuo cha CoSECSa.
Programu hii itakuwa ya kwanza Afrika Mashariki, Kati na kusini mwa Afrika ambapo Dkt. Ayal Wilner ameeleza lengo la Mending Kids ni kuhakikisha wanatatua changamoto za kiafya kupitia kuwezesha mafunzo na ujuzi kwa wataalamu ndani ya Afrika ambao wataweza kusaidia jamii na kuutoa kwa wengine sambamba na kuwezesha kupitia vifaa na ufadhili mwingine unaohitajika.
Kikao hiki kimeshirikisha Mkurugenzi Mkuu wa Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga kwa njia ya mtandao, Wataalam wa Mending Kids, Madaktari wa ENT Bugando, mwakilishi wa COSECSA na Chuo Kikuu cha CUHAS.
Kwa upande wa Chuo cha CUHAS, Prof. Peter Rambau amesema ni wazo jema na watazingatia miongozo katika kuhakikisha programu hiyo inaanzishwa kwani Chuo kitatoa ushirikiano kufanikisha hilo.
Pamoja na hayo, idara ya ENT inaendelea na kambi ya wiki moja ya upasuaji kwa watoto wenye changamoto Masikio(pua,masikio na koo) kupitia wataalamu wa Bugando na Mending Kids, kambi itakayodumu hadi tarehe 19 Sepetemba, 2025.
TIMU YA BUNGE SPORTS KLABU YATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO
.
Timu ya Bunge sports klabu kutoka Makao Makuu ya Nchi Dodoma, leo Septemba 15,2025 imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa wa saratani na kuendeleza mashirikiano mazuri na shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za serikali (SHIMIWI)
Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa huduma za tiba Bugando Dkt. Bahati Wajanga akiwa amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, ameipongeza timu ya bunge sports klabu kwa umoja wao na maono yao mema kwa wagonjwa lakini pia kwa ushiriki wao hasa katika shirikisho la michezo kwa Watumishi wa Umma
"Ugonjwa wa saratani ni kati ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanakuwa kwa kasi lakini pia gharama za matibabu yake ziko juu hali ambayo inasumbua wananchi na hasa walio na kipato cha chini, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imeendelea kutoa vifaa tiba pamoja na madawa lakini bado ipo haja ya kuunga mkono jitihada hizi, ambapo Hospitali ya Bugando imeamua kuanzisha Marathon msimu wa pili kwa lengo la kusaidia wagonjwa wa saratani na mbio hizi zinatarajiwa kufanyika mapema mwezi Novemba, 2025 na kuomba wanamichezo waweze kushiriki kikamilifu katika mbio hizo ili kurejesha tabasamu kwa wagonjwa" ameeleza hayo Dkt. Bahati Wajanga
Aidha, Bwn. Waziri Kizingiti ambaye ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo kwa Watumishi tawi la Bunge ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa kuendelea kutoa huduma nzuri na njema kwa wagonjwa lakini pia kwa kuwapokea na kuwaruhusu kuwatia moyo wagonjwa japo kwa majitoleo yao mbalimbali kwani hii ilikuwa ni tamanio lao kuweza kufanya majitoleo hayo.
BUGANDO YAENDELEA KUREJESHA TABASAMU KWA WATOTO WA MDOMO WAZI NA MDOMO SUNGURA.
.
Shirika la Smile Train kwa kushirikina na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wametoa mafunzo kwa wataalamu wa afya yanayofahamika kwa jina la “Nursing Care Saves Life” kwa wauguzi waliopo wodini,vyumba vya upasuaji, madaktari, pamoja na wataalamu wa usingizi.
Malengo ya mafunzo haya ni kuwapa wataalamu wa afya ujuzi zaidi wa kuwahudumia watoto wenye mdomo wazi kabla,wakati na baada ya upasuaji.
Changamoto za watoto wenye midomo wazi zilijadiliwa kwa kina mojawapo ikiwa ni changamoto ya lishe, katika mafunzo haya pia wataalamu hawa wamefundishwa namna bora ya kuwaelekeza wazazi au walezi wa watoto hawa namna ya kuwalisha watoto wao kabla na baada ya upasuaji.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo haya amesema amefurahi kupata mafunzo haya kwani hakuwahi kufahamu kama watoto wenye mdomo wazi wanapitia changamoto walizojifunza katika ukuaaji wao.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inatoa shukrani kwa shirika la Smile Train kwa mafunzo ya nadharia na vitendo yaliyo tolewa kwa wataalamu mbalimbali ndani ya Taasisi.
MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO YATOLEWA KWA WATUMISHI WA TIBA NA MAFUNZO.
.
Idara ya Afya ya akili leo Septemba 2,2025 kupitia kitengo cha saikolojia kimeendesha mafunzo kwa watumishi wa Tiba na matunzo (CTC ) juu ya kukabiliana na msongo wa mawazo kwa wagonjwa pindi wanapokuwa wakiwahudumia.
Lengo la mafunzo haya likiwa limelenga kuwajengea uwezo watumishi wa idara hiyo ili kuweza kuleta mazingira mazuri ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika eneo la kazi.
Sambamba na hayo Mkuu wa kitengo cha Saikolojia Bw.Justine Maghina amewaomba viongozi kujenga tabia ya kugundua changamoto mbalimbali walizonazo watumishi na kuwa chanzo cha kusaidia kumaliza changamoto kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuwasaidia watumishi kukabiliana na wagonjwa wenye changamoto ya msongo wa mawazo.
MAFUNZO YA KUWAHUDUMIA WAGONJWA WANAOSUMBULIWA NA MARADHI KWA MUDA MREFU
.
Watoa huduma wa idara ya Saratani pamoja na wahudumu wengine wa afya Bugando watunukiwa vyeti baada ya kuhitimisha mafunzo ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu(Tiba Shufaa-Palliative Care Treatment).
CHANJO YA HOMA YA INI
..
Huduma ya upimaji na chanjo ya homa ya ini zinapatikana katika Banda la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
JARIDA LA "TABASAMU JIPYA" LAZINDULIWA BUGANDO, KUSAIDIA MATIBABU YA MDOMO WAZI NA MDOMO SUNGURA
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando hii leo Agosti 11, 2025 kupitia timu ya matibabu jumuishi ya mdomo wazi na mdomo sungura imezindua rasmi jarida la TABASAMU JIPYA lenye taarifa mbalimbali za matibabu ya mdomo wazi na mdomo Sungura ikiwemo elimu, shuhuda za waliopona, hatua za matibabu na kurejesha tabasamu kupitia matibabu yanatolewa kwa wenye changamoto hii.
Matibabu haya muhimu na ya kipekee nchini yanayotolewa na timu hii ya wataalamu wa Bugando kwa kushirikiana na wadau mbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi, matibabu haya jumuishi yalianza kutolewa mwaka 2021 na mpaka sasa yametolewa kwa zaidi ya watu 1000.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Idara ya Upasuaji Sanifu na Mkuu wa timu hii Dkt. Francis Tegete amesema ushirikiano mkubwa baina yao ndiyo nguzo katika kufanikisha matibabu haya na jarida hilo limelenga kuhamasisha, kuponesha, kuonesha ubunifu na ufumbuzi, ushirikiano na wadau wa ndani ya nchi na nje hivyo jarida hilo linatoa tabasamu.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Samson Kichiba ambaye pia yupo kwenye timu, amesema jarida hili ni kielelezo cha yale mengi na makubwa yaliyofanywa na timu hii kwani matibabu haya ni ya kipekee nchini kufanyika kwa ujumuishi, na Taasisi imekuwa mfano kwa wengine kuja kujifunza namna huduma hii imekuwa ikitolewa mpaka kwenye ngazi ya jamii na kusadia watu wengi zaidi.
Katika uzinduzi huu, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga ameipongeza timu hiyo kwa wazo zuri, ubunifu na jitihada za dhati kuwafikia na kuwasaidia wagonjwa hawa na kusema "Tunawashukuru sana timu hii kwa majitoleo haya, maana kwa hakika ni zaidi ya sadaka mnachokifanya, kupitia ushirikiano huu siyo jambo rahisi kufikia mafanikio haya, mmetuheshimisha na nyie ndiyo mnatubeba na niwaombe Idara nyingine kuiga mfano huu katika miradi mbalimbali mnayotengenza kuwa na timu yenye kada mbalimbali ili kufikia malengo kwa ufanisi zaidi, hongereni sana".
BUGANDO YAPIGWA MSASA KWA MAFUNZO YA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI.
..
Viongozi wa hospitali ya Bugando wamepata wasaa wa kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu wabobezi wa tathmini na ufuatiliaji kutoka wizara ya afya mafunzo ambayo yatasaidia katika upimaji wa utendaji kazi katika kuelekea maono ya 2050( Vision 2050).
Mafunzo hayo yametolewa na Bw. Kilwanila H. Kiiza (Mkuu na mfuatiliaji upimaji wa utendaji) akiwa ameambatana na DKt.Endrew Hamis (Afisa Uafilishaji na Tathmini Mwandamizi na Bw.Evaristus Makota (Mshauri Mwandamizi na Mkufunzi wa Ufuatiliaji na Tathmini) katika kuhakikisha Bugando inaanzisha kitengo U&T.(Mfumo wa ufuatiliaji na Tathmini).
Dkt. Bahati Wajanga, akiwa amemkaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga, amewashukuru wataalamu hao kwani mafunzo hayo yatakwenda kuitoa Hospitali kya Bugando katika hatua moja kwenda hatua nyingine kwa kuhakikisha kunakua na mabadiliko katika ufuatiliaji na utendaji na kupunguza changamoto mbali mbali.
Mafunzo hayo yatakua ya siku kumi kuanzia tarehe 01, Septemba hadi Septemba 10, 2025.
Mafunzo hayo yameanza tarehe 02, septemba hadi Septemba 16, 2025.
HOSPITALI YA BUGANDO YAADHIMISHA SIKU YA HOMA YA INI DUNIANI KWA KUTOA CHANJO YA AWALI BURE.
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Homa ya Ini Duniani, ambayo hufanyika Julai 28, kila mwaka, huku wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Bugando wakitoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kupima, kupata chanjo na elimu juu ya ugonjwa huo, ambao ni hatari usiotambulika kwa urahisi katika hatua za awali.
Akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo yamefanyika Katika kliniki ya Madaktari Bingwa Bugando iliyopo Nera jijini Mwanza, Dkt. Davidi Majinge, daktari bingwa na bobezi wa magonjwa ya mfumo wa chakula na ini, amesema; “lengo ni kuifanya jamii kufahamu zaidi kuhusu homa ya ini na kuweza kuweka mikakati ya kupambana na maambukizi ya homa ya ini duniani, kwasababu imeonekana homa ya ini nitatizo kubwa duniani na kwasababu kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla imeonekana ni changamoto, na madhara ni makubwa ambayo hupelekea saratani ya homa ya ini, kutokana na ongezeko hilo ili kupunguza janga hili tumekuja na kampeni tunapima homa ya ini bila malipo na chanjo ya awali, pia akiendekea kwa kutoa mfano, chanjo ya kwanza imetolewa leo ya pili baada ya mwezi mmoja na yatatu baada ya miezi sita nahii itakuwa kinga ya kupata homa ya ini na zaidi ya haya tumelenga kuwafikia zaidi ya watu 700.
Kwa upande wake, Dkt. Mathias Mlelwa kutoka chuo kikuu cha kikatoliki cha Sayansi za Afya (CUHAS) anbae ni mtaalam wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na hasa virusi, ameeleza kuhusu aina kuu za homa ya ini na takwimu zilizopo nchini Tanzania.“Kuna aina sita za homa ya ini: A, B, C, D , E na G. Aina hatari zaidi zinazochangia vifo vingi ni hepatitis B na C, ambazo huambukizwa kwa njia ya damu au majimaji ya mwili,” ameeleza Dkt. Mlelwa.
MAFUNZO YA USINGIZI NA GANZI SALAMA YATOLEWA KWA WATAALAM WA AFYA BUGANDO
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa kushirikiana na kampuni ya Vifaa ya Afya ya Competech Healthcare na GE Healthcare (GEHC) kutoka nchini Marekani, imeendesha mafunzo ya matumizi ya vifaa vipya vya kisasa vya usingizi na ganzi salama kwa Madaktari na Wauguzi wa Idara mbalimbali katika Hospitali ya Bugando.
Mkuu wa Idara ya Usingizi na Ganzi Salama wa Bugando Dkt. Rebecca Shija amesema mafunzo haya ya siku mbili yamelenga kuongeza ujuzi kwa Wataalam wa Afya Bugando kumhudumia Mgonjwa kabla, wakati na baada ya upasuaji na hata Mgonjwa mahututi.
"Hii itaboresha utoaji huduma kwa Wagonjwa, ukizingatia vifaa hivi vinakuja kuongeza ufanisi haswa katika kutambua hali ya Mgonjwa baada ya kupatiwa dawa, kiwango cha lishe anachotakiwa kupata akiwa mahututi na faida nyingine ambazo kwa kweli itaongeza ufanisi mkubwa" amesema Dkt. Rebecca Shija.
Mafunzo haya ya siku mbili (tarehe 14-15 Agosti, 2025) yametolewa kwa jumla ya Madaktari na Wauguzi 35 wa Idara tofauti katika Hospitali ya Bugando.
WATUMISHI WA BUGANDO WAKUMBUSHWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Sr. Dkt Alicia Massenga ameendesha kikao cha watumishi mapema leo Julai 28, 2025 kujadili mipango mikakati mbalimbali ya namna ya uendeshaji wa huduma ndani ya Hospitali.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Sr. Dkt Alicia Massenga ameendesha kikao cha watumishi mapema leo Julai 28, 2025 kujadili mipango mikakati mbalimbali ya namna ya uendeshaji wa huduma ndani ya Hospitali.
Akizungumza katika kikao hicho Sr. Dkt Massenga amewapongeza wafanyakazi kwa kuendelea kufanya kazi nzuri hususani katika kuwahudumia wagonjwa huku akisisitiza wawe na maadili na uadilifu wakati wa utendaji kazi nakusema
"Sisi kama viongozi wenu tunaomba ushirikiano na ushauri wenu kwani uongozi ni dhamana hivyo tufanye kazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu huku tukiongeza ubunifu ili tuweze kufika kule tunapotamani kufika na kufikia malengo ya Taasisi kwa ujumla"
Naye, Profesa Erasmus Kamugisha ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo cha CUHAS amempongeza Sr. Dkt. Alicia Massenga kwa kuteuliwa na kuaminiwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kuongoza Taasisi ambayo inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na chuo cha CUHAS pamoja na MWACHAS lakini pia amewapongeza wakurugenzi mbalimbali walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali ndani ya taasisi akiwemo Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dkt. Samson Kichiba, na Mkurugenzi wa fedha Fr. Martin H. Sumbi.
Pia, amempongeza na kumshukuru Dkt. Bahati Wajanga ambaye amekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu katika kipindi cha mchakato wa kupata Mkurugenzi Mkuu na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano kwani Jumuiya ya Bugando inafanya kazi kwa kushirikiana na kwa kutegemeana.
BUGANDO KUIMARISHA HUDUMA ZAKE KUPITIA MAFUNZO YA KIMKAKATI YA VIWANGO VYA KIMATAIFA YA UKAGUZI WA NDANI.
..
Viongozi wa Hospitali ya Bugando leo Septemba 09, 2025 wamepata fursa ya kupata mafunzo kuhusu miongozo, kanuni na taratibu za ukaguzi wa ndani yakiwa na lengo la kuimarisha utendaji. Mafunzo haya yametolewa na CPA Alphonce Muro (Mkufunzi) akiwa ameambatana na CPA Tadei Lujuo mjumbe wa kamati ya ukaguzi Bugando.
Mafunzo hayo yamebeba dhamira ya kujenga uelewa shirikishi wa jukumu la ofisi ya ukaguzi wa ndani katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yao katika kuhakikisha huduma Bora zinaendelea kutolewa kwa wagonjwa na jamii kwa ujumla.
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO NA WADAU WA AFYA WAFANYA MAKABIDHIANO YA SAMPULI ZA UTAFITI WA VIASHIRIA VYA VIRUSI VYA UKIMWI (THIS).
...
Wadau wa sekta ya afya — wakiwamo U.S. CDC Tanzania, ICAP, Maabara ya Taifa pamoja na Wizara ya Afya wametembelea Hospitali ya Bugando leo Agosti 5, 2025 na kufanya makabidhiano ya sampuli zilizotumika katika utafiti wa viashiria na matokeo ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI (THIS).
Kwa kipindi cha 2022–2023, maabara ya Bugando ilikuwa ni maabara kuu ya upimaji na hifadhi (biorepository) ya sampuli za THIS, zilizokusanywa kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kusimamiwa na ICAP kwa msaada wa CDC Tanzania kwa kupitia ufadhili wa PEPFAR.
Akifafanua katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Sr. Dkt. Alicia Massenga, amewapokea wageni hao na kuwashukuru kwa kuiamini Hospitali ya Bugando kama kituo kikuu cha utekelezaji wa mradi huo, uliochangia kuboresha huduma na uwezo wa kufanya tafiti.
Naye, Bw. Ambele Mwafulango, Kaimu Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa, aliwapongeza wadau na Hospitali ya Bugando kwa mchango wao mkubwa katika juhudi za kitaifa za kukabiliana na VVU kupitia utafiti wa THIS. Amesema,"sampuli hizo zimetumika kutathmini maambukizi ya UKIMWI nchini na kubaini maeneo muhimu zaidi kwa kuimarisha mikakati ya uingiliaji (interventions)" .
Kwa upande wake Dkt. George Mgomella, Mkurugenzi wa Miradi wa CDC Tanzania, aliitaja sifa ya ushirikiano uliopo baina ya Hospitali ya Bugando, ICAP na CDC kwani kupitia ushirikiano huo, huduma za ugunduzi na utambuzi wa usugu wa VVU dhidi ya dawa za kufubaza makali ya VVU ( HIV drug resistance) imeweza kufikia mikoa nane kanda ya Ziwa. Aidha, aliongeza kuwa hifadhi ya sampuli hizo ni muhimu endapo zitakuwa na matumizi ya baadaye katika tafiti nyingine zenye umuhimu kwa taifa.
MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI WA UPASUAJI BUGANDO WAKUMBUSHWA KUTEKELEZA WAJIBU NA MIONGOZO.
..
Mapema leo Agosti 14,2025 Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Sr. Dkt. Alicia Massenga amepata wasaa wa kuzungumza juu ya uboreshaji wa huduma za upasuaji na madaktari bingwa, bingwa bobezi na pia wataalamu wa usingizi wa Bugando pamoja kuwakuumbusha wataalamu hao kuhakikisha huduma za upasuaji zinaendelea kuimarika.
Akizungumza na wataalamu hao Sr. Massenga amesisitiza kuendelea kufuata miongozo ya kazi pamoja na kuhakikisha wataalamu hao wanaendelea kutunza na kuthamini vifaa vya upasuaji.
Akimuawakilisha Prof. Erasmus Kamugisha Makamu Mkuu wa chuo Kikiuu cha kikatoliki cha Sayansi za Afya CUHAS Prof. Peter Rambau
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo- Taaluma, Utafiti na Ushauri Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya CUHAS amesema "Wataalamu wa upasuaji ni watu muhimu sana katika hospitali na hivyo amewaasa pale zinapopatikana nafasi za masomo, kuzitumia lakini pia kuhakikisha wanawajengea uwezo wataalamu ambao wapo chini yao kwani ndio Bingwa na Bingwa bobezi wa baadae".
Sambamba na hayo Kaimu Mkurugenzi wa Upasuaji Bugando Dkt. Samson kichiba, amewapongeza kwa kazi wanazozifanya na pia amewakumbusha wataalamu hao kuendelea kufanya kazi kwa weledi hasa katika kuhakikisha wanaendelea kuboresha afya za watanzania kwakutoa huduma za kibingwa na bingwa bobezi zinazoendana na nyakati hizi.
Bodi ya utawala ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jumatano ya leo tarehe 27 Agosti, 2025 imekagua moja ya miradi ya Hospitali.
..
Bodi ya utawala ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando jumatano ya leo tarehe 27 Agosti, 2025 imekagua moja ya miradi ya Hospitali.
HOSPITALI YA BUGANDO KUPOKEA MASHINE YA FLOW- CYTOMETRY INAYOTAMBUA MAGONJWA YA DAMU.
Mkurugenzi wa huduma za maabara na patholojia kutoka shirika la Global HOPE Texas, Baylor's college of Medicine na Profesa wa magonjwa ya watoto na damu Dkt. Julie M. Gastier- Foster,(PhD, FACMG) kutoka Nchini Marekani
wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Agosti 7, 2025 na kuona eneo ambalo mashine ya Flow-cytometry itakaposimikwa ambayo itasaidia kutambua magonjwa mbalimbali ya damu ikiwemo saratani za damu.
Sambamba na ujio huu Dkt. Julie amesema licha ya kutembelea maabara pia wanalengo la kuendelea kuboresha huduma za kihistopatholojia pamoja na kutoa mafunzo yaliyojikita katika huduma ya uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya damu (flow cytometry) kwa watoto .
Nae Sr. Dkt. Alicia Massenga Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando amemshkuru Dkt. Julie kwa kufika Bugando na kuendelea kudumisha ushirikiano wao uliojengeka katika kuboresha matibabu kwa wagonjwa kwani hospitali ipo tayari kufanya kazi kwa pamoja pia inashukuru kwa uwekezaji wa mashine kwani itasaidia upatikanaji wa huduma za uchunguzi na kuondoa adha mbalimbali kwa wagonjwa.
Pamoja na hayo, Dkt. Nestory Masalu Mkuu wa Idara ya saratani Bugando ameeleza kuwa Idara ya saratani inafanya kazi kwa ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo chuo cha Duke, Global HOPE, St. Jude children's research hospital, BMSF, TLM ambapo ushirikiano huo umejikita katika eneo la tafiti, mafunzo mbalimbali pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kazi (matibabu) na kwa sasa kupitia ushirikiano huo tuna malengo ya kuanzisha mafunzo ya uuguzi bobezi katika Idara ya saratani.
Pia Dkt. Julie amepata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Bugando ikiwemo eneo ambalo mashine hiyo itasimikwa ( Idara ya saratani), Maabara kuu, maabara ya histopatholojia, maabara ya vinasaba pamoja na Idara ya hemophilia.
BUGANDO YAENDELEA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA.
Washiriki na wawakilishi wa Miss Universe Tanzania 2025 kutoka Kanda ya Ziwa wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Leo julai 25, 2025 lengo likiwa kuchangia damu.
"Sisi ni washiriki na wawakilishi wa Kanda ya Ziwa tumeamua kufanya hivi kwasababu tuna lengo la kusaidia maisha ya watoto pamoja na watu wazima wenye uhitaji wa damu ambapo pia mimi mwenyewe hii ni moja ya ziara ya mradi wangu yenye lengo la kuchangia damu kwa wahitaji na hasa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa sikoseli" ameyasema hayo Samira Yassin ambaye ni Mshiriki wa fainali ya miss universe Tanzania.
Akizungumza katika ujio wa wageni hao Mkuu wa Idara ya Maabara Esther Reuben amewakaribisha na kuwapongeza washiriki hao kwa kujitoa kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu kwani damu ni uhai na kupitia zoezi hilo wataweza kusaidia wagonjwa wengi.
BUGANDO YAENDELEA KUPANUA WIGO WA KUWAFIKIA WAGONJWA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inaendesha mafunzo ya tiba shufaa (palliative care) kwa wafanyakazi wa Idara ya saratani
katika kuhakikisha inaboresha maisha ya wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya muda mrefu ikiwemo ugonjwa wa saratani.
Mafunzo haya yameanza rasmi Agosti 18 na yanatarajiwa kutamatika Agosti 29, 2025 ambapo Hospitali kupitia kitengo chake cha tiba shufaa (Palliative care) kina malengo mahususi ya kusaidia na kupanua wigo wa huduma hii kwa Idara zingine ambazo pia magonjwa yake ni ya muda mrefu kama vile ugonjwa wa UKIMWI, Kifua Kikuu, kisukari pamoja na Sikoseki ili wagonjwa waweze kupata huduma kamili na ya ubora kwa kuzingatia hali ya mgonjwa kimwili, kiakili na pia kijamii.
HOSPITALI YA BUGANDO YAPOKEA WATAALAM KUTOKA VENDERBELT UNIVERSITY KWA AAJILI KAMBI MAALUM YA UPASUAJI WA MFUMO WA FAHAMU
Katika kutekeleza agizo la Serikali la mashirikiano baina ya mataifa ya nje kwa upande wa afya
, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa fahamu kutoka Chuo Kikuu cha Vanderbelt cha nchini Ujerumani. Wataalamu hawa wamekuja Hospitali ya Bugando kushirikiana na Wataalam wetu kwaajili ya kambi maalumu ya upasuaji wa mfumo wa fahamu kwa lengo la kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa mgongo na mfumo wa fahamu waliokuwa wakihitaji huduma za kibingwa, kutoa mafunzo ya vitendo na nadharia kwa madaktari, kuchangia vifaa tiba vya kisasa vinavyosaidia katika tiba za mishipa ya fahamu.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Sr. Dr. Alicia Massenga amewakaribisha kwa furaha na shukrani za dhati kwa ujio wao na kutambua mchango wao mkubwa katika kuboresha huduma za afya, huku akisisitiza umuhimu wa mashirikiano ya kimataifa katika kuleta mabadiliko endelevu kwenye sekta ya afya na Taifa kwa ujumla.
“Tumefarijika sana na ujio wenu, si tu kwa ajili ya huduma mtakazotoa, bali kwa mafunzo mliyokuja kushirikisha na vifaa vya thamani mliyotuletea. Ushirikiano huu ni msingi wa maendeleo ya afya duniani, pia kambi hii si tu kutoa huduma, bali ni nafasi ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha uwezo wetu wa ndani,” amesema Sr. Dkt. Massenga.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dkt. Samson Kichiba amesema; “Tunawakaribisha na kuwashukuru kwa kutuletea vifaa vya upasuaji ambayo vitakuwa na manufaa kwa jamii yote ya kitanzania itakayokuwa inakuja hapa Hospitali ya Bugando kupata matibabu haya ya mfumo wa fahamu. Sisi tunachoomba muendelee kuwa na mashirikiano na wataalamu wetu huku mkiwapa mafunzo yatakayosaidia wagonjwa katika Taifa letu la Tanzania” amesema Dkt. Kichiba.
Kwa upande wake Dkt. Christopher Bonfield kutoka Chuo kikuu cha Venderbelt nchini ujerumani amesema, “sisi pia tunajihisi furaha kuwa na mashirikiano nanyi kwa madaktari na wauguzi wetu kupeana ujuzi katika kazi tumeona umuhimu katika upasuaji wa mfumo wa fahamu mahitaji ni makubwa.
BUGANDO YAPOKEA PONGEZI KWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA NZURI KWA WAGONJWA.
Ikiwa ni Jubilee ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kwaya ya Mtakatifu Yuda Thadei Epifania
Bugando Leo Julai 20, 2025 wametembea Wagonjwa wa fistula katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo likiwa ni kutoa matendo ya huruma kwa wagonjwa.
Akizungumza katika mapokezi ya kwaya hiyo Bi. Dativa Munishi ambaye ni Muuguzi katika wodi ya akina mama ameishukuru kwaya hiyo na kuipongeza kwaya hiyo kwa kutimiza miaka 25 ya utume na majitoleo yao kwa wagonjwa kwani kwa kufanya hivyo wameweza kurejesha tabasamu katika nyuso za wagonjwa na kutimiza agano la Mungu
Aidha, mwenyekiti wa kwaya Bwn. Gozbert Mugisha ameupongeza uongozi pamoja na wafanyakazi wa Hospitali kwa kuendelea kutoa huduma njema na nzuri kwa wagonjwa
WAUGUZI WAKUMBUSHWA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO
Wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wamekumbushwa kuimarisha uwajibikaji
Wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wamekumbushwa kuimarisha uwajibikaji ikiwemo kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya kazi na kutatua changamoto mara tu zinapotokea.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za uuguzi Bugando Sr. Salome Marandu aliyeongoza kikao kazi hiki kwa kushirikiana na wauguzi viongozi wa kila idara na lengo la kikao hiki ni kujadili na kusikiliza hoja mbalimbali za wauguzi ili kuendelea kuboresha huduma zitolewazo hospitalini hapa.
Akizungumza katika kikao hicho Sr. Marandu amewapongeza wauguzi kwa ushirikiano na bidii wanayoiyonesha kazini ili kuhakikisha matibabu ya mgonjwa yanakamilika na kusema " hospitali inatambua mchango, jitihada na bidii mnazozionesha katika utendaji kazi wenu na kiu ya kuhakikisha mgonjwa anapata matibabu stahiki na kufikia malengo ya taasisi, kwa niaba ya menejimenti niahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa kuzitatua changamoto mlizoziwakilisha hapa”.
Sambamba na hayo Sr. Salome amewakumbusha wauguzi kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo na taratibu za kazi, weledi wa hali ya juu pindi wawapo kazini na kusisitiza uaminifu na uadilifu.
Pia wauguzi wameahidi kuwa sehemu ya kupata Bilioni moja ya matumaini na kushiriki kikamilifu katika mbio ya Bugando Health Marathon msimu wa pili itakayofanyika tarehe 03/08/2025, na kwakuanza tayari wamejisajili kushiriki mbio hii na kuchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya saratani.
Sambamba na hayo wameushukuru uongozi wa Bugando kwa kutoa nafasi ya kikao hiki na kusikiliza hoja na changamoto zao na kusema kikao hiki kitaongeza ufanisi na ushirikiano katika kazi.
DESK AND CHAIR FOUNDATION WATOA VITI MWENDO VYA KUBEBEA WAGONJWA 12 KWA WAGONJWA WA SARATANI BUGANDO
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr. Salome Marandu amepokea msaada wa viti mwendo
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr. Salome Marandu amepokea msaada wa viti mwendo vya kubebea Wagonjwa (wheelchair) kutoka kwa shirika la kijamii la Desk and Chair Foundation hii leo Julai 14, 2025 Kwa ajili ya kubebea watoto na watu wazima katika Wodi ya Saratani. Akikabidhiwa jumla ya viti vya kubebea Wagonjwa 12 vyenye thamani ya Tsh 4,200,000/= Sr. Marandu amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo muhimu, huruma na ukarimu wao wa kuona uhitaji mkubwa wa viti kwa Wagonjwa wa Saratani kwani vitasadia kurahisisha kuhudumiwa kwa wagonjwa, itagusa maisha yao moja kwa moja na Mungu atawaongezea zaidi.
Wizara ya Afya na Shirika la CDC Tanzania wametembelea Idara ya maabara ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Wizara ya Afya nchini ikishirikiana na shirika la CDC Tanzania pamoja na wadau wa maendeleo MDH
Wizara ya Afya nchini ikishirikiana na shirika la CDC Tanzania pamoja na wadau wa maendeleo MDH Leo July 11, 2025 wametembelea Idara ya maabara ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kufanya ukaguzi na usimamizi shirikishi ili kuendelea kuboresha huduma za uchunguzi wa usugu wa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI ( HIV Drug Resistance).
Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi wa Hospitali ya Bugando Dkt. Cosmass Mbulwa, amewakaribisha na kuwapongeza wataalamu hao kwa kuweza kutembelea Idara ya maabara kwani wameweza kubaini maeneo mbalimbali yanayohitaji maboresho zaidi ili kuendelea kutoa huduma nzuri zaidi.
Aidha, kwa upande wa wageni hao wameendelea kutoa pongezi kwa Hospitali ya Bugando kwa jitihada na kazi nzuri wanayoendelea kuitoa na hasa kwa upande wa maabara na wageni hao wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili wafike kule wanapotamani kufika.
Bugando Katika kuboresha huduma za dharura pamoja na jitihada mbalimbali
Shirika la Abbott Fund Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Katika kuboresha huduma za dharura pamoja na jitihada mbalimbali za kuwezesha watumishi wa afya wa kada mbalimbali kupata mafunzo ya namna ya kuhudumia wagonjwa wa dharura,
Shirika la Abbott Fund Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, leo wamekabidhiwa rasmi eneo kwa kuwezesha ujenzi wa maabara ya kisasa (Emergency Medicine training skills laboratory) ya kufundishia mafunzo ya huduma za dharura.
Dhamira kubwa ya maabara hiyo ni kuwezesha wanafunzi wa vyuo, watumishi wa sekta ya afya wa kada mbalimbali wa mikoa inayoizunguka Hospitali ya Bugando kuweza kusogezewa mafunzo hayo karibu zaidi badala ya kuhitajika kusafiri umbali mrefu kuyapata Mafunzo.
Maabara hii itasimikwa na miundombinu na vifaa vya kisasa vya kuendesha mafunzo hayo kwa vitendo na kwa njia ya mtandao.
BMC inashukuru jitihada za serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Afya kuwa na maono makubwa kwa ajili ya fani ya huduma za dharura nchini.
Mhe. MHAGAMA (MB) ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO.
WAZIRI WA AFYA, MHE.JENISTA MHAGAMA (MB) ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO.
Mhe.Jenista Mhagama (Mb) ametembelea Hospitali ya Bugando leo juni 17, 2025 kwa lengo la kutoa mkono wa pole kwa majeruhi wa ajali iliyotokea wilaya ya Meatu, mkoa wa Simiyu ambapo majeruhi hao wanapatiwa matibabu na madaktari bingwa na wanaendelea vizuri.
Mhe.Jenista Mhagama amepata wasaa wa kuongea na uongozi wa Hospitali ya Bugando na kuwapa pongezi kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kuomba wataalamu wote wa Afya kufanya kazi kwa ushirikiano ili taasisi izidi kukuwa.
Hata hivyo waziri wa Afya ameomba Hospitali kutumia vizuri uwekezaji mkubwa uliowekwa na serikali ili uzidi kuwa na manufaa kwa wananchi na kuwa tayari kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoyakuambukiza na kujikita zaidi Katika suala zima la tafiti ili kuleta majibu ya magonjwa mbalimbali.
Naye Kaimu mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt.Bahati Wajanga amefurahishwa na ujio wa Mhe.Jenista Mhagama na kusema kuwa uwekezaji wa miundo mbinu,vifaa tiba, madawa na wataalamu wa Afya walionufaika kupitia uongozi wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ni mkubwa na umekuwa na manufaa sana kwa Hospitali na wananchi kiujumla na kuahidi kuwa uwekezaji huo hautapotea bali utaleta manufaa makubwa zaidi.
BUGANDO YAENDELEA KUPOKEA WADAU, KUSAIDIA WATOTO WENYE SARATANI
.
BUGANDO YAZINDUA MSIMU WA PILI WA MBIO ZA BUGANDO HEALTH MARATHON, 2025
HOSPITALI YA BUGANDO YAZINDUA MSIMU WA PILI WA MBIO ZA BUGANDO HEALTH MARATHON, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni 14, 2025 amezindua msimu wa pili wa mbio za Bugando Health marathon katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando yenye kauli mbiu isemayo " Kimbia changia matibabu ya saratani" huku kilele cha siku ya mbio hizo za Bugando health Marathon msimu wa pili kufanyika Agosti 03, 2025.
Akiongea katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza bodi ya uendeshaji na uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa maamuzi yenye busara na yenye lengo la kusaidia wagonjwa wasio na uwezo kwa kugharamia matibabu yao ikiwa sambamba na kutoa shukrani kwa Clouds Media group kwa kuongeza hamasa, uelewa na ushawishi kwa jamii juu ya ugonjwa wa saratani,
"Ni dhahiri kwamba ugonjwa wa saratani unakua kwa kasi na hii imeonekana hata baada ya matibabu haya yalipoanza kutolewa hapa katika Hospitali ya Bugando ugonjwa huu unaonekana kuwa na gharama za juu kiasi ambacho baadhi ya Wananchi hawawezi kumudu gharama hizo hivyo nitoe rai kwa jamii na wananchi kwa ujumla kujitoa katika mbio hizi tukikusudia kuwasaidia Watanzania wenzetu mimi pia pamoja na ofisi ya Mkuu wa Mkoa tutatoa kiasi cha shillingi 5,000,000/=."
Aidha Dkt.Bahati ameishukuru Serikali ya jamhuri ya Muungano na pia wananchi kwa ujumla kwa juhudi zilizofanyika katika Marathon msimu wa kwanza kilifanikiwa kukusanya kiasi cha shillingi 222, 420,652.00 fedha ambayo ilitumika katika matibabu ya watoto 153 waliokuwa wanatoka katika familia duni, pia vifaa mbalimbali vilipokelewa vya kusaidia matibabu ya saratani vyenye thamani ya kiasi cha Tshs 77 millioni kutoka benki ya NMB na wadau wengine. “Ikumbukwe mbio hizi za msimu wa pili zimelenga kukusanya kiasi cha shillingi Billioni 1 ya matumaini ambapo fedha ya ushiriki ni shillingi 35,000/= kwa kila mshiriki".
SIGN FRACTURE CARE INTERNATIONAL YATOA VIFAA VYA KUTIBU MIFUPA , BUGANDO Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
SIGN FRACTURE CARE INTERNATIONAL YATOA VIFAA VYA KUTIBU MIFUPA , BUGANDO Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
SIGN FRACTURE CARE INTERNATIONAL YATOA VIFAA VYA KUTIBU MIFUPA , BUGANDO
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Juni 09, 2025, imepokea msaada wa seti 3 za vifaa vya kutibu mifupa (sign set 1, pelvis set 2, na sign nails 54) kutoka kwa Shirika la Sign Fracture Care International la nchini Marekani. Vifaa hivi vimepokelewa na uongozi wa Hospitali ya Bugando na kukabidhiwa kwa Mkuu wa idara ya mifupa Dkt. Andrew Nkilijiwa.
Akiongea katika makabidhiano hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Bahati Wajanga amelishukuru Shirika hilo kwa msaada huu muhimu, wa vifaa ambavyo vitatumika kutibu mifupa ilioyovunjika na kusaidia kuunganisha mifupa na kuhakikisha uponyaji sahihi kwa wagonjwa, pia vitaboresha huduma za afya kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya mifupa, hasa wale wanaopata majeraha makubwa kutokana na ajali au magonjwa yanayoathiri mifupa.
Sambamba na hayo ameongeza kuwa vifaa hivi vitasaidia kupunguza changamoto za ukosefu wa vifaa tiba na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wagonjwa wa mifupa. Pia amewataka wataalamu hawa, kutumia vifaa hivi kwa ufanisi ili kufikia malengo ya kuboresha huduma za afya kwa jamii katika kanda ya ziwa.
“Msaada huu ni mfano mzuri wa ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya afya, ambapo juhudi za pamoja zinasaidia katika kuboresha huduma za afya na kupunguza vifo vinavyotokana na majeraha ya mifupa. Hospitali ya Bugando inatarajia kuwa na athari chanya katika jamii kutokana na msaada huu, na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa kanda ya ziwa” amesema Dkt. Wajanga.
Chuo kikuu cha Duke cha nchini Marekani kwa kushirikiana na taasisi ya Healing the Children North East wamekabidhi mashine ya Automated external defibrillator na vifaa tiba vingine kwa Hospitali ya Bugando.
Chuo kikuu cha Duke cha nchini Marekani kwa kushirikiana na taasisi ya Healing the Children North East wamekabidhi mashine ya Automated external defibrillator na vifaa tiba vingine kwa Hospitali ya Bugando.
Chuo kikuu cha Duke cha nchini Marekani kwa kushirikiana na taasisi ya Healing the Children North East wamekabidhi mashine ya Automated external defibrillator na vifaa tiba vingine kwa Hospitali ya Bugando.
Kazi ya mashine hiyo ni kushtua mapigo ya moyo ambayo yapo chini au yakiwa yamesimama na kuyarudisha katika hali yake ya kawaida.
Kwaniaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dkt. Sr. Alicia Massenga Mkurugenzi wa Huduma za upasuaji amepokea vifaa hivyo na kushukuru taasisi hizi kwa kuwa na ushirikiano wenye tija na kuahidi kuendeleza ushirikiano huu ,kwani umezidi kuimarishwa haswa katika kurugenzi ya upasuaji.
Duke wamekuwa wakiendesha kambi za upasuaji kwa kushirikiana na Idara ya upasuaji sanifu na rekebishi na idara ya ENT(Idara ya koo,pua na masikio).
MAFUNZO YA KUONGEA(MATAMSHI) YATOLEWA KWA WALIMU KUSADIA WANAFUNZI WENYE CHANGAMOTO.
MAFUNZO YA KUONGEA(MATAMSHI) YATOLEWA KWA WALIMU KUSADIA WANAFUNZI WENYE CHANGAMOTO.
MAFUNZO YA KUONGEA(MATAMSHI) YATOLEWA KWA WALIMU KUSADIA WANAFUNZI WENYE CHANGAMOTO.
Hii leo Juni 05, 2025 Hospitali ya Bugando kupitia Idara ya Koo, Pua na Masikio kitengo cha Kuongea (matamshi) kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka nchini Marekani, wameendesha mafunzo ya kuongea na lugha kwa Walimu wa shule ya msingi Faith ya Wanafunzi wa kawaida na wenye mahitaji maalumu iliyopo Ilemela jijini Mwanza.
Mafunzo haya kwa Walimu yametolewa na Mtaalamu wa Kuongea(Matamshi) Adam Mang'ombe wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Prof. Blessly Mathews na Prof. Ysabella Hincapie wa nchini Marekani kutoka Chuo Kikuu Cha Duke.
Mtaalamu wa matamshi Adam Mang'ombe amesema Mwanafunzi ili apate uelewa mzuri anahitajika kuweza kuona, kusikia na kuongea ambapo kupitia mafunzo hayo ya kuongea kwa Walimu yatasaidia kuwalea na kuwasaida Watoto walio kwenye mahitaji Maalumu katika shule hiyo na jamii kiujumla.
Naye Prof. Blessly Mathews amesema ushirikiano huu katika kuwasaidia watoto katika Matamshi na uelewa darasani katika nyanja mbalimbali utakuwa endelevu kwani wameona uhitaji uliopo na umuhimu wa huduma hiyo ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu namna ya kuwasaidia Watoto wenye tatizo katika Matamshi na lugha.
Kwa upande wa Shibide Nyanda ambae ni Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Faith ameishukuru Hospitali ya Bugando na wataalamu hao hao kwa kutoa mafunzo muhimu kwa Walimu na kuomba yawe endelevu kwani yana msaada mkubwa katika kuwasaidia watoto wenye uhitaji maalumu wanaolelewa katika shule hiyo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanya kambi ya matibabu ya uchunguzi wa fistula ya uzazi na kuchanika msamba kwa wanawake
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanya kambi ya matibabu ya uchunguzi wa fistula ya uzazi na kuchanika msamba kwa wanawake
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanya kambi ya matibabu ya uchunguzi wa fistula ya uzazi na kuchanika msamba kwa wanawake waliopata changamoto wakati wa kujifungua,na kambi hii inahusisha madaktari Bingwa na Bingwa bobezi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Somalia, Uswizi , Ufaransa kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Bugando ili kujengeana uwezo, kubadilishana ujuzi na kurejesha tabasamu kwa wanawake wenye changamoto hiyo.
Kambi hii imeanza juni 2 , 2025 na inatarajia kumalizika Juni 7, 2025.
MAADHIMISHO YA SIKU YA HUDUMA ZA DHARURA DUNIANI YAFANA BUGANDO.
MAADHIMISHO YA SIKU YA HUDUMA ZA DHARURA DUNIANI YAFANA BUGANDO.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeungana na dunia kuadhimisha siku ya Huduma za Dharura Duniani(World Emergency Day) hii Leo Mei 27, 2025, maadhimisho yaliyohudhuriwa na viongozi , wadau wa maendeleo na wananchi yakiwa na kaulimbiu ya "Fahari Kutoa Huduma Yako Ya Dharura ".
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo, Dkt. Bahati Wajanga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando na Mgeni Rasmi amepongeza Idara ya Dharura kwa maadhimisho mazuri na kusema;
"Niwashukuru Idara ya Dharura kwa kufanya maadhimisho haya muhimu yanayoonesha jinsi gani huduma zinazotelewa katika Idara hii ni muhimu, huwa tunasema Idara ya Dharura ni kioo cha Hospitali, ndilo eneo Mgonjwa anakofika kwa mara ya kwanza kuhudumiwa na linaonesha ni namna gani tuko tayari katika kutoa huduma bora, mmetoa mafunzo kwa watu mbalimbali ambayo yatakuwa chachu ya kuendelea kutoa huduma bora kuanzia ngazi ya jamii, kama Hospitali tumeendelea kupata mrejesho bora kutoka kwa wananchi juu ya huduma za Dharura, hatutakiwi kubweteka bali kuendelea kuwa kioo na kuwalea wengine katika mafunzo na kukaza buti zaidi katika kutimiza lengo kwa kutoa huduma bora za Afya, hongereni sana". Amesema Dkt. Wajanga
Naye Mkuu wa Idara ya Huduma za Dharura Dkt. Shahzmah Suleman ameushukuru uongozi wa Hospitali, wadau wa maendeleo na zaidi Serikali kwa juhudi zilizoelekezwa katika kuimarisha huduma za Dharura ambazo zimewezesha kuwa na wataalamu, vifaa vya kisasa na mafunzo kwa wataalamu ambayo yote imekuwa nyenzo katika kutoa huduma bora kwa Mgonjwa wa dharura.
Maadhimisho haya yamehitimisha wiki ya Dharura ambapo Idara ya Dharura iliitumia kutoa elimu ya huduma ya kwanza na usalama kwa kwa Wanafunzi, Walimu, Walinzi (SUMA JKT) Watoa huduma za Afya na Madereva.
WANAFUNZI WAPEWA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA NA USALAMA KWA JAMII
WANAFUNZI WAPEWA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA NA USALAMA KWA JAMII
Kuelekea siku ya Huduma za Dharura Duniani tarehe 27 Mei 2025, Hospitali ya Bugando kupitia Idara ya Dharura imetoa mafunzo ya huduma ya kwanza na usalama kwa jamii kwa baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlimani ya Jijini Mwanza hii leo Mei 21, 2025, mafunzo yanayoratibiwa kitaifa na Chama cha Madaktari wa Huduma za Dharura Tanzania (EMAT).
Katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Dkt. Christina Asheely wa Idara ya Dharura katika Hospitali ya Bugando kwa Wanafunzi 15 na Walimu wawili wa Shule hiyo, yamelenga kuwapa uelewa Wanafunzi juu ya kutoa huduma ya kwanza kwa usahihi na kwa wakati sambamba na kwenda kuwa mabalozi wa mafunzo waliyoyapata kwa wengine na kwa jamii kiujumla.
Akizungumza baada ya mafunzo, Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mlimani Kipeja Elias amesema “tunawashukuru sana Bugando kwa mafunzo haya muhimu mliyotupatia, hakika mmepanda mbegu katika safari ya maisha ya watoto hawa na jamii, mafunzo ni mazuri na yatawasaidia wao wenyewe, wengine na kwa jamii kwa ujumla, asanteni sana” Idara ya Dharura inaendelea kutoa mafunzo kwa jamii, yote ni kuelekea siku ya huduma za dharura duniani itakayoadhimishwa tarehe 27 Mei, 2025 yakiwa na Kaulimbiu isemayo “fahari kutoa huduma yako ya dharura”.
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA MATIBABU YA SARATANI.
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA MATIBABU YA SARATANI.
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imejizatiti kuwekeza katika uchunguzi na matibabu ya Saratani kwa kuhakikisha kunakuwepo na wataalamu wenye ujuzi ili kuendana na uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kuanzia mwaka 2022, ikiwemo kununua mashine za Kisasa za uchunguzi wa Saratani katika Hospitali za Mikoa na za Rufaa kote nchini lengo likiwa ni kuwasogezea huduma wananchi. ambapo sasa wananchi wanaweza kufanyiwa uchunguzi kwa wakati na kupata matibabu stahiki jambo ambalo linaokoa idadi kubwa ya wagonjwa ambao walikua wanafika hospitali wakiwa katika hatua za mwisho na kushindwa kutibika.
Haya yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya Dr. Omary Ubuguyu wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya Wataalamu wa utambuzi wa picha za mionzi za uchunguzi na matibabu ya saratani kutoka Hospitali za Mikoa na Rufaa Tanzania yaliyofanyika katika Hospitali ya Bugando. Dkt. Ubuguyu amebainisha "ufungaji wa mashine za CT scanner katika hospitali zote za Mikoa, na Rufaa za Kanda, MRI mashine kwa hospitali za Kanda na Taifa ni ushuhuda wa Serikali ilivyojizatiti dhidi ya Saratani" Dkt. Ubuguyu
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt. Bahati Wajanga amepongeza washiriki na kuwataka kwenda kufanyia kazi ujuzi walioupata kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa na kusisitiza kuwa Hospitali ya Bugando ipo wazi kupokea uratibu wa mafunzo yajayo muda na wakati itakapohitajika.
BUGANDO YAENDELEA KUNUFAIKA NA UJIO WA PROFESA HAROLD KUTOKA NCHINI MAREKANI.
HOSPITALI YA BUGANDO YAENDELEA KUNUFAIKA NA UJIO WA PROFESA HAROLD KUTOKA NCHINI MAREKANI.
Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Prof. Harold E. Varmus katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ameendesha kikao kazi na wafanyakazi wa idara mbalimbali ikiwemo idara ya saratani , radiologia, histopathologia na kitengo cha nuclear medicine(mionzi ya atomiki) pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha CUHAS lengo likiwa ni kufahamishana tulipotoka, tulipo na tunapoelekea juu ya tafiti za saratani ulimwenguni kote.
Prof Harold ameeleza ukubwa wa janga la ugonjwa wa saratani na hasa kwa Nchi zinazoendelea ambapo amesema; "Tunalo jukumu la kupambana na janga hili kwa kutoa elimu sahihi kwa jamii kupitia vikundi mbalimbali vitakavyoelimisha jamii na kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa pamoja na kuanzishwa kwa programu mbalimbali za uchangishaji fedha zitakazoweza kusaidia huduma hizi kwani kwa kufanya hivyo Afya za wananchi zitaimarika kwa kupata huduma stahiki na kipato kitaongezeka kwa ujumla".
Kwa upande wa wafanyakazi na wanafunzi walioshiriki kikao hicho wamemshukuru Prof. Harold kwa kikao hicho kizuri kwani kina manufaa makubwa katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Pia wameushukuru uongozi wa Hospitali kwa kuwapatia nafasi ya kufanya mazungumzo chanya na Profesa huyo kwani kupitia mazungumzo hayo wameendelea kufahamishana ni wapi walipo na ni nini kifanyike ili waweze kufika wanapotamani kufika.
BUGANDO MWENYEJI MAFUNZO YA KITAIFA YA UCHUNGUZI YAKINIFU WA SARATANI KWA KUTUMIA MIONZI
HOSPITALI YA BUGANDO MWENYEJI MAFUNZO YA KITAIFA YA UCHUNGUZI YAKINIFU WA SARATANI KWA KUTUMIA MIONZI
Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando imekua mwenyeji wa mafunzo ya uchunguzi na uvumbuzi wa saratani kwa kutumia mitambo mbalimbali ya mionzi. Mafunzo haya ya siku 9, ambayo yameanza leo Mei 19 na yanatarajiwa kutamatika mei 27, 2025 yanafanyika katika Hospitali ya Bugando na yamehusisha washiriki kutoka Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa nchini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo watoa huduma za uchunguzi wa saratani kwa kutumia mionzi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo haya mapema leo Mei 19. 2025, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt. Bahati Wajanga amewashukuru waandaji wa mafunzo haya kwa kuichagua Hospitali ya Bugando kuwa mwenyeji wa Mafunzo haya huku akiwataka washiriki kuwashirikisha wengine ujuzi watakaoupata.
" Niwashukuru Wataalamu wa kimataifa na kitaifa kuja kuwajengea uwezo washiriki hawa kinadharia na kivitendo, nina matumaini na imani haya mafunzo yamekuja wakati sahihi na yanakwenda kuwanufaisha siyo washiriki tu bali wananchi na wagonjwa kwa ujumla wake. Niwaombe washiriki mkirudi mkayafanyie kazi mtakayojifunza ili kuwawezesha na wengine ambao hawajapata fursa hii.
Amesisitiza Dkt. Bahati Mafunzo haya yameratibiwa kwa ushirikiano wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Tume ya nguvu za Atomu Tanzania, Chuo cha CUHAS na yamefadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu Duniani.
WAGONJWA 40 WASIOWEZA KUMEZA KUWEKEWA KOO BANDIA HOSPITALI YA BUGANDO
WAGONJWA 40 WASIOWEZA KUMEZA KUWEKEWA KOO BANDIA
Hospitali ya Bugando imezindua kambi ya matibabu ya saratani ya koo la chakula,ambapo koo hili bandia (stent) litamsaidia mgonjwa kuweza kumeza chakula. Kambi hii imehusisha wataalamu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Marekani, Kenya kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani ya nchi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na KCMC. Huduma hii imetolewa bure kwa wagonjwa hawa.
Akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga, Dkt. Sr. Alicia Massenga,Mkurugenzi Huduma za Upasuaji Bugando amewashukuru wataalamu hawa kwa kufika katika Hospitali ya Bugando na kuwasidia wagonjwa, pia kutoa mafunzo yatakayoweza kuwajengea uwezo wataalamu wa Hospitali ya Bugando wakiwemo Madaktari wa upasuaji na kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakua msaada mkubwa katika matibabu ya wagonjwa hawa.
Sambamba na hayo Dkt.Michael Mwachiro Daktari bingwa wa Upasuaji na mtafiti wa saratani ya njia ya chakula kutoka Kenya(Africa Esophageal Cancer) amesema, “shida hii hutokana na saratani ya njia ya chakula inayoonekana zaidi Afrika ya Mashariki na Kusini na hivyo kwa umoja wetu tumekuja katika hospitali ya Bugando kuwajengea uwezo wa njia rahisi ambayo wataalamu hawa wataweza kuweka vyema kifaa hiki cha koo bandia (stent) pia naishukuru kampuni ya Marekani kwa kusaidia kwa vifaa hivyo vya kuweka koo bandia”.
Dkt. Mwachiro ameongeza kuwa, tafiti katika hatua ya awali zinaonesha saratani ya njia ya chakula inasababishwa na kurithi, moshi kutokana na matumizi ya kuni au sigara, pombe kali pia za kienyeji pamoja na dawa zinazotumika kwa mifugo na sababu zingine nyingi.
KAMBI YA MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHUO CHA DUKE - MAREKANI
KAMBI YA MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHUO CHA DUKE
Madaktari Bingwa kutoka chuo kikuu cha Duke, kwa kushirikiana na Madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na taasisi mbalimbali Afya za nchini Marekani ikiwemo taasisi ya Healing the Children North East wameendesha kambi ya upasuaji sanifu rekebishi wa uso (facial plastic) kwa wakazi wa kanda ya ziwa, ikiwa pia ni sehemu ya kubadilishana uzoefu kwa wataalamu hawa. Kambi hii inafanyika kupitia idara ya upasuaji sanifu na Idara ya pua , koo na masikio, katika kutoa huduma za matibabu na upasuaji.
MUWAKILISHI KUTOKA SHIRIKA LA (IAEA) DKT. SANDRA ATEMBELEA BUGANDO
DKT. SANDRA KUTOKA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA NISHATI YA ATOMU DUNIANI (IAEA) ATEMBELEA BUGANDO.
Dkt. Sandra Ndarukwa ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya saratani na Mtaalamu anayesimamia shughuli za tiba ya mionzi kutoka shirika la nishati ya Atomiki Duniani (International Atomic Energy Agency) ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo likiwa ni kuangalia na kutembelea shughuli mbalimbali zinazosimamiwa na shirika la Nishati ya Atomiki Duniani (IAEA)
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga, amemkaribisha na kumpongeza Dkt. Sandra kwa kutembelea Bugando na kuendelea kudumisha mashirikiano hasa katika eneo la ununuzi wa vifaa tiba, matibabu ya mionzi pamoja na mafunzo mbalimbali ambayo Watumishi wanaendelea kubadilishana uzoefu na ujuzi katika fani mbalimbali,
"Tumejitoa na tuna bidii katika suala la utoaji wa matibabu ya saratani ambapo kama Hospitali tunatarajia kufanya mbio za Marathon msimu wa pili kwa lengo la kusaidia Wagonjwa wa saratani wanaoshindwa kulipia gharama za matibabu. Hivyo, tunawakaribisha kuungana pamoja nasi katika suala hili" ameeleza hayo Dkt. Bahati Wajanga.
Aidha, Dkt. Sandra ameushukuru Uongozi wa Hospitali kwa kumpatia nafasi ya kipekee kuweza kutembelea na kuzungumza na baadhi ya Wafanyakazi katika Idara ya saratani kwani mashirikiano yamejengwa katika utoaji huduma bora kwa Wagonjwa.
Pia ameipongeza Hospitali ya Bugando kwa kuendelea kutoa huduma nzuri kwa Wagonjwa kwani shirika linafurahi kuona Hospitali inaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya mashirikiano na kusema " mafunzo yanayoendelea ya uchunguzi yakinifu wa saratani kwa kutumia mionzi yana lengo la kuwajengea uwezo watoa huduma za saratani kupitia mionzi hivyo niwaombe Watumishi mliopata nafasi ya kupata mafunzo haya mkayatumie vyema katika vituo vya kazi".
TUZO ZA MALKIA WA NGUVU 2025 KANDA YA ZIWA
DKT. EMMANUELA AMBROSE KUTOKA HOSPITALI YA BUGANDO KINARA SEKTA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Dkt. Emmanuela Ambrose Kinara Sekta ya Afya na Ustawi wa Jamii
Dkt. Emmanuela Ambrose, Daktari Bingwa wa Watoto Kitengo cha Sikoseli kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ameshinda u Tuzo ya Malkia wa Nguvu Kanda ya Ziwa katika Kipengele cha Afya na Ustawi wa Jamii kutokana na Mapambano yake kusaidia jamii dhidi ya ugonjwa wa Sikoseli kupitia Tafiti na kuibua suluhu ya kukabiliana na Ugonjwa wa Sikoseli.
Tuzo hii imetolewa katika hafla ya Kilele cha Malkia wa Nguvu Kanda ya Ziwa zilizofanyika katika Ukumbi wa Winterfell Jijini Mwanza na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mtanda mbali na kupongeza Uongozi wa Clouds Media Group na wadau ametoa wito kwa walioshinda tuzo mbalimbali kutokua na kiburi badala yake wawasaidie na kuwainua wengine.
" Naomba niwapongeze kwa dhati ndugu zetu Clouds, serikali yetu ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo nanyi begabega katika juhudi mnazozifanya kupitia jukwaa hili kwani mnavumbua na kuwapiga jeki malkia wa nguvu, tuendelee kufanya kazi" Mhe. Mtanda.
Mhe. Mtanda ameongeza kuwa
" Jukwaa la Malkia wa Nguvu linajenga umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa wanawake na ni kichocheo cha maendeleo miongoni mwao".
Tuzo za Malkia wa Nguvu Kanda ya Ziwa ambazo zimefikia kilele chake usiku wa kuamkia leo zimehusisha wanawake kutoka Mikoa ya kanda ya ziwa huku tuzo zilizowaniwa zikijikita katika vipengele mbalimbali ikiwa ni pamoja na Madini, Ujasiliamali, Afya na Ustawi wa Jamii na Uvuvi.
HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MATIBABU YA MDOMO WAZI NA MDOMO SUNGURA
KARIBU UPATE MATIBABU YA KIBINGWA YA MDOMO WAZI NA MDOMO SUNGURA
MISA TAKATIFU NDANI YA JUMUIYA YA BUGANDO
MISA TAKATIFU PAMOJA NA SAKRAMENTI YA KIPAIMARA KATIKA KANISA LA ST. MARTIN DE PORRES - BUGANDO
Padri Valentine Kabati ambaye ni Makamu wa Askofu wa jimbo kuu Katoliki Mwanza akimuwakilisha Mhashamu Baba Askofu Renatus Nkwande Leo Mei 10, 2025 ameongoza misa takatifu ndani ya jumuiya ya Bugando Pamoja na saktramenti ya kipaimara katika kanisa la St. Martin De Porres - Bugando
Akizungumza katika misa hiyo Padri valentine amewataka watu wote kuwa mfano wa kuigwa hasa katika malezi ya watoto kwani msingi na maadili ya watoto huanzia utotoni na kusema
"Sisi ni vyombo ambavyo Kristo anatutumia kuhubiri na kuwa faraja kwa wengine kwani kupitia sisi watoto wetu wanapata ujasiri na nguvu za kutangaza habari njema kwa wengine ".
Aidha amewapongeza waumini wa Kanisa Katoliki pamoja na Watumishi wa Jumuiya ya Bugando kwa kujumuika katika misa hiyo.
KAMBI YA MAFUNZO, UPIMAJI NA TATHIMINI YA USIKIVU (HEARING THE CALL VISIT AND HEARING ASSESSMENT) YAHITIMISHWA.
KAMBI YA MAFUNZO, UPIMAJI NA TATHIMINI YA USIKIVU (HEARING THE CALL VISIT AND HEARING ASSESSMENT) YAHITIMISHWA.
KAMBI YA MAFUNZO, UPIMAJI NA TATHIMINI YA USIKIVU (HEARING THE CALL VISIT AND HEARING ASSESSMENT) YAHITIMISHWA. Hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Koo, Pua na Masikio (ENT) kitengo cha Usikivu, imehitimisha kambi ya siku nne ya mafunzo, upimaji na tathimini ya usikivu(HEARING THE CALL VISIT AND HEARING ASSESSMENT CAMP) yaliyoanza tarehe 19 Mei, 2025 na kuhitimishwa leo Mei 22, 2025 kwa kushirikiana na madaktari saba wa masikio na usikivu kutoka nchini Marekani.
Mkuu wa Idara ya ENT Dkt. Rogers Machimu ameshukuru uongozi wa Hospitali, wataalamu wa usikivu wa Bugando na Madaktari saba kutoka nchini Marekani kwa kuwezesha kambi hii muhimu ambayo amesema imefikia lengo kwa idara kuweza kunufaika kwa kubadilishana ujuzi, kupata mafunzo na kutoa huduma kwa wananchi na kuomba ushirikiano huu kuendelea ili kufikisha huduma bora zaidi kwa wananchi .
Akizungumza wakati wa kuhitimisha kambi hii, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga ameipongeza Idara ya ENT na Madaktari wageni na kusema, “Nishukuru na niwapongeze idara kwa kambi hii muhimu kwani Hospitali tumeweza kunufaika kupitia ushirikiano huu kwa kubadilishana uwezo na ujuzi kati yenu na wenzetu , hii inaenda kugusa moja kwa moja katika utoaji huduma bora kwa Wananchi tunaowahudumia, zaidi niwashukuru wenzetu kwa kuichagua Bugando na kushirikiana nasi, kubadilishana ujuzi na uzoefu, kutuletea vifaa na kutoa huduma kwa wagonjwa na niwakaribishe tena wakati mwingine kuja Bugando kwani ushirikiano huu kwetu utakuwa endelevu, Asanteni sana”.
Aidha, mratibu wa Madaktari wa Hearing Call Dkt. Joan Mc Cormack amepongeza kwa maandalizi, mazingira mazuri ya kambi na ushirikiano mkubwa walioupata katika kambi hii nakusema haitakuwa safari yao ya mwisho kuja Bugando na watakuwa mabalozi wazuri wa ushirikiano huu.
BUGANDO YAPOKEA VIFAA TIBA KUTOKA SHIRIKA LA GOAL 3
BUGANDO YAPOKEA VIFAA TIBA KUTOKA SHIRIKA LA GOAL 3
BUGANDO YAPOKEA VIFAA TIBA KUTOKA SHIRIKA LA GOAL 3 Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea msaada wa vifaa tiba vya kufuatilia maendeleo ya watoto wanaohitaji uangalizi maalumu kutoka katika shirika la Goal 3.
Msaada huu umepokelewa leo Mei 22, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga na kushukuru shirika la Goal 3 kwa kuleta mashine za IMPALA Monitors ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwa watoto lakini pia kupitia mashirikiano haya yataleta mafanikio katika kubadilishana uzoefu na ujuzi kazini.
Naye Dkt. Tulla Masoza ambaye ni Mkuu wa Idara ya watoto ameushukuru uongozi wa Hospitali pamoja na shirika la Goal 3 kwa msaada wa vifaa hivyo kwani vitakua msaada mkubwa katika maeneo yao ya kazi na kuahidi kwamba vifaa hivyo vitaenda kufanya kazi iliyokusudiwa.
HOSPITALI YA BUGANDO YAENDESHA KAMBI MAALUMU YA USIKIVU KWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI WA MASIKIO NA USIKIVU KUTOKA NCHINI MAREKANI
HOSPITALI YA BUGANDO YAENDESHA KAMBI MAALUMU YA USIKIVU KWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI WA MASIKIO NA USIKIVU KUTOKA NCHINI MAREKANI
HOSPITALI YA BUGANDO YAENDESHA KAMBI MAALUMU YA USIKIVU KWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI WA MASIKIO NA USIKIVU KUTOKA NCHINI MAREKANI
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Pua, Koo na Masikio (ENT) kitengo cha Usikivu inaendesha kambi maalumu ya Mafunzo, Upimaji na tathimini ya Usikivu (HEARING THE CALL VISIT AND HEARING ASSESSMENT CAMP) kwa kushirikiana na Madaktari wa Masikio na Usikivu kutoka nchini Marekani kwa muda wa siku nne, kambi hii inalenga kubadilishana uzoefu na kutoa huduma za usikivu kwa wananchi.
“kambi hii ni muhimu, kupitia Madaktari wenzetu kutoka Marekani itatusadia sana katika kujengeana uwezo na ujuzi sambamba na kutoa mafunzo jumuishi kwa Wanafunzi, tunaendelea kutoa huduma ya upimaji na matibabu kwa watu wenye matatizo ya usikivu kuanzia watoto wachanga na kufanya tathimini ya tatizo kupitia kambi hii” amesema Dkt. James Komanya, Daktari wa Masikio na Usikivu na Raisi wa Chama cha Wataalamu wa Usikivu Tanzania.
MAADHIMISHO YA SIKU YA KANGAROO DUNIANI
..
Wakina mama wajawazito wametakiwa kuhudhuria kliniki mara tu wanapopata ujauzito ili kuhakikisha usalama wa watoto hususani wanapojifungua kabla ya muda waweze kupata huduma stahiki ikiwemo ya Kangaroo.
Wito huu umetolewa mapema leo Mei 15, 2025 na Muuguzi Kiongozi Idara ya Watoto, Sr. Dismas Mauki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Kangaroo Duniani ambayo huadhimishwa kila lfikapo Mei 15 kila mwaka na kwa mwaka huu ikiwa na kauli mbiu
" Mikononi Mwangu, Unaishi"
Sr.Mauki ameongeza "uhusiano kati ya mzazi na mtoto unajengwa toka mtoto akiwa mdogo na nitoe rai kwa wazazi wawe karibu na watoto wao tangu wakiwa wadogo siyo jukumu la Mama tu kulea mtoto njiti wote Baba na Mama washirikiane". Amesema Sr. Mauki.
Maadhimisho haya katika Hospitali ya Bugando yamekwenda sambamba na kupokea msaada wa vibebeo maalum na utoaji elimu ya namna ya kutumia vibebeo hivyo vilivyotolewa na Taasisi ya Babymoon Africa ya Jijini Mwanza kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda ili kuwawezesha wazazi kufanya shughuli nyingine.
Msaada huu umepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Tiba Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Benard Gombanila ambaye ameishukuru Taasisi ya Babymoon kwa msaada huo huku akiahidi ushirikiano nao zaidi na kuangalia uwezekano wa kuagiza vibebeo zaidi kama Hospitali kutoka Taasisi ya Babymoon ambao ni wazalishaji wa vibebeo hivi.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inapokea wastani wa watoto njiti 30 hadi 40 kwa mwezi ambao wanahudumiwa katika kitengo cha watoto wachanga kupitia wataalamu wabobezi wa eneo hili.
BUGANDO YAHITIMISHA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA BUHONGWA.
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Mei 6, 2025, imehitimisha zoezi la utoaji huduma ya uchunguzi na ushauri wa magonjwa yasiyoambukiza kwa wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza. Zoezi hili limekuwa na manufaa makubwa sana kwa jamii kwani watu mbalimbali wa kila rika wameweza kujitokeza kupata huduma ya upimaji wa virusi vya UKIMWI (VVU), shinikizo la damu, uzito pamoja na ushauri kwa tiba lishe na tiba ya kisaikolojia.
Bugando imetoa huduma hizi ikiwa na lengo la kuwasogezea huduma wananchi ili kupunguza kasi ya ongezeko la magonjwa yanayoambukiza katika jamii.
MAONESHO YA SANAA YA UCHORAJI KWA WATOTO WENYE SIKOSELI (SELIMUNDU) YAFANA BUGANDO.
..
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa kushirikiana na wadau wakiwemo Taasisi ya Mashujaa wa Sikoseli (TASIWA) imeendesha Maonesho ya Michoro ya sanaa kwa watoto wenye sikoseli inayoelezea mambo ambayo wanayoyapitia na matamanio yao kwa watoa huduma na jamii kutokana na madhira wanayokumbana nayo wao wagonjwa wa sikoseli .
Maonesho hayo yamegusa na kuteka hisia za wahudhuriaji kutokana na ubunifu uliooneshwa kupitia michoro yamefanyika katika Hospitali ya Bugando mapema leo April 25,2025 na kuhudhuriwa na Uongozi wa Hospitali sambamba na wadau mbalimbali wakiwemo Jumuiya ya Bugando, wazazi wa watoto wenye Sikoseli na wananchi. Dkt.Sr. Alicia Massenga, Mkurugenzi wa huduma za Upasuaji akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga, amepongeza waandaji wa maonesho hayo ambayo yameonyesha ubunifu wa hali ya juu na kutoa wito kwa wazazi kutowakatia tamaa watoto wenye Sikoseli kwani wana uwezo sawa na Mtoto mwingine yoyote.
" Tumejifunza na tunathamini sana vipaji vyenu, leo mtu asipoona hawezi kufikiria ni ninyi mmetengeneza kazi hizi, ninyi wazazi tuwaibue tulikowaficha watoto wenye Sikoseli ili wawezeshwe na watimize ndoto zao" Amesisitiza Dkt. Massenga.
Kwa upande wao, watoto wenye Sikoseli wameshukuru waandaji kuwawezesha na kutoa wito kwa jamii kupitia sanaa ya michoro yao kuweka mazingira na huduma za afya bora, kuthaminiwa, kuaminiwa na kutokatiwa tamaa kwani kuwa mgonjwa wa sikoseli siyo mwisho wa maisha bado wanao uwezo kama watoto wengine.
MAFUNZO YA NAMNA YA KUWAHUDUMIA WATOTO WAKATI WA DHARURA YAFANYIKA KWA WATAALAMU WA USINGIZI
..
Wataalamu wa Afya wa Usingizi na Ganzi salama kutoka Kanda ya Ziwa wamepata mafunzo ya nadharia na vitendo juu ya kuwahudumia Watoto wakati wa dharura yaliyoendeshwa kwa siku mbili na kuhitimishwa hii leo Mei 6, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Mafunzo haya ni kuelekea Mkutano mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Usingizi na Ganzi salama Tanzania(SATA) yatakayoanza tarehe 7 Mei 2025 jijini Mwanza, ambapo mafunzo haya yameendeshwa na Rais wa SATA nchini Dkt. Edwin Lugazia kutoka Muhimbili, Mkuu wa Idara ya Anesthesia Bugando Dkt. Rebecca Samwel, Dkt. Anna Assenga kutoka MOI, Dkt. Hosiana Athanase, Dkt. Kevin Mero na Bwn. Daniel Obure kutoka Bugando huku washiriki wakiwa tisa kutoka Hospitali za Kanda ya Ziwa.
Mafunzo haya ni Maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo watoa dawa za usingizi na ganzi salama katika kuwahudumia Watoto wanaopata dharura yeyote kabla ya upasuaji, wakati wa upasuaji na baada ya upasuaji.
WABUNGE WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA MTAKATIFU AUGUSTINO MWANZA (SAUT) MEI 4, 2025 WAMETEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO
Wabunge wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Mtakatifu Augustino Mwanza ( SAUT) mei 4, 2025 wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo likiwa kuwaona na kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa wa saratani pamoja na kuchangia damu.
Wabunge wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Mtakatifu Augustino Mwanza ( SAUT) mei 4, 2025 wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo likiwa kuwaona na kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa wa saratani pamoja na kuchangia damu.
Akizungumza Bwn. Joseph Paul ambaye ni spika wa Bunge serikali ya Wanafunzi (SAUTSO) ameushukuru na kuupongeza uongozi wa Hospitali kwa kuwapokea na kuruhusu waweze kutembelea wagonjwa na kusema
" Tuliona kama viongozi kuna haja ya kurudisha kwa jamii kwa kufanya matendo ya huruma na kupata elimu ambayo itatusaidia sisi kama viongozi na kuweza kuwa mabalozi kwa wengine".
Aidha, kwa niaba ya uongozi wa hospitali, mtaalamu Bingwa wa Afya ya jamii ya Saratani Bwn. Kidaya Bashari amewakaribisha na kuwapongeza wabunge hao wa Serikali ya wanafunzi kwa kutembelea na kuwaona wagonjwa kwani kwa kufanya hivyo wagonjwa wanafarijika na kurejesha tumaini.
Pia wanafunzi hao wamepata nafasi ya kupata elimu juu ya magonjwa ya saratani na kutoa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa wa saratani.
BUHONGWA YANUFAIKA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
BUHONGWA YANUFAIKA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
Katika harakati za kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imewasogezea huduma ya uchunguzi wa magonjwa yasiambukiza ikiwemo upimaji wa shinikizo la damu, uzito, sukari, VVU na utoaji wa chanjo kwa watoto pamoja na ushauri wa lishe, na kisaikolojia, kwa wakazi wa Kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza. Zoezi hili lililoongozwa na Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Bugando limefanyika mapema leo Mei 5, 2025 na linatarajiwa kumalizika Jumanne ya Mei 6, 2025.
BUGANDO YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI (MEI MOSI) MKOANI MWANZA.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakishikilia vyeti baada ya kuchaguliwa kuwa Watumishi Hodari katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambapo kwa Mkoa wa Mwanza yamefanyika Wilayani Kwimba.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakishikilia vyeti baada ya kuchaguliwa kuwa Watumishi Hodari katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambapo kwa Mkoa wa Mwanza yamefanyika Wilayani Kwimba.
Mgeni rasmi katika maadhimisho haya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Saidi Mtanda amewapongeza wafanyakazi wa Mwanza kwa maadhimisho ya siku hii muhimu na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidiii huku akiwataka kujiepusha na vitendo vinavyoenda kinyume na maadili ya mtumishi.
"Niwapongeze kwa kazi kubwa mnayofanya, nyie ndio mnahakikisha wananchi wanapata huduma bora, kupitia zawadi hizi kwa watumishi hodari ni motisha na chachu kwa wengine kuongeza juhudi, ubunifu na maarifa kwenye majukumu yenu" Mh. Mtanda.
Aidha, Mhe. Saidi Mtanda amesema ameona jumbe kwenye mabango na kusikiliza risala ya wafanyakazi, kupokea pongezi, shukurani kwa serikali sambamba na changamoto zinazowakabili na kusema zimefika sehemu sahihi kushughulikiwa ili kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi na kuleta maendeleo yanayohitajika.
Akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dkt. Cosmas Mbulwa ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma Saidizi, amewapongeza watumishi hodari wa Bugando na kuwasihi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na waendelee kuwa chachu kwa wengine kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na ubunifu zaidi.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (Mei Mosi) kwa Mkoa wa Mwanza yameadhimishwa Wilayani Kwimba huku kitaifa yakifanyika Mkoani Singida, yakiwa na kaulimbiu isemayo "Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki "
KIKAO KAZI CHA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI
KIKAO KAZI CHA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI HOSPITALI YA BUGANDO
PADRI DKT. PAUL CHOBO ATEMBELEA BUGANDO
Padri Dkt. Paul Chobo, kutoka jimbo la Tabora na Mkurugenzi wa huduma za Afya Baraza la Maaskofu (TEC) Atembelea Hospitali ya Bugando
Padri Dkt. Paul Chobo, kutoka jimbo la Tabora na Mkurugenzi wa huduma za Afya Baraza la Maaskofu (TEC) leo Aprili 15, 2025 amezungumza na jumuiya Bugango(BMC,CUHAS, MWACHAS) akiwa amemuwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Bugando, Askofu Mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mwanza Mhashamu Askofu Renatus Nkwande na pia Baraza la Maaskofu TEC.
PD. DKT. CHOBO AZUNGUMZA NA JUMUIYA YA BUGANDO
PD. DKT. CHOBO ATEMBELEA NA KUZUNGUMZA NA JUMUIYA YA HOSPITALI YA BUGANDO
Padri Dkt. Paul Chobo, kutoka jimbo la Tabora na Mkurugenzi wa huduma za Afya Baraza la Maaskofu (TEC) leo Aprili 15, 2025 amezungumza na jumuiya Bugango(BMC,CUHAS, MWACHAS) akiwa amemuwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Bugando, Askofu Mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mwanza Mhashamu Askofu Renatus Nkwande na pia Baraza la Maaskofu TEC.
Akizungumza katika Mkutano huo, Padri Chobo amewatambulisha viongozi wapya walioteuliwa hivi karibuni akiwaasa jumuiya hiyo kupokea mabadiliko hayo na pia kuwapatia ushirikiano viongozi hao ambao ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Dkt. Bahati Wajanga,Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango CPA (T) Livino Malya,Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt.Benard Gombanila na pia Kaimu Mhasibu Mkuu CPA (T) Sr.Leotina Malago.
Aidha Padri Chobo amesema ujumbe alioagizwa kwa jumuiya ya Bugando na Mwenyekiti wa bodi Askofu Mkuu Renatus Nkwande ni mambo matatu, Kujiamini,kudumisha uwajibikaji na pia kufanya kazi kwa ushirikiano (Team work) Sambamba na hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt Bahati Wajanga amemshukuru Padri Chobo kwa kufika Bugando na pia kwa maneno yakujenga kwa jumuiya hiyo ya Bugando. Dkt. Wajanga ameongeza na kuwasisitiza jumuiya hiyo kuishi ujumbe huo ulioletwa kutoka Baraza la Maaskofu kwa kuzingatia na kutafakari kauli mbiu ya Bugando inayosema” Bugando Mpya, Yenye Huruma na Upendo. Tunathamini Afya yako, Kazi Iendelee”
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (Mb) atembelea banda la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (Mb) atembelea banda la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (Mb) atembelea banda la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ikiwa ni katika kilele cha siku ya Afya kitaifa ambapo maadhimisho hayo yanaenda na kauli mbiu isemayo, "Tulipotoka, Tulipo,Tunapoelekea, Tunajenga Taifa Imara lenye Afya"
Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi Dkt. Cosmas Mbulwa
Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi Dkt.Cosmas Mbulwa
Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi Dkt. Cosmas Mbulwa Leo Aprili 7, 2025 atembelea Banda la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lililopo katika viwanja vya Jakaya Kikwete convention Centre kuona jinsi huduma zinavyoendelea kutolewa kwa Wananchi ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya Afya kitaifa yakiangazia
"Tulipotoka, Tulipo, Tunapoelekea"
MAADHIMISHO YA WIKI YA AFYA KITAIFA.
MAADHIMISHO YA WIKI YA AFYA KITAIFA.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya Afya kitaifa yanayofanyika mkoani Dodoma. Maadhimisho haya yameambatana na ufunguzi wa mdahalo wa wiki ya Afya Kitaifa na umefunguliwa rasmi na Katibu mkuu wa wizara ya Afya, Dkt.Seif Shekalaghe.
Mdahalo wa maadhimisho hayo umelenga kuangazia mafanikio mbalimbali ya Sekta ya Afya ilipotoka, ilipo na inapokwenda.
Sambamba na mdahalo huo, Hospitali ya Bugando inatoa huduma za upimaji wa afya ya macho bure kwa wananchi katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma.
Wananchi wote mnakaribishwa kupata huduma hizi za kibingwa na kibingwa bobezi.
BUGANDO FC YAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO.
HOSPITALI YA BUGANDO FC YAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO.
Timu ya mpira wa miguu ya Bugando Football Club imepokea vifaaa vya mazoezi kutoka katika uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando hii leo Aprili 2, 2025 kama vile jezi, mipira, koni, vihunzi pamoja na bendera ya timu kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali ambayo yanajenga mahusiano na Taasisi nyigine kupitia mpira wa miguu.
Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Dkt. Bahati Wajanga amewapongeza viongozi na wachezaji wa timu hiyo kwani Michezo ni sehemu ya kuboresha Afya na kusema; "Sisi kama Taasisi ya Afya tunalo jukumu la kuhamasisha mazoezi ili tuweze kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza hivyo kupitia vifaa hivi twende tukahamasishe jamii kwa vitendo na tukavitunze vifaa hivi ili vitumike muda mrefu na kufanya kazi iliyokusudiwa".
Aidha Bw. Kelebe Luteli ambaye ni mratibu wa timu amepongeza na kushukuru uongozi wa Hospitali kwa kuendelea kulea timu ya Bugando FC kwani timu hii mbali na michezo bado inashirikiana vyema na timu nyingine Pamoja na jamii kwa ujumla, na kuahidi kwenda kutunza vyema vifaa hivyo ambavyo vitaleta manufaa makubwa ndani ya timu na Taasisi kwa ujumla.
BUGANDO YAINGIA MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO NA TAASISI YA AFYA IFAKARA.
BUGANDO YAINGIA MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO NA TAASISI YA AFYA IFAKARA.
BUGANDO NA AGAKHAN YAKUBALIANA KUPAMBANA NA SARATANI UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.
HOSPITALI YA BUGANDO NA AGAKHAN YAKUBALIANA KUPAMBANA NA SARATANI UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa awamu nyingine imeingia makubaliano na Hospitali ya Agakhan kushirikiana na kutekeleza mradi mtambuka wa saratani kwa Afrika Mashariki (East Afrika Comprehensive Cancer Project) wenye lengo la kuboresha huduma za saratani ndani ya ukanda huo.
Makubaliano haya yamesainiwa kwa mara nyingine baada ya awamu ya kwanza ya makubaliano kuisha mwaka 2023 na Bugando ilinufaika na mradi huu mtambuka.
Mradi huu umelenga kuboresha huduma za saratani kwa jamii kwa kutanua huduma za elimu ya saratani na uchunguzi wa awali wa saratani, tafiti za saratani na mafunzo kwa watoa huduma.
Akizungumza wakati wa uwekaji saini makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt.Bahati Wajanga amepongeza mashirikiano hayo yaliyosainiwa kati ya Bugando na Agakhan, amesema kuwa Bugando itaendeleza kutoa huduma za uchunguzi kwa wananchi ikiwa ni moja ya hatua za kuzuia na kulinda afya za wagonjwa ili iwasaidie kufika Hospitali kwa wakati na kupata matibabu.
Naye Bw.Sisawo Konteh ameipongeza Hospitali ya Bugando kwa kuyaendeleza mashirikiano hayo na kuendelea kusisitiza utoaji Bora wa huduma za Afya, hulu tukuzingatia ubora wa huduma zinazotolewa na mradi huu ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa Wananchi na Afrika mashariki kwa ujumla.
BUGANDO KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU, KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA WATOTO WACHANGA
BUGANDO KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU, KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA WATOTO WACHANGA
Hospitali ya Rufaa ya ya Kanda Bugando leo Machi 17, 2025 imepokea msaada wa vifaa tiba mahsusi kwa ajili ya kupunguza vifo vya Watoto wachanga vyenye thamani ya Tshs. Million 116 Kupitia Programu ya Newborn Essential Solutions & Technologies (NEST 360).
Vifaa hivi vimekabidhiwa na Mratibu wa Programu ya NEST 360, Bi. Magdalena Mwaikambo katika hafla fupi iliyofanyika katika Hospitali ya Bugando.
Akiongea katika makabidhiano hayo, Bi Magdalena amesema, Programu hii ya NEST 360 imekua ikishirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Wizara ya Afya, Ifakara Health Institue (IHI), Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) pamoja na Dar es salaam Institute of Technology (DIT) katika kuhakikisha wanapunguza changamoto hii.
Akipokea vifaa hivyo Dkt. Bahati Wajanga Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, ameshukuru kwa vifaa hivi vilivyotolewa na NEST 360 kwa kushirikiana na wafadhili wengine na kuongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuokoa maisha ya watoto wengi.
Aidha Dkt. Wajanga ametanabaisha kuwa, Programu hii imekua ikisimamia mafunzo kwa wauguzi wanaotoa huduma katika maeneo mengi ya hospitali ikiwemo chumba cha watoto walio katika uangalizi maalum (Neonatal ICU), Chumba cha kujifungulia wanawake (Labor Ward) na kwingine. Lakini pia imekua ikifanya ufatiliaji wa mafunzo waliyoyatoa kazini.
Huku akiongeza kuwa programu hii iko katika ukarabati wa chumba cha watoto wachanga na baadae kusaidia katika ujenzi wa jengo la mama na Mtoto.
Hospitali ya Bugando yaendelea kutoa huduma ya uchunguzi wa Kinywa na Meno
Hospitali ya Bugando yaendelea kutoa huduma ya uchunguzi wa Kinywa na Meno
Hospitali ya Bugando yaendelea kutoa huduma ya uchunguzi wa Kinywa na Meno pamoja na utoaji Elimu na ushauri kwa Wanafunzi wa Sekondari Igoma, Ili kujenga uelewa wa utunzaji Kinywa, huduma hizi ambazo zinaenda sawia na kaulli mbiu; "Kinywa chenye furaha Akili yenye furaha"
KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI, MACHI 20, 2025
KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI, MACHI 20, 2025
KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI, MACHI 20, 2025
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Kinywa na Meno imeendesha huduma ya uchunguzi wa awali wa Afya ya Kinywa na Meno sambamba na kutoa elimu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, Shule za Sekondari na Wanachuo Jijini Mwanza.
Huduma hii inafanyika katika Shule za Msingi Nyanza, Buhongwa, Mirongo, Shule za Sekondari Igoma, Nyaburugoya na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Jijini Mwanza kwa siku tano ambapo imeanza leo tarehe 13 Machi katika Shule ya Msingi ya mchepuo wa kingereza Nyanza na itahitimishwa tarehe 20 Machi, 2025.
Huduma hii inatolewa bila malipo na ina lengo la kuwasogezea huduma wananchi ili kujenga jamii yenye Afya hususani ya Kinywa na Meno kwa kutambua hali ya Afya zao na kuchukua hatua mapema.
Maadhimisho ya Afya ya Kinywa na Meno kwa mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu
"Kinywa chenye furaha na Akili yenye furaha"
MAADHIMISHO YA SIKU YA FIGO DUNIANI.
HOSPITALI YA BUGANDO YAADHIMISHA SIKU YA FIGO DUNIANI.
Kila Alhamisi ya Wiki ya Pili ya Mwezi Machi, Dunia uhadhimisha siku ya magonjwa ya figo, ikiwa ni uhamaishaji kwa wananchi kujilinda dhidi ya magonjwa ya figo huku wataalamu wakiendelea kuelimisha umma juu ya magonjwa haya. Kwa mwaka huu Maadhimisho haya yamebeba yamebeba kauli mbiu isemayo "Gundua mapema, Linda Afya ya figo" . Na Hospitali ya Bugando imeadhimisha siku hii kwa kuendesha huduma ya uchunguzi wa kibingwa na bingwa bobezi kwa magonjwa hatarishi kwa Afya ya figo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Dkt. Jesca Lebba, Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza ambaye amekuwa mgeni rasmi katika siku hii muhimu, ameipongeza Hospitali ya Bugando kwa kuendelea kuboresha mazingira na huduma kwa watu wenye changamoto za figo ili kuendana na mahitaji yaliyopo kwenye jamii kwani hii inaendana sambamba na juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Afya katika uendelezaji wa taaluma za kibingwa na bingwa bobezi ambazo ni muhimu katika kukabiliana na ongezeko la watu wenye changamoto za figo, tatizo ambalo linaweza kuzuilika kwa mtindo bora wa maisha na matibabu bora.
Dkt. Lebba ameipongeza Bugando kwa kuwa na mikakati thabiti ya maandalizi ya huduma ya upandikizaji wa Figo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya. Pia amewasihi wananchi kuendelea kuishi katika msingi bora wa kulinda afya zao huku wakizingatia suala zima la kupata bima ya Afya.. Ameyasema hayo Dkt. Lebba
Sambamba na hayo, Dkt.Sr. Alicia Massenga akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga, ameeleza “Bugando inahudumia wagonjwa wenye changamoto za figo takribani 400 hadi 600 kwa mwezi na tumebaini wanawake wengi wanapata changamoto za figo wakati wa kujifungua kwa kupoteza damu nyingi huku ikichangiwa na sababu nyingine nyingi “.
BUGANDO YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
WANAWAKE WATUMISHI WA BUGANDO, WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Kuelekea Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyobeba kauli mbiu isemayo "Wanawake na Wasichana 2025, tuimarishe haki, Usawa na Uwezeshaji". Wanawake watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wameadhimisha sherehe hii kwa kutoa elimu na mafunzo mbalimbali wakiwa na dhumuni la kukumbushana wajibu, kutathmini mafanikio na changamoto mbalimbali katika jitihada za kutoa fursa sawa kwa Wanaume na Wanawake ili kushiriki katika harakati za kuboresha maisha ya kila siku bila ubaguzi wa kijinsia.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga amewashukuru na kuwapongeza wanawake kwa ushirikiano na umoja wanaouonyesha katika shughuli hii ya maadhimisho na kusema
" Ni kweli kwamba ukielimisha Mwanamke umeelimisha jamii na Taifa kwa ujumla na sisi kama viongozi wenu tuna imani na elimu mliyoipata hapa kwamba mtayaishi na kuyadumisha yale yote mema kwa ajili ya kutengeneza Taifa lililo jema na kwa kupitia haya tuna imani na tunathamini kazi zenu katika kuhakikisha Bugando inaendelea kupaa kwa kutoa huduma zilizobora zaidi”.
Kwa upande wao Wanawake watumishi wa Bugando wameushukuru uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kuendelea kuwalea vyema na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kujenga Taasisi na Nchi kwa ujumla.
BRAC NA QUEENS WATEMBELEA BUGANDO KUFARIJI WAGONJWA
BRAC NA QUEENS WATEMBELEA BUGANDO KUFARIJI WAGONJWA
WANAWAKE WA BUGANDO WASHIRIKI MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, ARUSHA.
WANAWAKE WA BUGANDO WASHIRIKI MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, ARUSHA.
VIKUNDI MBALIMBALI VYAJITOKEZA KUTOA MKONO WA POLE KWA WAGONJWA BUGANDO.
VIKUNDI MBALIMBALI VYAJITOKEZA KUTOA MKONO WA POLE KWA WAGONJWA BUGANDO.
VIKUNDI MBALIMBALI VYAJITOKEZA KUTOA MKONO WA POLE KWA WAGONJWA BUGANDO.
Kuelekea Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025 vikundi mbalimbali kutoka Wilayani Ilemela, Wanawake Watumishi wa Hospitali ya Bugando,Wanawake Tughe Bugando,Shirika la madawa na vifaa tiba ( TMDA) pamoja na Mratibu wa dawati la maendeleo ya jinsia halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Bi. Neema Majura wameungana pamoja katika kutoa Mkono wa pole kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
" Tumeamua kutoa mkono wa pole kwa Wagonjwa wa saratani kwani ugonjwa huu ni ugonjwa wenye matibabu ya muda mrefu na gharama zake zinaonekana kuwa juu kiasi kwamba tumeona tuje kushika mkono Watanzania wenzetu japo kwa kidogo tulicho barikiwa nacho kwani tabasamu lao linaleta furaha mioyoni mwetu " ameyasema hayo Bi. Neema Majura.
Akizungumza katika ujio huo Dkt. Cosmas Mbulwa Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewashukuru na kuwapongeza wageni hao kwa majitoleo yao kwani yana rejesha furaha kwa Wagonjwa na kusema
"Ni kweli matibabu haya yanachukua mda mrefu na yana gharama kwa kiasi chake hali ambayo Watanzania wenzetu wanahitaji faraja na usaidizi pale tunaweza, hivyo kupitia majitoleo haya nina imani Wagonjwa wetu watarejesha tabasamu na furaha mioyoni mwao".
Aidha amewaomba wageni hao elimu waliyoipata hapa ikawasaidie na kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawakuweza kufika kwani ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yoyote.
Kwa upande wa viongozi wa vikundi hivyo wametoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa Hospitali kwa kuwapa elimu na nafasi ya kuweza kutoa mkono wa pole na kuwaona wagonjwa kwani kwa kufanya hivyo wameweza kutimiza yalioyokuwa malengo na adhima ya vikundi vyao.
WAWATA JIMBO KUU KATOLIKI MWANZA WATEMBELEA BUGANDO
WAWATA JIMBO KUU KATOLIKI MWANZA WATEMBELEA IDARA YA SARATANI KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO.
Hii leo Wanawake Wakatoliki wa Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu Katoliki Mwanza wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kuwaona, kuwapa pole na kutoa majitoleo mbalimbali kwa Wagonjwa wa Saratani.
Akimuwakilisha Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza na kuongoza Ibada ya Misa Takatifu, Padre Fabian Ngeleja Paroko wa Parokia ya Mt. Josephine Bakhita Nyamanoro, Jimbo Kuu Katoliki Mwanza amewapongeza WAWATA kwa jambo kubwa la kiimani walilofanya na kusema "Huruma ni uponyaji, ukifanya matendo ya huruma ni sehemu ya Tiba, kuna Magonjwa pengine yanaonekana matibabu yake hayawezekani lakini kupitia huruma na rehema za Mungu watu wanapona, kusanyiko hili na ibada hii nina uhakika malaika wa mbinguni wameungana na WAWATA wakishangilia na kumsifu Mungu katika matendo ya huruma mnayoyafanya, hongereni sana" amesema hayo Padre Fabian Ngeleja.
Kwa upande wa Bi. Ester Bundala ambaye ni Mwenyekiti wa WAWATA Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, amesema lengo kuu ni kumshukuru Mungu kwa kuwasimamia na wameamua kufika kuwaona, kuwapa mkono wa faraja na kuwaombea Wagonjwa wa Saratani kupona na kuondokana na mateso wanayopitia na kuwapongeza WAWATA kwa majitolea na kuwaomba kuendelee na moyo huo huo wa kujitoa.
Aidha, Dkt. Nestory Masalu Mkuu wa Idara ya Saratani akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando amewapongeza na kuwashukuru WAWATA kwa Ibada na mkono wa pole walioutoa kwa Wagonjwa wa Saratani kwani utasaidia kuwapunguzia makali ya gharama za kuuguza pamoja na kuwapa moyo Wagonjwa hao.
WAWATA Jimbo Kuu Katoliki Mwanza wameshiriki Ibada ya misa takatifu katika Kanisa Katoliki Bugando, kisha wakapata elimu juu ya ugonjwa wa Saratani na kutoa vitu mbalimbali kwa Wagonjwa wa Saratani ikiwemo pampasi, unga lishe, sukari, mafuta, sabuni,dawa za meno na miswaki.
Dkt. Heronima Joas Kashaigili ambaye ni Daktari Bingwa bobezi wa magonjwa ya saratani za Watoto ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Bugando,
Dkt. Heronima Joas Kashaigili ambaye ni Daktari Bingwa bobezi wa magonjwa ya saratani za Watoto ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Bugando,
Dkt. Heronima Joas Kashaigili ambaye ni Daktari Bingwa bobezi wa magonjwa ya saratani za Watoto ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Bugando, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wadau na wafadhili kwa kufanikisha maadhimisho ya siku hii na kuwaasa wazazi na walezi kuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi mara kwa mara kwani saratani za watoto kwani saratani zinatibika iwapo mgonjwa atawahi kufika Hospitali.
Kwa upande wake Sabuni Daniel Busungu ambaye ni shujaa wa saratani ya mishipa ameushukuru uongozi wa Hospitali na Madaktari kwa kazi kubwa wanayoendelea kutoa katika kupamba na maisha yao na kuomba Serikali kuendelea kujitoa kikamilifu katika kutatua changamoto za saratani kwani ni matumaini yao kwamba kupitia jitihada mbalimbali wataenda kutimiza ndoto za maisha yao.
Maadhimisho haya yamemalizika kwa utoaji wa zawadi na majitoleo yaliyoambatana na Michezo na burudani mbalimbali kutoka kwa wafadhili ikiwemo timu ya mpira ya Mwanza Veteran na ngoma za asili.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeungana na Dunia nzima katika Kuadhimisha Siku ya Saratani za watoto duniani
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeungana na Dunia nzima katika Kuadhimisha Siku ya Saratani za watoto duniani
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeungana na Dunia nzima katika Kuadhimisha Siku ya Saratani za watoto duniani leo Februari 15, 2025 kwa kutoa elimu , huduma za uchunguzi wa magonjwa ya saratani za watoto, upimaji wa virusi vya Ukimwi( VVU) pamoja na zoezi la kuchangia damu ambapo maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Nyamagana Mkoani Mwanza na kauli mbiu isemayo " Kuongeza ushirikiano tofauti ili kupunguza ukosefu wa usawa katika huduma za saratani ya watoto".
Mkuu wa wilaya ya Ilemele, Mhe. Hassan Masala akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Hospitali ya Bugando kwa kutoa elimu ya magonjwa ya saratani za Watoto kwani elimu hiyo itakuwa chachu kwa wananchi kuujua ugonjwa huu na kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa wa saratani.
Mhe. Hasan Masala ameendelea kusema takwimu zinaonyesha ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani ya watoto kutoka wagonjwa 50 kwa mwaka 2008 hadi kufikia wagonjwa 350 kwa mwaka 2023, hali inayoashiria ukubwa wa tatizo hili.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuongeza vituo mbalimbali vya utoaji wa huduma za saratani nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lakini pia tafiti mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kujua vyanzo mbalimbali vya tatizo hili.
Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa wilaya, wafadhili na wadau mbalimbali kwa kuendelea kusimama pamoja Bugando kwa hali na mali katika kuhakikisha Bugando inaendelea kutoa huduma za Saratani zinazidi kuimarika.
Pia, ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kuchukua hatua muhimu za kukabiliana na tatizo la Saratani ikiwemo uboreshwa wa miundombinu, kufundisha wataalamu pamoja na kununua mashine za kisasa za matibabu.
BUGANDO YASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAGONJWA DUNIANI MKOANI KIGOMA.
HOSPITALI YA BUGANDO YASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAGONJWA DUNIANI MKOANI KIGOMA.
Maadhimisho ya siku ya wagonjwa Duniani yamefanyika mkoani Kigoma katika Hospitali ya Rufaa ya Kabanga ambapo
maadhimisho hayo yalianza kwa misa takatifu ambayo iliongozwa na Mhashamu baba Askofu mstaafu wa Tabora Askofu Paul Ruzoka.
Mhashamu baba Askofu Ruzoka ameishukuru sana Hospitali ya Bugando kwa kuiongezea nguvu Hospitali ya Kabanga kwani Uwepo wa madaktari bingwa toka Bugando umeiongezea nguvu kubwa Hospitali hiyo, pia Mhasham baba Askofu amewaasa watoa huduma kutoa huduma kwa weledi bila kuweka matabaka kwa wagonjwa.
Akimuwakilisha mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt.Cosmas Mbulwa ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi amesema, "Bugando itaendelea kuleta madaktari bingwa na bingwa bobezi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa"
Dkt.Mbulwa amewahimiza wahudumu wote wa Afya kufuata miongozo na kanuni za utoaji huduma kwa wagonjwa na pia amewaomba wananchi kupima afya zao na kuchangia damu kwa wingi kwani damu husaidia sana kina mama wajawazito na wahanga wa ajali.
Hata hivyo Dkt.Mbulwa amewaasa watoa huduma kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kufanya hivyo huduma za Afya zitazidi kuboreka.
Naye mganga mfawidhi ya Hospitali ya Kabanga Dkt.Peter Kitenyi amewashukuru viongozi na wananchi wote kuhudhuria maadhimisho hayo adhimu bila kuisahau Hospitali ya Bugando kwa mashirikiano mazuri yaliyopo hasa katika kuilea na kuionyesha njia Hospitali hiyo kupitia kambi maalumi zinazofanywa kila mwezi na kwa Hospitali hiyo kupeleka madaktari bingwa katika Hospitali hiyo.
HOSPITALI YA BUGANDO NA TANLIK ZAENDESHA KAMBI YA SIKU NNE YA MATIBABU YA KIBINGWA NA BINGWA BOBEZI KUPITIA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI KUTOKA INDIA NA HOSPITALI YA BUGANDO.
HOSPITALI YA BUGANDO NA TANLIK ZAENDESHA KAMBI YA SIKU NNE YA MATIBABU YA KIBINGWA NA BINGWA BOBEZI KUPITIA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI KUTOKA INDIA NA HOSPITALI YA BUGANDO.
HOSPITALI YA BUGANDO NA TANLIK ZAENDESHA KAMBI YA SIKU NNE YA MATIBABU YA KIBINGWA NA BINGWA BOBEZI KUPITIA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI KUTOKA INDIA NA HOSPITALI YA BUGANDO.
Aidha, Dkt. Fyumagwa Hassan ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANLIK amesema kambi hii ni ushirikiano mzuri uliopo na Hospitali ya Bugando ambapo Madaktari hawa kutoka nje wamekuwa na mchango mkubwa katika kupeana uzoefu na Madaktari wa Bugando ikiwa ni kutimiza lengo la kufikisha huduma bora za Kibingwa na Bingwa Bobezi kwa Wananchi.
Mwisho Dkt. Sachin Mahajan ambaye ni Daktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa upasuaji wa Kichwa, Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka Hospitali ya Sahydran ya India amemaliza kwa kusema mazingira ya kutoa huduma za matibabu ya Kibingwa katika Hospitali ya Bugando ni nzuri kuweza kuwahudumia Wananchi wengi na hivyo amewahimiza wananchi wa Mwanza na viunga vyake kufika na kupatiwa huduma.
HOSPITALI YA BUGANDO NA TANLIK ZAENDESHA KAMBI YA SIKU NNE YA MATIBABU YA KIBINGWA NA BINGWA BOBEZI KUPITIA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI KUTOKA INDIA NA HOSPITALI YA BUGANDO.
HOSPITALI YA BUGANDO NA TANLIK ZAENDESHA KAMBI YA SIKU NNE YA MATIBABU YA KIBINGWA NA BINGWA BOBEZI KUPITIA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI KUTOKA INDIA NA HOSPITALI YA BUGANDO.
HOSPITALI YA BUGANDO NA TANLIK ZAENDESHA KAMBI YA SIKU NNE YA MATIBABU YA KIBINGWA NA BINGWA BOBEZI KUPITIA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI KUTOKA INDIA NA HOSPITALI YA BUGANDO.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Kliniki yake ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi(Bugando Specialized Polyclinic - BSPC) iliyopo Nera Jijini Mwanza, imezindua rasmi kambi kubwa ya siku nne ya matibabu ya Kibingwa Bobezi ya Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio(ENT), matibabu ya ubongo, uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu kupitia Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Sahyadri ya India kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa Bobezi wa Hospitali ya Bugando, kambi iliyoanza hii leo Februari 06, 2025 mpaka February 09, 2025 ikidhaminiwa na Shirika la TANLIK Medical Tourism Agency. Akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Sr. Dkt Alicia Masenga ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji amepongeza huduma za Madaktari hao kwa kujitoa na kuhudumia Wananchi na kuwaasa Wananchi kutumia vyema fursa hiyo adhimu. "Tuko tayari kuwahudumua kwa ubora wa hali ya juu kwani Bugando ina wataalam na vifaa vya kutosha ambapo kwa kweli kupitia huduma hizi ambazo badala ya kusafiri kufuata huduma hizi nje ya nchi sasa unaweza kuzipata hapa Bugando na kupunguza gharama kubwa ambayo ingetumika, tumekuwa tukishirikiana vyema na Madaktari hawa na wengine kutoka nje nchi katika kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo, niwasihi tu mtumie vyema fursa hii na msiwe wachoyo nkitoka hapa muwambie na wengine waje kupata huduma hizi muhimu" Kwa upande wa Dkt. Samson Kichiba ambaye ni Meneja wa Kliniki ya BSPC ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Bugando na Shirika la TANLIK kwa kuleta kambi hii muhimu katika kutoa huduma bora za Kibingwa na Bingwa Bobezi ambazo zilikuwa zinapatikana nje ya nchi lakini Sasa zinapatikana Bugando na kambi hii ikisadia kufikisha huduma hizo karibu zaidi na Wananchi.
MADAKTARI KUTOKA NCHINI INDIA WAWASILI HOSPITALI YA BUGANDO
MADAKTARI KUTOKA NCHINI INDIA WAWASILI HOSPITALI YA BUGANDO
MADAKTARI KUTOKA NCHINI INDIA WAWASILI HOSPITALI YA BUGANDO
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Februari 5, 2025 imetembelewa na Madaktari Bingwa bobezi kutoka Hospitali ya Sahyadri iliyopo mjini pune - India waliofika kwa ajili ya Kambi ya matibabu ya kibingwa bobezi yanayohusisha magonjwa ya Pua, Koo,Masikio (ENT), ubongo, uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu katika Kliniki ya Madaktari Bingwa na Bingwa bobezi (Bugando Specialized polyclinic -Nera).
Akizungumza katika ujio wa Madaktari hao Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewakaribisha Madaktari hao katika kliniki ya Madaktari Bingwa na Bingwa bobezi ya Bugando Specialized polyclinic-Nera na kusema "Ni matumaini yetu kwamba kupitia kambi hii tutabadilishana ujuzi na kupeana uzoefu katika kazi kwani malengo yetu na nia zetu katika mashirikiano haya ni kusogeza huduma za kibingwa bobezi kwa wananchi kwa kutoa huduma zilizo boreka".
Dkt.Massaga ameendelea kueleza umuhimu wa mashirikiano haya kwa timu ya Madaktari wa Bungando kwani kupitia kambi hii tutajengeana uwezo wa hali ya juu katika utendaji kazi.
Naye Dkt. Samson Kichiba ambaye ni Meneja wa Kliniki ya Bugando amemshukuru Dkt. Massaga na uongozi mzima wa Hospitali kwa kuendelea kusimama pamoja nao hata katika suala zima la mashirikiano na kusema " Tunaenda kuanza kambi hii kwa kushirikiana na Madaktari wa Sahyadri kuanzia Februari 6 hadi 9, 2025 ambapo tutafanya uchunguzi wa kina na upasuaji wa magonjwa ya koo,pua,masikio,ubongo pamoja na mishipa ya fahamu na ni matumaini yetu kwamba wagonjwa 200 wataenda kunufaika na kambi hii".
BUGANDO YAFANYA MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI
HOSPITALI YA BUGANDO YAFANYA MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI
Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt.Fabian A.Massaga ameipongeza idara ya Saratani kwa kufanikisha maadhimisho ya siku ya Saratani na kutoa huduma za upimaji bure kwa wananchi wa Mwanza na kusema kuwa Hospitali ya Bugando inahudumia wagonjwa 2,000 wapya kwa mwaka na kati ya hao 80% ya wagonjwa hufika Hospitalini wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa huu.
Dkt.Massaga ametoa takwimu ya ugonjwa wa Saratani kwa Dunia nzima ambapo kwa mwaka watu wanaogundulika na saratani ni 19,000,000 na watu 10,000,000 hufariki kwa ugonjwa huu ndani ya mwaka mmoja.
Tatizo la saratani ni kubwa na ugonjwa huu unaongezeka kwa kasi sana.Kwa Tanzania watu 45,000 hugundulika kuwa na saratani na kati ya hao watu 29,000 hufariki.Saratani za mlango wa kizazi,matiti, tezi dume na umio zimekuwa ni saratani zinazowapata zaidi Wananchi wa Tanzania, na vitu vinavyochochea ongezeko la saratani hizi ni matumizi ya tumbaku,unywaji wa pombe kupita kiasi na kutofanya mazoezi pamoja na kuchelewa kupata matibabu kitu kinachopelekea mgonjwa wa saratani kufariki.
Serikali yetu imekuwa ikiongeza juhudi za kutatua tatizo hili kwa kutoa chanjo ya HPV kwa wasichana ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi na kampeni za uchunguzi wa saratani mbalimbali.
Dkt.Massaga ameongeza kwa kusema kuwa Bugando inaendelea kutoa elimu kwa jamii inayolenga kuongeza uelewa wa ugonjwa wa saratani na umuhimu wa kufanya uchunguzi mapema.
Hata hivyo Dkt.Massaga ameongeza kwa kusema Bugando Health Marathon msimu wa kwanza imekuwa chachu katika kutoa elimu, kufanya mazoezi na kuboresha huduma za saratani.Amewashukuru wananchi wote walioshiriki katika mbio hizo kwani Michango na pesa zimewasaidia sana wagonjwa wa saratani,
Mkurugenzi mkuu ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuunga mkono wagonjwa wa Saratani kwa kushiriki mbio za Bugando Health Marathon msimu wa pili zitakazofanyika mapema mwezi Agosti, 2025.
BUGANDO SPECIALIZED POLYCLINIC YAANZA KUFANYA KIPIMO CHA BRONCHOSCOPY
KILINIKI YA HOSPITALI YA BUGANDO YA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI(BSPC) YAANZA KUFANYA UCHUNGUZI KWA KIPIMO CHA BRONCHOSCOPY.
Kliniki ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi Bugando Specialized polyclinic) iliyopo Nera jijina Mwanza, leo Februari 03, 2025 imeanza kufanya huduma za kipimo cha Bronchoscopy kwa mara ya kwanza chenye uwezo wa kufanya uchunguzi na matibabu ya mfumo wa upumuaji na mapafu kwa kutumia Kamera.
"Kipimo hiki ni kipimo salama na chenye ufanisi wa hali ya juu kinachosaidia kugundua na kutibu (diagnostic and therapitical ) Magonjwa kama kifua kikuu, vivimbe mbalimbali kwenye njia ya hewa na mapafu" ameyasema hayo Dkt. Elizabeth Kwiyolecha ambaye ni Daktari Bingwa Bobezi wa mfumo wa upumuaji.
Naye Dkt. Samson Kichiba ambaye ni Meneja wa Kliniki ya Madaktari Bingwa na Bingwa bobezi amewashukuru wataalamu wa mfumo wa hewa na mapafu kwani huduma hii ni huduma ya Kibingwa na Bingwa bobezi ambayo itakuwa inapatikana katika kliniki hii ya Nera kwa wagonjwa wote wenye uhitaji wa uchunguzi wa kina na matibabu ya mfumo wa hewa.
BUGANDO YASOGEZEA WANANCHI HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA SARATANI.
HOSPITALI YA BUGANDO YASOGEZEA WANANCHI HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA SARATANI.
Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Saratani duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Februari 04, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inatoa huduma bure za upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi, tezi dume, matiti , magonjwa yasioambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la damu.
Upimaji huu unafanyika Kliniki ya Madaktari Bingwa - Nera ( Bugando Specialized polyclinic) na siku ya kilele cha maadhimisho haya yatafanyika katika viwanja vya Hospitali ya Bugando yakiwa na kauli mbiu isemayo "Ungana kwa Upekee"
BUGANDO YAPATA UGENI KUTOKA NEST 360 {NEW BORN ESSENTIAL SOLUTION AND TECHNOLOGY
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata fursa ya kutembelewa na Nest 360(New born Essential Solution and Technology)
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata fursa ya kutembelewa na Nest 360(New born Essential Solution and Technology) mradi ambao unajishughulisha na kupunguza pamoja na kutatua changamoto zinazozuia kutoa huduma jumuishi za watoto wachanga.
Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amefurahishwa na ujio huu ambao una lengo la kuboresha zaidi huduma za watoto wachanga ambao ni viongozi wa taifa la baadae na kuahidi kuendeleza mashirikiano hayo adhimu.
Hata hivyo wageni kutoka Nest 360 wakiongozwa na Dkt. Honorati Massanja ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Afya Ifakara na mradi wa Nest 360 amefurahishwa sana na mapokezi toka Hospitali ya Bugando na kusema kuwa kupitia mradi huo Bugando itapata uwezo wa kusaidia Hospitali nyingine mkoani Mwanza ikiwa ni pamoja na kujengea uwezo Hospitali hizo na kusema kuwa mradi huu utasaidia sana kupunguza vifo vya watoto.Dkt Honorati ameahidi kuwa karibu na kuendeleza ushirikiano mzuri na Hospitali ya Bugando.
Aidha ujio huu umekuwa na lengo la kutoa mafunzo kwa wahudumu wa Afya, kuboresha utunzaji na utumiaji wa takwimu za watoto wachanga, kutoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali ya Bugando na kutumia teknolojia katika suala zima la kuboresha afya na kuondoa vifo vya watoto wachanga.
HOSPITALI YA BUGANDO YAPOKEA UGENI KUTOKA DENMARK
TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU(NIMR) PAMOJA NA WATAALAMU KUTOKA DENMARK KUENDELEKEZA MASHIRIKIANO NA HOSPITALI YA BUGANDO.
TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU(NIMR) PAMOJA NA WATAALAMU KUTOKA DENMARK KUENDELEKEZA MASHIRIKIANO NA HOSPITALI YA BUGANDO.
Watafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wanaoshirikiana na Watafiti kutoka Copenhagen nchini Denmark wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kuangalia fursa na kuendeleza ushirikiano katika Utafiti wa Magonjwa mbalimbali ikiwemo Kifua Kikuu, Virusi vya UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza leo tarehe 09 Januari, 2025.
Wageni hao wamepokelewa na kukaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dkt. Fabian A. Massaga na Viongozi wengine ambapo wameelezwa namna Hospitali ya Bugando na Chuo Kikuu cha CUHAS wamekuwa wakishirikiana na NIMR kufanya tafiti za Magonjwa mbalimbali na kupata fursa ya kutembelea Idara kadhaa ikiwemo Idara ya Radiolojia na Saratani.
"Ni furaha kubwa kushirikiana na kufanya kazi na nyie na Kwa ujio huu ushirikiano wa Bugando, NIMR na Dernamk utaleta matunda makubwa, katika Hospitali ya Bugando kwa kushirikiana na chuo kikuu CUHAS tafiti zimekuwa nguzo kuu.Kanda ya Ziwa imekuwa na changamoto ya Magonjwa yasiyoambukiza hivyo mmefika muda muafaka na sisi kama Hospitali tuko tayari kushirikiana nanyi kwenye kila nyanja na kufanya tafiti hizi muhimu kwani ni kipaumbele chetu" Amesema hayo Dkt. Massaga.
Aidha, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya kuambukiza kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen, Dernamk Prof. Daniel Faurholt amesema ushirikiano huu uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 sasa ni muhimu katika Sayansi, Mabadiliko ya hali ya hewa na tafiti mbalimbali kupambana na Magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza yaliyo tishio hivi sasa.
VIONGOZI WA MENEJIMENTI WAPEWA KONGOLE KATIKA UTENDAJI KAZI.
VIONGOZI WA MENEJIMENTI WAPEWA KONGOLE KATIKA UTENDAJI KAZI.
Uongozi na menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanya kikao cha mwisho wa mwaka kwa lengo la kufanya tathmini, maboresho, mapendekezo na kutoa Dira ya Hospitali kwa mwaka 2025 ambapo viongozi wamepata wasaa mzuri wa kutoa mapendekezo mbalimbali juu ya uboreshwaji wa huduma.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian A. Massaga amewapongeza Wakuu wa Idara na vitengo kwa ushauri na michango mbalimbali na kusema
"Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya sisi kama menejimenti tunafahamu mchango wenu katika Hospitali hivyo niwaombe kuendelea kufanya kazi kwa kujituma zaidi katika mwaka ujao wa 2025 huku tukizingatia kutoa huduma bora kwa wagonjwa"
Dkt.Massaga ameendelea kusisitiza suala zima la uaminifu na uadilifu kazini na kuwataka viongozi hao kuendelea kusimamia miongozo na taratibu ya kazi pamoja na kutengeneza mazingira rafiki ya kazi.
Hata hivyo wakuu wa Idara na vitengo wamepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na uongozi wa Hospitali katika kuboresha huduma na kuweka mazingira rafiki ya kazi kwani kwa kufanya hivyo huduma zitazidi kuimarika.
UONGOZI WA HOSPITALI YA BUGANDO UMEFANYA KIKAO CHA PAMOJA NA WATUMISHI KUELEKEA MWISHO WA MWAKA WA KALENDA 2024
HOSPITALI YA BUGANDO UMEFANYA KIKAO CHA PAMOJA NA WATUMISHI KUELEKEA MWISHO WA MWAKA WA KALENDA 2024
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Askofu Renatus Nkwande leo Desemba 19, 2024 umekaa kikao cha pamoja na watumishi kwa lengo la kutakiana kheri ya sikukuu za Mwisho wa Mwaka
" Mimi niwatakie kheri ya sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya na kuwapongeza kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi hiki, zipo sifa nyingi nzuri tunazozipata kutokana na kazi kubwa mnayoifanya, hatujafikia ukamilifu lakini hapa tulipo tunawapongeza sana na niwashukuru kwa majitoleo yenu na kujituma na ninasisitiza suala la uaminifu na huduma bora" Mhashamu Askofu Nkwande
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga
amewashukuru wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando,CUHAS, MWACHAS na Viongozi kwa ushirikiano na kuongeza kuwa,
"Sisi kama Menejimenti tuliona tukae pamoja na Watumishi wote kabla ya sikukuu za mwisho ya Mwaka tuje tutakiane heri, tumefanya mengi mazuri lakini changamoto pia zimeweza kutukumba na leo tupo hapa tunamuomba Mungu azidi kutulinda
" Dkt. Massaga.
Dkt. Massaga pia amazungumzia maboresho na miradi inayoenda kutekelezwa na Hospitali ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa matibabu ya figo kwakuanzisha huduma ya upandikizaji wa figo, uboreshaji wa tiba mionzi, saratani na ununuzi wa mashine na vifaa tiba pamoja na dawa ambapo tayari Hospitali iimeanza kupokea dawa toka India, ukamilishaji wa mradi wa Bugando Hoteli na ujenzi wa jengo la kisasa la Wagonjwa wa nje (OPD).
Kikao hiki cha pamoja kimeambatana na utoaji wa zawadi ya Mchele kwa watumishi wote ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya pamoja na siku maalum ya Bugando day ambayo huadhimishwa mwishoni mwa kila mwaka huku zoezi hili likiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali, Mhashamu Askofu Renatus Nkwande.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Maabara leo Disemba 11, 2014 imefanya kikao chake cha mwaka (Management Review Meeting)
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Maabara leo Disemba 11, 2014 imefanya kikao chake cha mwaka (Management Review Meeting)
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Maabara leo Disemba 11, 2014 imefanya kikao chake cha mwaka (Management Review Meeting) ikiwa ni takwa la muongozo wa Kimataifa wa maabara za Afya yaani ISO 15189 : 2022 lengo likiwa ni kujadili utendaji wa ubora wa huduma za maabara pamoja na kujadili maendeleo, mafanikio na changamoto za utekelezaji wa huduma zake.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi Dkt. Cosmass Mbulwa ameshukuru na kupongeza kurugenzi pamoja na Idara mbalimbali kwa jitihada na mchango wanaoutoa katika kuhakikisha huduma za maabara zinaendelea kutolewa katika ubora na kiwango stahiki kwa wateja.
Na kusema "Idara ya maabara kupitia kikao hiki inaweza kuendelea kufanya vizuri zaidi kwa kuwa kikao hiki kinatupatia nafasi ya kuweka mikakati mbalimbali ya kiutendaji na kuboresha zaidi huduma kwa wateja ndani na nje ya Hospitali"
Aidha amewaomba Watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia miongozo na taratibu za kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maabara Esther Reuben amemshukuru Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi na uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa ujumla kwa kuendelea kuonyesha ushirikiano wa hali na mali katika kuhakikisha huduma za maabara zinasonga mbele.
HOSPITALI YA BUGANDO YAENDESHA UCHUNGUZI WA AFYA WILAYANI BUSEGA
HOSPITALI YA BUGANDO YAENDESHA UCHUNGUZI WA AFYA WILAYANI BUSEGA
HOSPITALI YA BUGANDO YAENDESHA UCHUNGUZI WA AFYA WILAYANI BUSEGA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Mionzi imeendesha huduma ya Uchunguzi wa magonjwa ya Ini, Figo na Tezi Dume kwa wananchi wa Wilaya ya Busega, huduma hii ya siku mbili inafanyika katika Kituo cha Afya Igalukilo, Wilaya ya Busega Mkoa wa Simiyu.
Akizungumzia zoezi hili, Dkt. Nelson Azande ametanabaisha kuwa
"Miongoni mwa tuliowafanyia uchunguzi wamekutwa na changamoto
ya Ini inayotokana na Kichocho na wengine Figo inayotokana na Tezi dume na tumewaelekeza wafike Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi na matibabu"
Dkt. Azande pia ametumia nafasi hii kutoa wito kwa jamii kutumia fursa hii adhimu ya kupata huduma ya kuchunguza afya bure na kushughulikia changamoto kwa wakati.
Hospitali ya Bugando imekua na utaratibu wa kuendesha huduma ya uchunguzi na tiba Mkoba wa magonjwa mbalimbali kwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao kwa lengo la kugundua mapema changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa wakati kabla ya kufikia hatua mbaya.
SHIRIKA LA FIC LATEMBELEA BUGANDO.
SHIRIKA LA FIC LATEMBELEA BUGANDO.
SHIRIKA LA FIC LATEMBELEA BUGANDO.
Wanachama wa Shirika la Kimataifa linalojihusisha na Michezo la Football International Charity wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Novemba 30, 2024 kwa lengo la kutoa mkono wa pole kwa Wagonjwa wa Saratani ikiwa ni moja ya dhima ya kikundi hicho katika kuelimisha jamii na kusaidia watu wenye uhitaji.
Bwn. Joseph Mathius ambaye ni Muuguzi Kiongozi katika Idara ya Saratani ameushukuru uongozi wa Shirika hilo la Kimataifa la michezo kwa msaada na majitoleo yao kwa Wagonjwa wa saratani.
Naye Bwn. Mosses Maduhu ambaye ni kiongozi Msaidizi wa Jukwaa la Football International Charity Kanda ya Ziwa ametoa shukrani kwa uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kukubali na kufanikisha ombi Lao kwani jambo hili limewagusa kwa kiasi kikubwa na kusema
" Sisi tuko tayari kushirikiana na Hospitali ya Bugando katika suala zima la kuelimisha jamii juu ya elimu ya Afya na kusaidia watu mbalimbali wenye uhitaji ".
HOSPITALI YA BUGANDO YAJIPANGA KUPANDIKIZA FIGO KUANZIA MWAKA 2025
HOSPITALI YA BUGANDO YAJIPANGA KUPANDIKIZA FIGO KUANZIA MWAKA 2025
HOSPITALI YA BUGANDO YAJIPANGA KUPANDIKIZA FIGO KUANZIA MWAKA 2025
Timu ya wakaguzi kutoka Wizara ya Afya imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kukagua utayari wa Hospitali hiyo katika huduma ya kupandikiza Figo, miondombinu, manunuzi, Wataalamu na uzingatiaji wa miongozo katika kuanzisha huduma hiyo inayotarajiwa kuanza kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2025.
Akimuwakilisha mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dkt.Bahati Wajanga ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba amewashukuru wakaguzi kutoka Wizara ya Afya na kusema,
"Haikuwa kazi rahisi kwa Wizara na Serikali kukubali Hospitali ya Bugando kuweza kutoa huduma hii, wigo umetanuliwa na sisi tunatakiwa kutimiza tu vigezo na Viongozi wametupa mrejesho huu chanya na sisi kama Uongozi ni jukumu letu kuwa tayari kupokea maboresho yote na kuyafanyia kazi ili huduma hii itakapoanza iweze kufanya vizuri zaidi".
Naye Shadrack Buswelu ambaye ni Mratibu wa Huduma za Figo wa Wizara ya Afya na Mkuu wa timu ya ukaguzi ameipongeza Hospitali ya Bugando kwa maandalizi mazuri na kusema kuwa wameridhishwa kwa hatua iliyofikiwa mpaka sasa,
"Tumefurahishwa kwa namna mlivyojiandaa, wataalamu wapo, vifaa vipo, Watumishi wapo tayari kuanza huduma ya upandikizaji ambao umefikia asilimia 95%, tunaondoka hapa tukiacha marekebisho machache na mwakani tujiandae kuanza upandikizaji " .Amesema hayo Dkt. Shadrack Buswelu.
Wataalam hao wa ukaguzi wa maandalizi ya upandikizaji wa Figo kutoka Wizara ya Afya wametembelea maeneo muhimu ikiwemo Vyumba vya Wagonjwa Mahututi(ICU), Vyumba vya upasuaji(Theater), Maabara pamoja na duka la madawa (Famasi).
ANASTY MICROFINANCE LTD WATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO KUONA WAGONJWA.
ANASTY MICROFINANCE LTD WATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO KUONA WAGONJWA.
ANASTY MICROFINANCE LTD WATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO KUONA WAGONJWA.
Kikundi cha mikopo cha Anasty Microfinance Ltd cha Jijini Mwanza leo terehe 09 Novemba 2024, kimetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kuona, kuwafariji na kuwapa mkono wa pole Wagonjwa katika Idara ya Saratani.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitu mbalimbali ikiwemo mafuta, sabuni, pampasi, tishu na vitabu, Mkurugenzi wa kikundi hicho chenye Wanachama 10, Bi Esther Stephen amesema ujio wao katika Hospitali ya Bugando umelenga kutimiza malengo yao ya mwaka ya kurudisha kwa jamii na hivyo kuamua kuelekeza mkono wao wa pole kwa Wagonjwa wanaoteseka na Saratani.
"Tunashukuru sana kwa ukaribisho wenu na kutupokea, tumekuwa tukisikia na kuona jinsi Wagonjwa wa Saratani wanavyoteseka, tunaamini kupitia hiki kidogo tulichojaliwa kitaenda kuwagusa kwa namna Moja ama nyingine katika kusadia matibabu yao hasa kwa wale wanaowahudumia"
Kwa upande wake Muuguzi Dativa Zelamla akimwakilisha Mkuu wa Idara ya Saratani wa Hospitali ya Bugando, amewashukuru wanakikundi hao kwa ujio wao kuwaona Wagonjwa, na akiwaambia misaada hiyo ina maana kubwa katika kuwasaidia Wagonjwa kwani matibabu ya Saratani yana Gharama kubwa na ni ya muda mrefu hivyo itaenda kusaidia kupunguzia familia makali ya kuwahudumia na kuwaomba kuendelea na moyo huo huo wa utoaji.
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO YAENDESHA KAMBI YA UPASUAJI WA USO NA UPANDIKIZAJI WA TAYA BANDIA.
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO YAENDESHA KAMBI YA UPASUAJI WA USO NA UPANDIKIZAJI WA TAYA BANDIA.
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO YAENDESHA KAMBI YA UPASUAJI WA USO NA UPANDIKIZAJI WA TAYA BANDIA. Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha kambi maalumu ya upasuaji wa uso na taya lengo likiwa ni kusadia wagonjwa wenye matatizo katika uso, kinywa na meno kwa kuwarejeshea muonekano mpya. kambi hiyo imefanywa kwa wagonjwa kumi na wawili (12) huku watano (5)wakiwa wamepandikizwa taya bandia.
BMC SACCOS LTD YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA
BMC SACCOS LTD YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA
Chama cha kuweka na kukopa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC SACCOS LTD) kimefanya Mkutano Mkuu wa ishirini wa mwaka leo Oktoba 26, 2024 kikiwa kimekutanisha Wanachama ambao ni Watumishi kutoka BMC, CUHAS na MWACHAS pamoja na Uongozi wa Chama cha Bodi hiyo. Mkutano huo ambao hufanyika mara moja kila mwaka, umeendeshwa kwa kuanza na semina kwa Wanachama wote washiriki wa Mkutano huku ukiongozwa na Bw. Justine Joseph kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Mkoa wa Mwanza, ikiwa na leongo la kuwakumbusha Wanachama kutambua na kuelimisha kuhusu miongozo na sera zilizowekwa na Chama hicho.
Akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando ambaye ni Mgeni Rasmi katika Mkutano huo Dkt. Bahati Wajanga Mkurugenzi wa Huduma za Tiba amesema, “Nawapongeza Uongozi wa BMC SACCOS kwa hatua mliopiga maendeleo ni mazuri, Wanachama wameongezeka na michango imeongezeka. Lakini pia tusiishie hapa tu bali nawaomba Viongozi muendelee kuwasisitiza Watumishi kujiunga katika Chama hiki, kutengeneza vipeperushi vyakutosha na kuongeza wigo, ili Watumishi waweze kuielewa vizuri SACCOS na kujiunga zaidi."
Hata hivyo Dkt. Bahati Wajanga amewashukuru na kuwapongeza Wanachama wote waliokwisha jiunga na Chama hicho cha BMC SACCOS na kusisitiza waendelee kufuata sera, dira na mipango mikakati iliyowekwa na Chama, ili kila mmoja kwa wakati wake aweze kunufaika nayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha BMC SACCOS Bw. Richard Masunga amemshukuru Mgeni rasmi Dkt. Bahati Wajanga kwa kuweza kushiriki katika Mkutano huo, nakuomba uongozi wa juu uweze kuliona hili na kusisitiza Watumishi wa BMC, CUHAS na MWACHAS waendelee kujiunga katika Chama hicho cha BMC SACCOS LTD kwa manufaa na maendeleo yao binafsi.
WANAFUNZI 35 WAHITIMU MAFUNZO YA UHUDUMU MOCHWARI-BUGANDO
WANAFUNZI 35 WAHITIMU MAFUNZO YA UHUDUMU MOCHWARI-BUGANDO
Wanafunzi thelathini na watano kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wamehitimu mafunzo ya huduma za mochwari.
Akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Mkurugenzi wa Huduma za Afya Saidizi na mgeni rasmi katika hafla hiyo Dkt. Cosmas Mbulwa, amempongeza Dkt. Kahima kwa ubunifu huu wa kuanzisha mafunzo haya, pia amewapongeza wahitimu kwa hatua waliyofikia."Nawaombeni mliyojifunza mkayafanyie kazi kwa waledi na kuepuka rushwa.Hata hivyo Hospitali ya Bugando kwa kushirikiana na Chuo cha CUHAS tuko mbioni kuanzisha programm hii kwa ngazi ya Diploma" amesema Dkt. Mbulwa.
Sambamba na hayo Dkt. Cosmas Mbulwa hakusita kuipongeza na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha huduma za mochwari, na kuupongeza Uongozi wa Hospitali ya Bugando hususani Mkurugenzi Mkuu kwa kuwa na utayari wa kukubali na kuhurusu mafunzo hayo ambayo yana tija na manufaa kwa jamii na Taifa kwa Ujumla
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt. Jackson Kahima amewaasa wahitimu kuwa watiifu na wanyenyekevu katika kazi na kuwaomba wakawe chachu katika kutoa huduma bora za mochwari.
Waumini kutoka Parokia ya watakatifu wote Kiloleli wakiongozwa na Paroko Joseph Mchole wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Waumini kutoka Parokia ya watakatifu wote Kiloleli wakiongozwa na Paroko Joseph Mchole wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Waumini kutoka Parokia ya watakatifu wote Kiloleli wakiongozwa na Paroko Joseph Mchole wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kuunga mkono uongozi wa Bugando katika kuchangia matibabu ya Watoto wenye saratani (Bugando Health Marathon).
Dkt. Fabian A. Massaga ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando amesema
"Kwa niaba ya Hospitali ya Bugando nikushukuru Paroko Joseph Mchole pamoja na waumini wote kwa kuwa na hamasa na kuguswa na suala la mbio hizi, kipekee nimefarijika kwa majitoleo yenu yatakayoenda kusaidia watoto hawa na kuweza kutimiza ndoto zao za baadae"
KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA DKT. JOHN JINGU ATEMBELEA CHUO CHA MWACHAS.
KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA DKT. JOHN JINGU ATEMBELEA CHUO CHA MWACHAS.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amefanya ziara katika Chuo cha MWACHAS jijini Mwanza kwa lengo la kuona shughuli za maendeleo, mazingira ya wanafunzi pamoja na kuzungumza na Wanafunzi wa chuo hicho.
Akizungumza wakati wa Kikao Wamafunzi pamoja na Uongozi wa Chuo cha MWACHAS, Dkt. Jingu amepongeza uongozi kwa jinsi wanavyofanya kazi yao vizuri na kuwapa moyo Wanafunzi kuwa wapo sehemu sahihi ya kupata taaluma yenye tija kwa jamii.
"Niwapongeze kwa shughuli za maendeleo zinazokwenda vizuri, Wanafunzi wametulia, baadhi ya changamoto zipo lakini hazijawakwamisha kufanya vizuri, kikubwa tunachofanya Serikali ni kuhakikisha mazingira sahihi ya kutengeneza wataalamu yapo sawa kwani utoaji wa huduma unategemea Watalamu wenye ubobezi na uwezo, na hapa kuna faida ya uwepo wa Hospitali ya Bugando mnaoshirikiana nao vyema kwa Wanafunzi kupata mafunzo ya vitendo na kupata wataalamu bora na wenye tija, hongereni sana"
Aidha Dkt. Jingu amewaasa Wanafunzi kutumia vizuri fursa waliyopata ya kujiunga na Chuo cha MWACHAS, kwani wapo sehemu sahihi na wanahitajika sana na jamii kwenda kutoa huduma.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Kaimu Mkuu wa Chuo, Lazaro Makungu ambaye ni Afisa Utumishi amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kutembea MWACHAS na hiyo imewapa faraja katika kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kupanua eneo la chuo ili kuhimili Wanafunzi wengi zaidi na kutekeleza Lengo la Serikali la kuzalisha Wataalam wenye weledi na uwezo kusaidia jamii.
BUGANDO FITNESS YASHIRIKI MBIO ZA HISANI ZA KUMBUKUMBU YA MIAKA 25 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWL. JULIUS K. NYERERE MKOANI MWANZA
BUGANDO FITNESS YASHIRIKI MBIO ZA HISANI ZA KUMBUKUMBU YA MIAKA 25 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWL. JULIUS K. NYERERE MKOANI MWANZA
Klabu ya mazoezi ya Bugando (Bugando Fitness) imeshiriki katika mbio za hisani za kumbukumbu ya miaka 25 ya kifo Cha Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius K. Nyerere ambapo mbio hizi zimeratibiwa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza baada ya mbio hizi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayoub Rioba pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa maandalizi na ubunifu mzuri katika kumbukizi hii ya kifo cha Baba wa Taifa na kuwaomba ubunifu huu uwe endelevu Kila mwaka tunapoenzi kumbukizi hii.
"Matembezi haya yametufanya tuwe marafiki na tuzidi kuwa wamoja na ni matumaini yangu kwamba kupitia mbio hizi tutayaenzi yale yote mema na mazuri aliyoyatenda Hayati Mwl. Julius K. Nyerere na hasa katika uongozi wake na tukatumie falsafa aliyoijenga ya kuwa na umoja, amani na upendo ambapo yote haya tunayaona pia kwa Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan".
Mhe.Said Mtanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amezipongeza klabu mbalimbali zilizoshiriki na kuunga mkono mbio hizi ikiwemo klabu ya Bugando Fitness pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga Kwa kuwa kiongozi mwenye hamasa hasa katika suala zima la kufanya mazoezi yanayosadia kupunguza wimbi la Magonjwa yasiyoambukiza.
Mazoezi haya yamejikita katika kuboresha miili lakini pia ni maandalizi ya mbio za Bugando Health Marathon zitakazofanyika Oktoba 20, 2024 zikiwa na lengo la kusaidia matibabu ya watoto wenye Saratani.
WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AZINDUA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA VIJANA KITAIFA MKOANI MWANZA
WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AZINDUA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA VIJANA KITAIFA MKOANI MWANZA
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amezindua rasmi Maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa na kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius K. NyerereLeo Oktoba 11, 2024 katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Akizungumza Katika ufunguzi huo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameupongeza Mkoa wa Mwanza kwa maandalizi mazuri ya maadhimisho haya sambamba na ubunifu katika utoaji wa huduma mbalimbali kwenye mabanda na maonesho hayo.
"niwapongeze sana vijana kwa maandalizi na kazi nzuri kuanzia kwenye mabanda yenu, maonyesho haya ni fursa ya vijana kujuana na kuenzi mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amri Abeid Karume kwenye maendeleo ya Taifa letu sambamba na kuja kupata falsafa na historia ya maendeleo ya waasisi wa Taifa letu. Vijana mnayo fursa kwenye eneo la kidijitali katika kuboresha maendeleo endelevu na Kila mmoja anapaswa kuchangamkia fursa hii ambayo si kwaajili ya kurahisisha tu kazi zetu bali kufanya maamuzi yenye tija, hongereni sana Vijana na wote mliopo katika maonesho haya" amesema Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania.
Kwa upande wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Ridhiwani Kikwete amewaasa vijana kutumia fursa ya kidijitali hasa kutumia mifumo wanayotengeneza wenyewe kwenye kufanya kazi zenye tija na manufaa kwa nchi.
Aidha, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewakaribisha Wageni wote wanaofika katika mabanda ya maonyesho yaliyo na huduma mbalimbali ikiwemo za kiafya ambapo Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kiafya bure kwa Wananchi ikiwemo uchunguzi wa saratani mbalimbali, upimaji wa Shinikizo la damu, Sukari, Virusi vya UKIMWI(VVU) pamoja na ushauri wa lishe katika Banda lake la utoaji huduma Furahisha jijini Mwanza.
MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI
MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Oktoba 11, 2024, imeadhimisha siku ya Afya ya Akili Duniani kwa kufanya mazoezi yaliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga katika eneo la maegesho la magari ya Watumishi.
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Fabian A. Massaga amesema, “kwa ulimwengu wetu unaokua kwa kasi, afya mwili imekua ikipewa kipaumbele, hivyo tukubali afya ya akili ni muhimu kama ilivyo kwa afya ya mwili”.
Dkt. Massaga ameendelea kusema kuwa changamoto ya Afya ya akili hutokea kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa uelewa, kunyanyapaliwa na inakadiriwa watu wenye changamoto hizi za afya ya akili asilimia 76 mpaka 85 hawapati matibabu yeyote na wale wanaokuja kupata matibabu ni chini ya asilimia 20.
Maadhimisho haya yameambatana na mafunzo ya stress management yaliyotolewa na Idara ya Afya Akili kwa watumishi wa Bugando, CUHAS na MWACHAS.
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mkuu ameipongeza idara ya Afya ya Akili kwa kazi kubwa inayofanya kwa kuhudumia wagonjwa na watu wenye changamoto ya Afya ya Akili “Tujitoe kufanya Afya ya Akili kuwa kipaumbele katika Taasisi yetu na Taifa kwa ujumla, pamoja tunaweza”
Dr.Massaga ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Afya, Wadau, Wanamichezo, na Taasisi kushiriki katika maadhimisho ya Afya ya Akili Duniani na kuhamasisha suala zima la mbio za Bugando Afya Marathoni zitakazofanyika Oktoba 20, mahususi kwaajili kuchangia watoto wenye saratani.
Aidha Dkt.Matiko Marwa kaimu mkuu wa idara ya Afya ya akili amesema Afya nzuri ya akili huleta mshikamano,kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi na Afya ya mwili kiujumla.Hivyo ni muhimu sana kwa Taasisi kuendesha mafunzo hayo.
Pia Dkt Matiko ameomba watumishi na wanachi wasisite kufika Hospitali Kupata huduma sahihi za kitabibu na kisaikolojia.
HOSPITALI YA BUGANDO YAADHIMISHA SIKU YA AFYA YA MACHO DUNIANI KWA KUFANYA UCHUNGUZI BURE
HOSPITALI YA BUGANDO YAADHIMISHA SIKU YA AFYA YA MACHO DUNIANI KWA KUFANYA UCHUNGUZI BURE
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeungana na Watanzania wote Duniani kuadhimisha siku ya Afya ya Macho Duniani kwa kutoa huduma ya uchunguzi wa macho bure na kutoa elimu kwa Wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo yanayoenda yenye kaulimbiu isemayo "penda macho yako, muhamasishe mtoto apende macho yake"
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando ameipongeza idara ya macho kwa ubunifu huo wa kutoa huduma ya uchunguzi bure na kuwapongeza Wananchi kwa kuhudhuria maadhimisho hayo.
"Tunasema penda macho yako, muhamasishe mtoto apende macho yake, Sisi kama wazazi tuna wajibu wa kuhamasisha Watoto kuyatunza macho yao. Nipongeze kazi kubwa ya Idara ya macho kwa kupima bure Wanafunzi 10,300 wa shule za msingi na Sekondari kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Leo hapa tunatoa huduma bure kwa lengo la kuhakikisha Wananchi wanapata huduma sahihi ya macho"
Aidha, Dkt Massaga ameishukuru serikali kwa uwekezaji mkubwa kwenye eneo la Afya hususani kwenye huduma za macho pamoja na Wadau mbalimbali wa Bugando kama CBM, Moran na KCCO kwa ushirikiano na msaada mkubwa wanaoutoa katika Idara ya Macho na kusisitizana kuwa jukumu la kulinda afya ya macho sio la serikali tu bali ni jukumu letu sote.
BENKI YA NMB YATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO
BENKI YA NMB YATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO
kiwa ni katika wiki ya Huduma kwa wateja Benki ya NMB imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ikiwa ni katika kutoa tathmini, kutambua na kuthamini mchango wa Hospitali ya Bugando huku wakiahidi kutoa huduma bora zaidi kwa Hospitali hiyo.
Dkt.Fabian Massaga ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Bugando amefurahishwa na Ujio wa viongozi wa Benki hiyo na kusema kuwa Bugando itazidi kuendeleza mashirikiano yaliyopo baina yao.
Hata hivyo Benki ya NMB imehamasika na mbio za hisani za Bugando Health Marathon na kuahidi kuwa sehemu ya mbio hizo kwa kuchangia watoto wenye saratani.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata fursa ya kutembelewa na wakurugenzi
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata fursa ya kutembelewa na wakurugenzi
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata fursa ya kutembelewa na wakurugenzi pamoja na viongozi kutoka Hospitali Kilutheri ya Hydom kwa lengo la kubadirishana uwezo na kujifunza namna Bugando inavyoendesha huduma zake.
MAFUNZO YA STRESS MANAGEMENT AT WORK PLACE KWA WAFANYAKAZI -BUGANDO
MAFUNZO YA STRESS MANAGEMENT AT WORK PLACE KWA WAFANYAKAZI -BUGANDO
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendelea kuendesha mafunzo ya namna ya kukabili changamoto katika maeneo ya kazi (Stress Management at work place) kwa Wafanyakazi wa BMC, CUHAS na MWACHAS ikiwa ni katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani ambayo hufanyika Octoba 10, kila mwaka.
Aidha mafunzo hayo ambayo yanahusisha kada mbalimbali katika ngazi ya Hospitali na Chuo yalianza Octoba 1, na yanatarajiwa kumalizika Octoba 9, 2024 yakiwa na lengo la kuboresha utendaji kazi katika maeneo ya kazi ikiwa sanjali na kauli mbiu inayosema ”Ni muda sahihi kufanya afya ya akili kuwa kipaumbele katika maeneo ya kazi.”
BALOZI WA ITALIA NCHINI TANZANIA MH. GIUSEPPE COPPOLA ATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
BALOZI WA ITALIA NCHINI TANZANIA MH. GIUSEPPE COPPOLA ATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi Shirikishi - CUHAS kwa pamoja wametembelewa na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mh. Giuseppe Coppola na Wasaidizi wake kwa lengo la kuona miradi ambayo Italia imekuwa ikishirikiana nao na namna ya utekelezaji na kuona namna ya kuzidi kuboresha mashirikiano hayo muhimu yaliyodumu tangu mwaka 1995.
"Mnakaribishwa sana na ni fahari kubwa kututembelea, Mimi pamoja na Prof. Kamugisha tunawashukuru kwa kuja, ushirikiano huu na nchi ya Italia una historia kubwa tangu mwaka 1995, umekuwa na matokeo chanya sana, mmetusaidia siyo kuanzisha tu Idara ya Saratani bali kuanzisha kituo cha Saratani Kanda ya Ziwa, kupitia usadizi wenu wa Madaktari Bingwa Bobezi na kuanzisha maabara kubwa ya histopatholojia" amesema Dkt Fabian A. Massaga, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando.
Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo cha CUHAS Prof. Erasmus Kamugisha ameshukuru kwa ujio huo wa ubalozi, na kusema mashirikiano kati ya Italia na Chuo cha CUHAS umekuwa msingi wa kuzalisha wataalamu kupitia mafunzo nchini Italia, kuanzisha Shahada ya Uzamili ya (Medicine in Atomical Pathology) pamoja na Watalamu wake katika Chuo cha CUHAS pamoja na kuanzisha Maabara ya Histopatholojia ambayo ni msingi wa uchunguzi wa tishu - Histopatholojia.
Mhe. Balozi Giuseppe Coppola ameshukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kusema; "Ni furaha kubwa kuwepo nanyi hapa, ugeni huu ni mwendelezo wa ushirikiano huu muhimu ambao tumekuwa nao kwa muda na kupitia malengo ya muda mrefu hasa kawajengea uwezo Madaktari kubadilishana ujuzi, kusaidia katika vifaa tiba".
Mhe. Balozi Giuseppe na Wasaidizi wake wamepata nafasi ya kukutana na Wataalam kadhaa waliopo Bugando na CUHAS na kutoa dira ya mwendelezo wa mashirikiano yao na kutembelea jengo la Saratani, Chuo cha CUHAS na kujionea hatua mbalimbali za maendeleo katika Hospitali ya Bugando na Chuo cha CUHAS.
UMOJA WA WATOA HUDUMA ZA AFYA NCHINI WAFANYA KIKAO CHA MWAKA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO JIJINI MWANZA.
Umoja wa watoa huduma za Afya nchini wamefanya kikao chao cha mwaka katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Septemba 28, 2024.
Umoja wa watoa huduma za Afya nchini wamefanya kikao chao cha mwaka katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Septemba 28, 2024 lengo likiwa ni kuzindua chama na katiba ya umoja wa chama cha Tanzania Health Assistant Association (TAHAA) wenye kauli mbiu isemayo "Msaidizi wa Afya ni muhimu katika utekelezaji wa maendeleo ya sekta ya Afya".
"Umoja wa watoa huduma za Afya ulianzishwa Oktoba 20, 2020 kwa lengo la kuunganisha watoa huduma wa Afya Nchi nzima lakini hatukuwa na chama wala katiba rasmi ya kusimamia umoja huu ndio mana leo hii tumeungana watoa huduma kutoka sehemu mbalimbali kwa lengo la kuzindua chama na katiba rasmi ya chama" ameyasema hayo, Ally Mtopwa ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya katiba ya chama cha Wasaidizi wa Afya Tanzania.
Mgeni rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewapongeza watoa huduma za Afya kwa kuchagua Hospitali ya Bugando kama sehemu ya kufanya hafla yao ya uzinduzi wa chama na katiba lakini pia amewapongeza kwa kuanzisha chama hiki cha TAHAA ambacho kitasaidia kuunganisha mawazo na kutatua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika utendaji wao wa kazi. "Nyie ni watu wa muhimu sana katika suala zima la utoaji wa huduma za Afya kwa mgonjwa hivyo niwaombe mkatimize wajibu wenu kwa weledi wa hali ya juu kwa kuwa yote haya tunafanya kwa lengo la kuimarisha huduma za Afya katika Taasisi na Hospitali zetu" Dkt Fabian A. Massaga.
Aidha Dkt.Massaga amewaomba kuonyesha ushirikiano kwa viongozi wao ili waweze kufikia malengo ya chama na na kuwaasa waweze kujiendeleza katika taaluma zao sambamba na kuwaalika kushiriki katika mbio za hisani za Bugando Afya Marathon 2024 zitakazofanyika October 20, 2024 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko (MB).
MAFUNZO YA HUDUMA TABIBU ZA KIFAMASIA (CPS) YAHITIMISHWA BUGANDO
Mkurugenzi wa Huduma za Afya Saidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Cosmas Mbulwa amefunga mafunzo ya siku 10 ya Huduma Tabibu za Kifamasia (Clinical Phamacy Services) yaliyoendeshwa katika Hospitali ya Bugando.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya Saidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Cosmas Mbulwa amefunga mafunzo ya siku 10 ya Huduma Tabibu za Kifamasia (Clinical Phamacy Services) yaliyoendeshwa katika Hospitali ya Bugando.
Mafunzo hayo yaliyohusisha Wafamasia 30 kutoka Mikoa mbalimbali nchini, yamelenga kumfanya Mfamasia kuhusika moja kwa moja kumuhudua Mgonjwa kwa pamoja na Wahudumu wengine wa Afya.
Dkt. Mbulwa amewapongeza waandaaji na washiriki wa mafunzo hayo na kusema;
"Niwapongeza sana waandaji na washiriki kwa mafunzo haya, tuna maendeleo makubwa ya Sayansi na teknolojia hivyo tunahitaji Wafamasia wazuri ili kuimarisha huduma za kiafya, lazima tubadilike na kupitia mafunzo haya ya Huduma Tabibu za Kifamasia muende mkasimamie hili swala, tushirikiane wote namna ya kuhudumia Mgonjwa na naamini kupitia ushirikiano huo wa Madaktari, Wauguzi, Wafamasia na Wataalamu wa Maabara Kwa hakika tutapunguza vifo"
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Idara ya Famasia wa Hospitali ya Bugando Mageni Magembe, amesema mafunzo hayo ya CPS yatakuwa chachu na yataleta tija na ahueni kwa wateja, uvumbuzi wa dawa ni gharama hivyo kunahitajika matunzo sahihi na ni nafasi yao kutumia vizuri walichokijifunza.
Kwa upande wa Professa Omary Minzi, ambaye ni Mwanzilishi wa Huduma Tabibu za Kifamasia (CPS) na mkufunzi kwenye mafunzo hayo, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Bugando na washiriki wote na kusema Mfamasia lazima uwe na kazi nyingi, tunataka kuongeza wigo wa Wafamasia katika kazi na lazima kuzingatia uingizaji sahihi wa takwimu kwenye mfumo.
Mafunzo ya siku 10 ya Huduma Tabibu za Kifamasia yamehusisha Wafamasia 30 kutoka Mikoa ya Mwanza, Kigoma, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mara na Kilimanjaro na kuhitimishwa hii Leo tarehe 27 Septemba, 2024 katika Hospitali ya Bugando.
HOSPITALI YA BUGANDO YAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKO SELI(SELIMUNDU) KWA WATAALAMU WA AFYA WA MKOA WA MWANZA
Mafunzo ya siku nne kwa wataalam wa Afya ikiwemo Madaktari, Wauguzi na wataalam wa Maabara kutoka Hospitali mbalimbali za Mkoa wa Mwanza, yaliyoendeshwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando yamehitimishwa leo Septemba 26, 2024.
Mafunzo ya siku nne kwa wataalam wa Afya ikiwemo Madaktari, Wauguzi na wataalam wa Maabara kutoka Hospitali mbalimbali za Mkoa wa Mwanza, yaliyoendeshwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando yamehitimishwa leo Septemba 26, 2024 yenye lengo la kujenga uelewa wa kutambua mapema vimelea vya ugonjwa wa siko seli kwa mtoto.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi MUHAS Dkt. Lulu Chirande ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kuwezesha mafunzo hayo muhimu kwa wataalam wa Afya ambayo yatasaidia kutambua mapema siko seli kwa mtoto kuanzia ngazi ya vituo vya Afya.
"Niwapongeza sana kwa kupata mafunzo haya muhimu, kwa siku hizi nne naamini mlichokipata ni kikubwa na Kwa hakika mtakaporudi sasa kwenye vituo vyenu mtaenda kutumia ujuzi huu na kuwapatia wengine mliowaacha, takwimu zinaonesha Kanda ya Ziwa inayo watoto wengi na watu wazima wenye siko seli hivyo, mwisho wa mafunzo haya ndio mwanzo wa kufanya kazi kwa ukubwa zaidi, na Kwa kipekee niushukuru uongozi wa Bugando kwa kuwezesha mafunzo haya, Asanteni sana" amesema Dkt. Lulu Chirande.
Mafunzo hayo ya siku nne yamehitimishwa kwa kuwapatia vyeti washiriki waliotoka Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya ya Ilemela, Sengerema na Nyamagana waliopata mafunzo hayo ya kutambua mapema siko seli, athari na matibabu ya siko seli kuanzia kwenye Kliniki za Mama na Mtoto.
KIMBIA CHANGIA WATOTO WENYE SARATANI.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga leo Septemba 25, 2024 ameendesha kikao na Watumishi wa Hospitali ya Bugando, baada ya kuunda kamati mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha mbio za Bugando Afya Marathoni.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga leo Septemba 25, 2024 ameendesha kikao na Watumishi wa Hospitali ya Bugando, baada ya kuunda kamati mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha mbio za Bugando Afya Marathoni ambapo kauli mbiu inasema, “Kimbia changia watoto wenye saratani” Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Oktoba 20, 2024 huku mgeni rasmi akiwa ni Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko. (MB).
Kwa upande wake Profesa Kidenya kutoka Chuo Kikuu Shirikishi cha Kikatoliki cha Sayansi na Tiba (CUHAS) na Mwakamati ya uhamasishaji wa mbio za marathoni amesema, 'Tumeandaa Marathoni hii ili kuthamini afya yako, kupunguza kasi ya magonjwa yasiyoambukiza na kuwasaidia watoto wenye saratani' ,Hivyo Prof.Kidenya amewasihi Wafanyakazi na Jamii kwa ujumla kuchangia kwaajili ya kuwasaidia watoto hawa kama sadaka.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amesema, lengo la kuanzisha mbio hizo ni kuchangia watoto wenye saratani na kusaidia matibabu ya watoto hao kwani matibabu ya saratani ni gharama japokuwa Serikali ina mchango mkubwa katika kusaidia matibabu haya na pia matibabu yake huchukua muda mrefu.
”Tukumbuke kwamba watoto hawa ni viongozi watarajiwa na kwa kupitia Marathoni watatimiza ndoto zao.” amesema Dkt. Massaga.
Aidha ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa msaada wa ujenzi wa jengo la saratani, vifaa tiba, dawa na matibabu ya wagonjwa wa saratani nakusema, “sisi ni jukumu letu kuunga mkono juhudi za Serikali yetu ili kuhakikisha watoto hawa wanatimiza ndoto zao.”
SEPTEMBA MWEZI WA UHAMASISHAJI DHIDI YA UGONJWA WA SIKOSELI ( SELIMUNDU)
SEPTEMBA MWEZI WA UHAMASISHAJI DHIDI YA UGONJWA WA SIKOSELI ( SELIMUNDU)
SEPTEMBA MWEZI WA UHAMASISHAJI DHIDI YA UGONJWA WA SIKOSELI ( SELIMUNDU)
WADAU MBALIMBALI WAJENGEWA UELEWA WA UGONJWA WA SIKOSELI
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Watoto Kitengo cha Sikoseli leo Septemba 23, 2024 imeendesha mafunzo ya kujengeana uelewa juu ya ugonjwa wa Sikoseli kwa wadau mbalimbali wakiwemo Madaktari, Wauguzi, Watendaji wa Kata kutoka Hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya vilivyopo Mkoa wa Mwanza sambamba na Wazazi/Walezi wa watoto wenye Ugonjwa wa Sikoseli pamoja na Mashujaa wa Sikoseli.
Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo haya, Mkurugenzi wa huduma za Afya Saidizi Dkt. Cosmas Mburwa kwa niaba ya Taasisi amewashukuru na kuwapongeza waratibu wa mafunzo haya
" Napenda kuwashukuru, kuwapongeza na kutambua uwepo wenu na juhudi zenu waratibu wa mafunzo haya, washiriki ninyi mna mchango mkubwa wa kupelekka elimu hii kwa jamii huko mtaani ili kuweza kupunguza madhira ambayo wagonjwa wenye sikoseli na wazazi wanakumbana nayo kiuchumi na kijamii ikiwemo kutengwa" Dkt. Mburwa.
Kwa upande wake Mratibu wa Sikoseli Hospitali ya Bugando Dkt. Emmanuela Ambrose amefafanua kuwa, lengo la mafunzo haya ni kujengeana uelewa kuhusu ugonjwa wa Sikoseli, jinsi ya kumgundua Mgonjwa na kumuhudumia kabla ugonjwa haujafikia hatua mbaya na kumpatia rufaa kwa wakati sambamba na kutoa elimu kwa wazazi na walezi namna ya kuwalea wagonjwa wa Sikoseli.
Aidha, Ndg. Gabriel Makoye Mtego ambaye ni kijana shujaa wa ugonjwa wa Sikoseli ametoa wito kwa Selikali kuwezesha upatikanaji wa dawa za Sikoseli kwa gharama nafuu au bure kama ilivyo kwa waathirika wa HIV ili kukabiliana na changamoto ya wagonjwa wengi kushindwa kumudu gharama za dawa na matibabu ya Sikoseli.
Mafunzo haya ya kujengeana uelewa wa ugonjwa wa Sikoseli kwa wadau yanafanyika kwa siku nne katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 26 Septemba, 2024.
WAWEZESHAJI NA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA HUDUMA TABIBU ZA KIFAMASIA (CPS)WAPONGEZWA
WAWEZESHAJI NA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA HUDUMA TABIBU ZA KIFAMASIA (CPS)WAPONGEZWA
WAWEZESHAJI NA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA HUDUMA TABIBU ZA KIFAMASIA (CPS)WAPONGEZWA
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewapongeza waandaaji, wawezeshaji na washiriki wa mafunzo ya Huduma Tabibu za Kifamasia (Clinical Phamacy Services) wanaotoka Kanda mbalimbali nchini ambapo mafunzo hayo yanaendela katika Hospitali ya Bugando tangu tarehe 17 Septemba, 2024.
Dkt. Massaga amesema "Nikushukuru na kukupongeza Profesa Omary Mashiku na timu yako kwa kuja na huu ubunifu, Sisi Madaktari ni kiungo muhimu katika kumhudumia Mgonjwa anapokuwa wodini, lakini hiki kinachotengezwa hapa Mfamasia naye atakuwa kwenye timu wakati wa kumwangalia Mgonjwa, hili ni wazo jema la kuwa pamoja kumwona Mgonjwa na naomba tulipokee kwa mtazamo chanya zaidi"
Kwa upande wa Professa Omary Mashiku Minzi, ambaye ni Mwanzilishi wa CPS na mkufunzi kwenye mafunzo haya, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kutoa nafasi ya mafunzo na kusema lengo ni kuleta mashirikiano mazuri wodini kwa Mfamasia kuwa pamoja na Madaktari na Wauguzi wodini ili kuboresha tiba kwa Mgonjwa, kuwa na mawasiliano mazuri na utaratibu bora wa kuhifadhi taarifa kwenye mfumo.
Naye mratibu wa mafunzo hayo Bertha Mallya ameishukuru Hospitali ya Bugando kwa mapokezi mazuri yenye Huruma na Upendo ya kutoa mafunzo hayo kwa Wafamasia 30 kutoka Mwanza, Kigoma, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mara na Kilimanjaro ambayo yanaendelea kutolewa hadi terehe 27 Septamba, 2024.
HOSPITALI YA BUGANDO YAWATUNUKIA TUZO WAUGUZI BORA KWENYE SMARTNESS AWARDS 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga ameongoza hafla ya utoaji wa tuzo kwa wauguzi waliofanya vizuri zaidi kwenye utendaji wao wa kazi kwa kuwakabidhi zawadi mbalimbali ikiwa ni motisha katika utoaji wa huduma.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga ameongoza hafla ya utoaji wa tuzo kwa wauguzi waliofanya vizuri zaidi kwenye utendaji wao wa kazi kwa kuwakabidhi zawadi mbalimbali ikiwa ni motisha katika utoaji wa huduma.
Katika tuzo hizi za Smartness awards 2024, Wauguzi wa wodi ya Medical ICU wameibuka kidedea Kwa kuwa washindi wa kwanza, wakifuatiwa na wodi ya J2 VIP na wodi ya watoto huku Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi Sr. Salome Marandu akitunukiwa tuzo ya jumla ya Muuguzi bora wa mwaka 2024 (Smart Nurse).
Akizungumza wakati wa kuwatangaza washindi na kuwatunukia zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt Fabian A. Massaga ameipongeza Kurugenzi ya huduma za Uuguzi Kwa ubunifu wa kutoa tuzo hizo ambazo ni motisha mkubwa katika kuimarisha huduma za matibabu.
"Leo ni siku maalumu kwa kweli, tukio hili ni kubwa sana kwa hospitali yetu, niwapongeze sana na jambo hili linafaa kuigwa kwa wengine, na tuzo hizi zitaongeza chachu na utendaji bora zaidi.
Hawa waliopewa zawadi wameonyesha njia kuwa tunaweza kubadilika na nafarijika kuona haya kuwa tunaweza kwenda kurekebisha yale mapungufu machache ambayo hatufanyi vizuri, suala la customer care kwa Mgonjwa tulizingatie sana na tuendelee kutoa huduma zetu kwa huruma na upendo" Dkt Fabian A. Massaga.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr. Salome Marandu amesema tuzo hizo zimelenga kuboresha huduma za matibabu kwa Mgonjwa kwa kuzingatia uingizaji wa taarifa za matibabu kwenye mfumo, huduma bora za Uuguzi na usafi wa mazingira ambapo washindi wametunukiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vyeti, pesa taslimu, T-shirts na ngao.
MKUU WA MKOA WA MWANZA AUNGANA NA WADAU KUCHANGIA MATIBABU YA SARATANI ZA WATOTO.
MWANZA
MKUU WA MKOA WA MWANZA AUNGANA NA WADAU KUCHANGIA MATIBABU YA SARATANI ZA WATOTO.
Mhe. Said Mtanda Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Mwanza kuungana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando katika kuchangia matibabu ya
watoto wenye saratani kupitia Bugando Health Marathon ambao wanakabiliwa na ukosefu wa fedha za matibabu.
Mhe. Mtanda amewaongoza wadau hao kwa kuchangia shilingi milioni tano na kuwaasa kuchangia matibabu ya saratani za watoto.
Mhe. Mtanda amesema “Hospitali ya Bugando imeamua kuisaidia juhudi za serikali kwa kuwa serikali haiwezi kufanya kila kitu hivyo ushiriki wa wadau katika kuchangia matibabu ya watoto hawa itasaidia kupunguza mzigo kwa serikali.
Matibabu ya Saratani ni gharama kubwa hivyo nimewaiteni ili mtusaidie na kutuunga mkono kuokoa maisha ya watoto hawa kwa kuchangia Bugando Health Marathon 2024.” Amesema Mhe. Mtanda
Naye Dkt. Fabian A. Massaga Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando amesema, “ Tumelenga kukusanya kiasi cha shilingi Billioni moja yenye lengo la kusaidia takribani watoto mia tano wanaougua saratani katika Hopitali ya Bugando , hivyo tuungane kwa pamoja kusaidia watoto hawa. “ Amesema Dkt. Massaga
Bugando Health Marathon itafanyika tarehe 20/10/2024 na Mgeni Rasmi wa mbio hizi anatarajia kuwa Mhe. Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Mnakaribishwa kuendelea kujisajili kupitia Tigo Lipa:22314082 ,
CRDB: 01J1053036501- BMC Cost Sharing & USSD Tigo; *150*01#
MAFUNZO YA WAFAMASIA YA HUDUMA SAIDIZI KWA MGONJWA YAFUNGULIWA BUGANDO
Mafunzo ya Huduma tabibu za kifamasia (Clinical Phamacy Services) yanaendeshwa kwa siku 10 kwa washiriki 30 kutoka Mikoa ya Kilimanjaro, Tabora, Simiyu, Kigoma, Shinyanga, Mwanza na Mara kushiriki.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Sr. Dkt. Alicia Massenga akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bugando, amefungua rasmi mafunzo ya Huduma tabibu za kifamasia (Clinical Phamacy Services) yanayotolewa kwa Wafamasia kutoka kanda mbalimbali nchini kuanzia leo terehe 17 mpaka tarehe 27 Septemba 2024 katika Hospitali ya Bugando ambapo mafunzo hayo
yanaendeshwa na Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi MUHAS kwa udhamini wa shirika la Christian Social Services Commission(CSSC) yakiwa na jumla ya Wafamasia 30 kutoka Hospitali mbalimbali nchini.
Sr.Dkt Massenga amewapongeza waandaaji na washiriki na kuwataka kutumia vizuri mafunzo hayo kwani yana tija kubwa katika kumhudumia Mgonjwa.
"Niwapongeza CSSC kwa mafunzo haya yenye matunda makubwa ambayo kwa kweli tumekuwa tukiyaona katika kuboresha sekta ya Afya, washiriki tutumie muda mwingi kwenye mafunzo haya, mzingatie yote mtakayopata hapa na mkayatumie huko muendako kumhudumia Mgonjwa na kuwafundisha wengine kwa kufanya kazi Kwa umoja, mkifanya hivyo itaongeza ufanisi kwani itasaidia Mgonjwa kutumia dawa kwa wakati na itapunguza gharama za matibabu, mkatumie ujuzi huu vyema" ameyasema hayo Sr. Dkt Alicia Massenga.
Kwa upande wake Dkt. Andrew Charles ambaye ni meneja wa CSSC Kanda ya Ziwa amesema mafunzo hayo ni muhimu kwani wafamasia watashirikiana na Madaktari moja kwa moja katika kumhudimia Mgonjwa.
Mafunzo ya Huduma tabibu za kifamasia
(Clinical Phamacy Services) yanaendeshwa kwa siku 10 kwa washiriki 30 kutoka Mikoa ya Kilimanjaro, Tabora, Simiyu, Kigoma, Shinyanga, Mwanza na Mara kushiriki.
BUGANDO YATOA MAFUNZO YA KUHUDUMIA VIDONDA KWA WAUGUZI NCHINI
Mafunzo hayo ya siku Tano yamehudhuriwa na Wauguzi kutoka Mikoa ya Njombe, Kilimanjaro, Tabora, Geita na Mwanza.
Mkurugenzi wa huduma za Upasuaji Sr. Dkt. Alicia Massenga akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, amefunga mafunzo ya kuhudumia vidonda (wound management) kwa wauguzi Saba kutoka Mikoa mbalimbali nchini yaliyolenga kuboresha na kuwapa ujuzi mpya wa namna ya kuhudumia vidonda kwa Wagonjwa hii leo Septemba 13, 2024.
Katika kufunga mafunzo hayo, Sr. Dkt Massenga ameipongeza Kurugenzi ya huduma za Uuguzi kwa kuandaa mafunzo hayo na Wauguzi hao kushiriki mafunzo hayo muhimu;
"hongereni sana kwa kuwa wabunifu wa kutoa ujuzi huu muhimu hadi kwa wauguzi wengine kutoka pande mbalimbali nchini, mlichukue hili kwa uzito wake na mkawe wakarimu kwa kutoa elimu hii kwa wengine na mtakuwa mmefanya kitu kizuri kusaidia watu, tunajua wote kuwa huduma ya vidonda inataka moyo na sisi tuendelee na moyo huo huo kwa kufanya kwa mapendo na tuwe faraja kwa Wagonjwa wenye vidonda" Amesema Sr. Dkt. Massenga.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr. Salome Marandu amewapongeza washiriki kwa kushiriki vyema mafunzo hayo na kuonesha mabadiliko makubwa kwenye mitihani waliyofanya vizuri, na kuwataka kwenda kutoa ujuzi huo kwa wengine huko waendako.
Aidha, mmoja ya washiriki wa mafunzo hayo Muuguzi Dennis Fikiri kutoka Geita ameishukuru Hospitali ya Bugando kuwapa mafunzo hayo na kusema kuna vitu vipya wamevipata, namna ya kuhudumia vidonda na kuongeza ujuzi zaidi na wataenda kuwa mabalozi wa hicho walichojifunza.
Mafunzo hayo ya siku Tano yamehudhuriwa na Wauguzi kutoka Mikoa ya Njombe, Kilimanjaro, Tabora, Geita na Mwanza.
MWEZI WA UELEWA WA SIKO SELI (SICKLE CELL) - SEPTEMBA
WATAALAMU WA AFYA WILAYA YA SENGEREMA WAPATIWA MAFUNZO YA SIKOSELI.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu ugonjwa wa sikoseli kwa wataalamu wa afya Halmashauri ya wilaya ya sengerema, mafunzo haya yametolewa na Madaktari Bingwa wa Sikoseli na magonjwa ya damu sambamba na Mtaalamu wa Maabara Kitengo cha Damu ambao ni Dkt. Emmanuela Ambrose, Dkt. Tekla Mtobesya na Ndg. Mwesige Charles.
Mafunzo haya yamehusisha wataalamu wa Afya sitini na tatu (63) wakiwemo Madaktari, Wauguzi, Wahudumu wa Afya na wataalamu wengine yamefanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 11-13 Septemba 2024 Wilayani Sengerema kufuatia maombi ya Halmashauri ya Sengerema kuhitaji wataalamu wake kupewa mafunzo na kuanzisha clinic za Sikoseli ikiwa ni huduma ya uchunguzi wa awali kwa wagonjwa wa sikoseli kabla ya kupewa Rufaa.
Kupitia mafunzo haya, washiriki wameweza kufundishwa jinsi ya kugundua ugonjwa kitaalamu, namna ya kumuhudumia mgonjwa na kutoa rufaa mapema inapohitajika.
Septemba ni Mwezi wa uhamasishaji wa Ugonjwa wa Sikoseli ambao unalenga kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huu na changamoto wanazokabiliana nazo watu wanaoishi na hali hii duniani kote.
BUGANDO YATOA ZAWADI KWA WASHINDI MISS LAKE ZONE 2024.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Kliniki yake ya Bugando Specialized Polyclinic iliyopo NERA imeshiriki Tamasha la Miss Lake Zone 2024 kwa kutoa zawadi ya matibabu bure kwa muda wa mwaka mmoja kwa washindi watatu wa shindano hilo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Kliniki yake ya Bugando Specialized Polyclinic iliyopo NERA imeshiriki Tamasha la Miss Lake Zone 2024 kwa kutoa zawadi ya matibabu bure kwa muda wa mwaka mmoja kwa washindi watatu wa shindano hilo ambalo Bugando ilikuwa mdhamini.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dkt Cosmas Mbulwa ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Afya Saidizi amewapongeza waandaaji, washindi na washiriki wote na kuwahakikishia Hospitali ya Bugando ipo bega kwa bega kwa kujali Afya zao.
"niwapongeza washiriki wote wa shindano hili na zaidi kwa washindi, waandaaji na wote tuliopo hapa, Sisi kama Bugando tunathamini Urembo kwa kujali Afya zenu na ndio sababu tumeungana nanyi hapa, na kupitia hilo washindi watatu wa shindano hili tutawazadia huduma ya matibabu bure kwa muda wa mwaka mmoja kwenye Kliniki yetu ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi iliyopo Nera, Bugando tupo kuhudumia Afya, niwapongeze sana washindi na mkawe mabalozi wazuri" Dkt Cosmas Mbulwa.
Tamasha la fainali ya Miss Lake Zone 2024 limehitimishwa kwa Mlimbende Agnes Simkanga, Mwanafunzi wa Chuo cha CUHAS Bugando Mwanza kushinda taji la Miss Lake Zone 2024 na atawakilisha Kanda ya Ziwa kwenye shindano la kumpata Miss Tanzania
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Agosti 30,2024 imepokea wageni kutoka Kampuni ya Japan (Asahi intecc)
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Agosti 30,2024 imepokea wageni kutoka Kampuni ya Japan (Asahi intecc)
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Agosti 30,2024 imepokea wageni kutoka Kampuni ya Japan (Asahi intecc) lengo likiwa kuangazia uwezekano wa mashirikiano baina ya Kampuni ya Japan
( Asahi Intecc) na Hospitali ya Bugando katika matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa kutumia mtambo wa Cathlab.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Tiba ameshukuru Kampuni ya Asahi Intecc kwa kutembelea Hospitali ya Bugando kwa lengo la mashirikiano ya matibabu ya moyo kwa kuwa imekuwa ni dhamira na imani ya Hospitali ya Bugando kukuza mashirikiano hayo
"Asahi intecc ina nia ya kushirikiana na watoa huduma wa ndani na nje katika nyanja ya upasuaji wa moyo na tumetambua Bugando ni moja ya Hospitali yenye nia ya uwekezaji wa matibabu ya moyo" ameyasema hayo Akira Iwai ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Japan (Asahi Intecc).
BUGANDO YAZINDUA JEZI KUELEKEA BUGANDO AFYA MARATHONI 31 AGOSTI, 2024.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imezindua Jezi zitakazotumika siku ya Bugando Afya Marathoni inayotarajiwa kufanyika Agosti 31, 2024.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imezindua Jezi zitakazotumika siku ya Bugando Afya Marathoni inayotarajiwa kufanyika Agosti 31, 2024.
Uzinduzi huu umefanyika mapema leo Agosti 17, 2024 katika Viwanja vilivyopo mbele ya Hospitali ya Bugando na kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga akiambatana na viongozi, watumishi, wanajumuiya ya Bugando na wadau mbalimbali.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa jezi, Dkt. Massaga amewahamasisha na kuwakaribisha wadau wote wakiwemo Wananchi wa Mkoa wa Mwanza na viunga vyake kuchangia watoto wanaoteseka na saratani
"Kimbia, Changia Watoto wenye Saratani, hii ndio kauli mbiu yetu. Naomba tutumie nafasi hii kuwahamasisha wananchi wote kuchangia watoto wanaoteseka na Saratani na hili si la kwetu pekee tunaungana na Serikali. Tukio letu litafanyika tarehe 31 Agosti, 2024 na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dotto Biteko (MB), naomba wananchi tuje tuungane pamoja. leo tupo hapa kuzitambulisha jezi zetu zitakazotumika siku hiyo" amesisitiza Dkt. Massaga
Sisi sote ni Wagonjwa watarajiwa, ni jambo letu sote na sisi kama watumishi wa Afya tunawiwa kuhamasisha jamii kuchangia na kuboresha Afya ya Watanzania na jamii kwa ujumla wake, ametanabaisha Dkt. Massaga.
Bugando Afya Marathoni imelenga kuwachangia Watoto wenye saratani,
ambapo hafla hii ya uzinduzi imehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Taasisi za Kibenki, Jogging Club, Umoja wa wakimbiaji, Vyombo vya habari, Makampuni ya huduma za simu, Watumishi na wanajumuiya ya Bugando na zimetanguliwa na uzinduzi wa kits na Route check za Bugando Marathon kwa wananchi kukimbia umbali wa Kilomita 5, Kilomita 10 na kilomita 21.
HOSPITALI YA BUGANDO YAUNGANA NA WATANZANIA KATIKA SIKU YA PAMBA (PAMBA DAY) 2024.
Uongozi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando wameungana na Watanzania katika tamasha la siku ya Pamba 2024 ambapo Timu ya Pamba Jiji Footbal Club imeadhimisha tamasha lake kwa kutambulisha wachezaji wapya.
Uongozi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando wameungana na Watanzania katika tamasha la siku ya Pamba 2024 ambapo Timu ya Pamba Jiji Footbal Club imeadhimisha tamasha lake kwa kutambulisha wachezaji wapya na kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Vital'O ya Burundi huku mgeni rasmi akiwa Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax Waziri wa ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiambatana na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma.
Akizungumza katika tamasha hilo Waziri Stegomena Tax amesema
"Mheshimiwa Rais anafanya kazi kubwa na katika mafanikio haya ya mkoa wa mwanza ni maono ya Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan hivyo wanamwanza niwapongeze sana Kwa maendeleo haya ya mpira ambao unadumisha amani na umoja, hili linatuunganisha sote, tunajua tunaandaaa mashindano makubwa 2027 na mkoa huu ni Sehemu ya kutimiza hayo, hongereni sana na niwatakie Kila la kheri Pamba yetu irudi kama ilivyokuwa zamani".
Aidha, Naibu waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa. Hamis Mwinjuma nae amesema "Moja kati ya mambo yanayonifurahisha ni kuona timu ya Pamba Jiji Footbal Club inarudi katika nafasi ya Premiere League na ninaamini kwamba timu hii itaendelea kufanya vizuri zaidi na kuandikwa katika historia za league na kuwaomba viongozi wa timu kufanya kila linalowezekana ili kila atakaejisajili katika timu hii asitamani kutoka au kuhamia kwenye timu nyingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Said Mtanda amemshukuru Waziri wa Ulinzi pamoja na Naibu Waziri wa Michezo kwa kuitikia wito na kushiriki pamoja nao katika tamasha hili na kuahidi kwamba timu ya Pamba itaendelea kufanya vizuri zaidi.
TUZO YA UFANISI KATIKA PROGRAM YA USIMAMIZI WA MATUMIZI BORA YA DAWA.
BUGANDO YASHINDA TUZO YA UFANISI KATIKA PROGRAM YA USIMAMIZI WA MATUMIZI BORA YA DAWA.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga amepokea tuzo maalumu kutoka Wizara ya Afya na USAID kwa kutambua ufanisi wa Hospitali ya Bugando katika program ya usimamizi wa matumizi bora ya dawa (Antimicrobial Stewardship Program) leo terehe 27 Agosti, 2024.
Tuzo hiyo Dkt Massaga amekabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa matumizi bora ya dawa wa Hospitali ya Bugando Prof. Jeremiah Seni na wajumbe wa kamati hiyo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea gari
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea gari
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea gari lililogharimu kiasi cha shillingi Milioni mia mbili na kumi (210,000,000) kutoka katika mradi wa pili wa shirika la CBM shirika linalojihusisha na kuboresha huduma za Afya ya macho lengo likiwa ni kuwezesha na kurahisisha shughuli za mradi kwa kufika maeneo mbalimbali na kusaidia shughuli za Hospitali kwa ujumla.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amempongeza Mkuu wa Idara ya Macho Dkt. Christopher Mwanansao na timu nzima inayofanya kazi moja kwa moja na mradi huo na kuwaomba kutunza gari hilo na kusisitiza gari hilo likafanye kazi iliyokusudiwa ili hata wafadhili waweze kuona matunda ya mradi huo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imetembelewa na Washiriki wa shindano la Miss Lake Zone 2024
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imetembelewa na Washiriki wa shindano la Miss Lake Zone 2024
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imetembelewa na Washiriki wa shindano la Miss Lake Zone 2024 leo Agosti 23,2024 kwa lengo la kuwatembelea watoto wenye saratani na kupata nafasi ya kupima Afya na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi katika Kliniki ya Bugando Specialized Polyclinic ambayo inadhamini shindano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewapongeza walimbwende hao kwa kuwa kioo cha jamii na kusema "Eneo hili la ulimbwende lina mchango na ushawishi mkubwa, hivyo mkawe mabalozi wazuri kwa kuelimisha wananchi juu ya ugonjwa wa saratani na umuhimu wa kufanya uchunguzi wa Afya mara kwa mara".
Pia Dr.Massaga amewaahidi walimbwende hao kuendelea kuwaunga mkono wakati wowote na kuahidi washindi watatu watakaoshinda katika shindano la Miss lake zone 2024 watapata matibabu ya kumuona Daktari bure kwa muda wa mwaka mzima katika kliniki ya kibingwa na Bingwa bobezi ya (Bugando Specialized polyclinic-Nera).
Aidha, Mwenyekiti na Mlezi wa
Walimbwende hao Bi. Rosemary Selemani ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kuunga mkono shindano hilo la Kanda ya Ziwa 2024 na kusema Bugando ina mchango mkubwa katika shindano la urembo kwa kuweka vema afya zao.Pia ameushukuru uongozi kwa kupima Afya zao na kutoa ushauri wa kitaalamu kutoka kwa Madaktari Bingwa na Bingwa bobezi katika tawi la Bugando Specialized polyclinic-Nera.
SHIRIKA LA KIHARUSI DUNIANI LATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
SHIRIKA LA KIHARUSI DUNIANI LATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
SHIRIKA LA KIHARUSI DUNIANI LATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
Prof. Sheila Martins, Rais wa Shirika la Kiharusi Duniani(WSO) na Pia Daktari Bingwa Bobezi wa mishipa ya Fahamu na Ubongo kutoka Brazil ametembelea hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando leo Agosti 21,2024 kwa lengo la Kujadili kuhusu mikakati na juhudi za kudhibiti kiharusi.
Katika Ziara hiyo Prof. Sheila kupitia Shirika la kiharusi duniani,ameahidi kutoa msaada Mwingine wa vifaa Tiba kwaajili ya kuwasaidia wagonjwa Wenye kiharusi."Uangalizi mzuri wa wagonjwa wa kiharusi unaweza kuleta mabadiliko chanya katika kudhibiti kiharusi, alisema Prof. Sheila.
Sambamba na hayo Dkt. Fabian A. Massaga,Mkurugenzi wa hospitali ya Bugando, amewapongeza na kuwashukuru Shirika la kiharusi duniani,kupitia Wizara ya Afya, kwa mafunzo maalumu na ufadhili wa vifaa Tiba utakaopunguza Idadi ya vifo na kuleta Mabadiliko kwa wagonjwa wa kiharusi.
Dkt. Sarah Matuja, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya mishipa ya Fahamu na mkufunzi katika Chuo Kikuu Cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya Shirikishi ( CUHAS) akiwa ameongozana na Rais wa Shirika la kiharusi Duniani amesema,"Takwimu za kiharusi Duniani Kote zinachukua nafasi ya pili kwa magonjwa yanayosababisha vifo na ulemavu. Ambapo Afrika kiharusi kinachukua nafasi ya kumi. Nakwa Tanzania kiharusi kinawaathiri Vijana Wenye umri kuanzia miaka 18 - 45,na watu Wazima Wenye umri zaidi ya miaka sitini"
Akiongeza kuwa asilimia 50% ya wagonjwa wa kiharusi wanachelewa kufika hospitali kupata Matibabu na kupelekea asilimia 30% Hadi 60% ya vifo ndani ya siku 30 baada ya kupata kiharusi.
KAMBI YA MATIBABU YA MAGONJWA YA MIFUPA NA MAGONJWA YA MFUMO WA MKOJO YAANZA RASMI.
KAMBI YA MATIBABU YA MAGONJWA YA MIFUPA NA MAGONJWA YA MFUMO WA MKOJO YAANZA RASMI.
KAMBI YA MATIBABU YA MAGONJWA YA MIFUPA NA MAGONJWA YA MFUMO WA MKOJO YAANZA RASMI.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa kupitia kliniki yake ya madaktari bingwa na bingwa bobezi iliyopo mtaa nera jijini Mwanza imeanza rasmi kambi ya matibabu ya magonjwa ya mfumo wa mkojo na magonjwa ya mifupa, kwa kushirikiana na taasisi ya Tanlink Medical Tourism Agency na Hoospitali ya Medcover iliyopo nchini India.
Kambi hii imefunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A Massaga kwa kuwaribisha wananchi walioweza kufika na kupata huduma hizi.
Akizungumza katika kambi hiyo Dkt. Massaga amesema " Bugando kama taasisi ya afya tunawajibu wa kuimarisha tiba utalii ( Medical tourism ) kama azma ya serikali, na kinachofanyika hapa ni kusimamia na kutekeleza azma hiyo, kama tunavyoona tumeshirikiana na madaktari kutoka nchini India ili kusogeza huduma hizi za kibingwa kwa wananchi wetu wa kanda ya ziwa, nipende kuwakaribisha na niwaombe kutumia fursa hii kupata matibabu ambayo mara nyingine ingewalazimu kusafiri kwa gharama kubwa kwenda India kupata matibabu, madaktari hawa watashirikiana na madaktari wetu wazawa hivyo niwahakikishe huduma mtakayopata ni bora na stahiki”.Amesema Dkt. Massaga
Kwa upande wake Dkt. Hassan Fyumagwa ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Tanlink ameushukuru na kuupongeza uongozi kwa kwa kukubali kushirikiana katika kutoa huduma hizi za kibingwa baina ya Bugando na madaktari kutoka nchi mbali mbali, pia ameahidi kuendeleza mashirikiano haya kwa kuandaa kambi nyingine hapo badae.
Tunaendelea kuwakaribisha wananchi kupata huduma hizi za kibingwa na kibingwa bobezi kwa kufika Kliniki ya madaktari bingwa Bugando iliyopo nera ambapo kambi hii itafanyika kuanzia 15-18/8/2024.
BUGANDO KUANZISHA MASHIRIKIANO YA KIMATAIFA NA CHUO KIKUU KATOLIKI CHA VILLANOVA, MAREKANI.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inatarajia kuanzisha Mashirikiano ya Kimataifa na Chuo Kikuu Katoriki cha Villanova kilichopo Philadelphianchini Marekani.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inatarajia kuanzisha Mashirikiano ya Kimataifa na Chuo Kikuu Katoliki cha Villanova kilichopo Philadelphianchini Marekani.
Haya yamebainishwa wakati wa kikao kilichowakutanisha wageni watatu kutoka Chuo Kikuu cha Villanova wakiongozwa na Ndg. Daniel Graffin na Uongozi wa Hospitali ya Bugando ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dkt. Fabian A. Massaga.
Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kujadili maeneo ambayo yatakwenda kujumuishwa katika mashirikiano hayo ambayo ni pamoja na kubadilishana uzoefu na ujuzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo uhandisi, Mfumo wa maji na mfumo wa taka ngumu na taka maji ambapo wataalamu hawa wametanabaisha kuwa wamevutiwa na Hospitali ya Bugando na kuona ni sehemu sahihi kuitumia kutekeleza miradi yao.
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Massaga ameshukuru kwa nia hii ya dhati iliyooneshwa na Wajumbe kutoka Villanova na kuahidi kuwapa ushirikiano mkubwa.
" Hospitali ya Bugando ni Kongwe tangu kuanzishwa kwake takribani zaidi ya miaka 53 mifumo ya maji na taka haipo katika ubora wake wa awali hivyo mashirikiano haya yatakwenda kuisaidia Hospitali kuboresha miundo mbinu huku ikizingatiwa kuwa Bugando kama Taasisi inashughulikia afya za wananchi, suala la uwepo wa maji safi na mifumo imara na ya kisasa ya maji safi, taka ngumu na taka maji ni kipaumbele kwa Taasisi yetu, tupo tayari kuwapokea na kushirikiana nanyi" amesema hayo Dkt. Massaga
Ndg. Hillary Sued, Msimamizi wa mradi huu na mtaalamu wa saratani Hospitali ya Bugando kwa upande wake ameelezea umuhimu wa mashirikiano haya kuwa mashirikiano haya yatakwenda kuinufaisha Hospitali ya Bugando kwani itatoa fursa kwa wataalamu wa Bugando kujifunza kwa vitendo Teknolojia mpya na za kisasa pamoja na kuboresha miundo mbinu na mifumo ya Maji safi, taka ngumu na taka maji kwa ustawi wa afya ya jamii yetu.
MWENYEKITI WA BODI YA HOSPITALI YA BUGANDO MHASHAMU BABA ASKOFU RENATUS NKWANDE, AWAPONGEZA WATUMISHI KWA KAZI NZURI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Mhashamu Baba Askofu Renutus Nkwande amewapongeza Watumishi kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwahudumia wagonjwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Mhashamu Baba Askofu Renutus Nkwande amewapongeza Watumishi kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwahudumia wagonjwa,
“Nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa kazi nzuri mnazofanya hapa Bugando mara nyingi tunapata pongezi kutoka kwa watu mbalimbali na hii ni kutokana na kazi mnazofanya nami nawapongeza, kwa niaba ya Bodi na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ambao ndio wamiliki nawapongeza na nitambua kazi kubwa mnazozifanya “ amesema Askofu Renatus Nkwande.
Pongezi hizi zimetolewa na Mhashamu Baba Askofu Nkwande wakati wa kikao kati ya Wajumbe wa Bodi ya Hospitali na Watumishi wa Bugando kilichofanyika katika ukumbi wa CUHAS Bugando lengo likiwa ni kukutana na kujadili mambo mbalimbali ya kuboresha huduma za Hospitali ya Bugando.
Askofu Renatus Nkwande amepata fursa ya kusikiliza maoni na ushauri kutoka kwa Watumishi na kuweza kuyatolea ufafanuzi huku akitanabaisha kuwa baada yakukaa na Uongozi kabla ya kikao hicho Bodi imeweza kuona changamoto zinazoikabili hospitali na kusisitiza kuwa changamoto hizo zitafanyiwa kazi kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali, pia amewakumbusha Watumishi kuhakikisha wanasimamia tunu za Hospitali ya Bugando kwa kujiepusha na vitendo ambavyo si vizuri ikiwemo rushwa na ubadhilifu.
Aidha Makamu Mwenyekiti wa Bodi Mhashamu Baba Askofu Beatus Kinyaiya, ameitaka Jumuiya ya Bugando kufanya kazi kwa manufaa ya Hospitali ya Bugando na kuwa tayari kuitetea kwa nguvu zote.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewashukuru Wajumbe wa Bodi kwa ujio wao sambamba na Watumishi kwa kushiriki kikao hicho chenye lengo la kuboresha huduma za afya na kuahidi kufanyia kazi changamoto mbalimbali za watumishi.
BODI YA HOSPITALI YA BUGANDO YAPEWA SEMINA YA UONGOZI NA UTENDAJI BORA WA KAZI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bugando Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande, Wajumbe wa Bodi na menejimenti ya Hospitali wamepewa semina ya uongozi na utendaji bora.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bugando Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande, Wajumbe wa Bodi na menejimenti ya Hospitali wamepewa semina ya uongozi na utendaji bora katika kikao cha kuwatambulisha na kuwakaribisha Wajumbe wapya wa Bodi leo terehe 30 Julai, 2024.
Katika semina hiyo iliyoendeshwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Inter Capital Limited Bw. Antony Chamungwami, Askofu Mkuu Renatus Nkwande amemshukuru na kumpongeza Bw.Antony kwa somo zuri aliloliwasilisha katika semina hiyo lililolenga kuboresha huduma za Afya na Ustawi wa Taasisi ya Bugando.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amesema semina hiyo italeta maendeleo makubwa katika utendaji na uendeshaji wa Taasisi kwani imegusa nyanja muhimu za uongozi na utendaji bora wa kazi.
WAKURUGENZI, WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA BUGANDO WAPEWA SEMINA YA UTENDAJI KAZI.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando umetoa hati ya viapo kwa wakurugenzi,wakuu wa idara na vitengo.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando umetoa hati ya viapo kwa wakurugenzi,wakuu wa idara na vitengo ikiwa ni ahadi ya uadilifu na kusimamia miongozo ya Taasisi, wizara na Kanisa kiujumla leo tarehe 29 Julai, 2024.
Hata hivyo, kiapo hicho kimefuatiwa na semina kwa viongozi iliyoendeshwa na Mkurugenzi mtendaji wa Inter Capital Limited Bw. Antony Chamungwami lengo likiwa ni kukumbushana kanuni za uongozi,uadilifu na utendaji bora wa kazi unaozingatia kanuni na taratibu za kiutumishi pamoja na kulinda mashirikiano kati ya Taasisi, Mashirika na wazabuni mbalimbali pamoja na mengine mengi yanayohusu Uongozi.
Bw.Antony amesema "Kiongozi ni mtu ambaye ana uwezo wa kutekeleza maono na malengo ya Taasisi na kusimamia utekelezaji wa kauli mbiu ya Huruma na Upendo na pia viongozi wanatakiwa kuwa msaada mkubwa kwa Mkurugenzi mkuu kuhakikisha lengo kuu la Hospitali linafikiwa".
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt Fabian A. Massaga amemshukuru na kumpongeza mwezeshaji wa semina kwa somo zuri linaloenda kuleta mabadiliko chanya katika utendaji kazi wa viongozi na kusema,
"Nikushukuru sana Mwezeshaji wetu Bw. Antony kwa semina hii uliyotupatia, mimi na viongozi wenzangu tumejifunza, na tupo tayari kufanyia kazi yale yote uliyotufundisha ndiyo maana tumeahidi kwamba katika nafasi zetu tutatenda haki, tutashirikiana vizuri katika kutoa huduma kwa wagonjwa na kutokiuka misingi ya utumishi"
Mwisho kabisa Dkt.Massaga amewasihi Viongozi kuendelea kutengeneza mazingira rafiki ya kazi kwa kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake kikamilifu na kupata haki yake.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI Wametembelea Hospitali ya Bugando
Leo Machi 08.2024 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI Wametembelea Hospitali ya Bugando
Leo Machi 08.2024 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslau Nyongo (MB), na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (MB) wametembelea Hospitali ya Bugando lengo likiwa ni kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwekeza nguvu kubwa katika utoaji huduma za afya hususani matibabu ya magonjwa ya saratani kwa Hospitali ya Bugando ambayo ni mkombozi kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.
Washiriki kutoka klabu mbalimbali walioshiriki hafla hiyo ikiwemo Wasafi Jogging, EFM, Geita jogging, RADA na Isamilo wameipongeza Bugando fitness
Aidha washiriki kutoka klabu mbalimbali walioshiriki hafla hiyo ikiwemo Wasafi Jogging, EFM, Geita jogging, RADA na Isamilo wameipongeza Bugando fitness
Aidha washiriki kutoka klabu mbalimbali walioshiriki hafla hiyo ikiwemo Wasafi Jogging, EFM, Geita jogging, RADA na Isamilo wameipongeza Bugando fitness kwa kutimiza mwaka mmoja na kuahidi kushiriki kikamilifu na kuwa mabalozi wa mbio za hisani za Bugando Health Marathon 2024.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewapongeza washiriki wote pamoja na jogging
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewapongeza washiriki wote pamoja na jogging
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewapongeza washiriki wote pamoja na jogging klabu mbalimbali kwa kushiriki hafla hiyo na kuwashukuru kwa kuungana na Bugando katika mazoezi.
"Klabu ya Bugando Fitness ilianzishwa kwa lengo la kupamba na magonjwa yasioambukiza na sisi kama wataalamu tumeona changamoto ya magonjwa yasioambukiza ni kubwa hivyo tukaona tuwe mfano kwa kuanzisha mazoezi ambayo yamekuwa na muitikio mkubwa kwa jamii, Sisi kama Bugando na wataalamu wa Afya tunalo jukumu la kuelimisha jamii juu ya magonjwa yasiyoambukiza ambapo saratani ni kati ya magonjwa yasioambukiza na sisi kama uongozi wa Bugando tumekuja na wazo la Bugando Health Marathon lenye lengo la kuchangia watoto wanaoteseka na saratani.
Tunapotimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa klabu ya Bugando Fitness nitumie nafasi hii kuhamasisha jamii na Watanzania wote kwa ujumla kuungana nasi katika mbio za Bugando health Marathon ambapo kwa kuchangia kiasi cha Tsh 35,000 utakuwa umesaidia Watoto wanaoteseka na janga hili" Amesema Dkt Massaga na kusema kuwa mgeni rasmi katika mbio hizi zinazotarajiwa kufanyika Agosti 31, 2024 atakuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati mheshimiwa Dkt. Dotto Biteko.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia klabu ya mazoezi inayojumuisha wafanyakazi wa Bugando, CUHAS, MWACHAS
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia klabu ya mazoezi inayojumuisha wafanyakazi wa Bugando, CUHAS, MWACHAS
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia klabu ya mazoezi inayojumuisha wafanyakazi wa Bugando, CUHAS, MWACHAS pamoja na jamii inayoizunguka imetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ambapo klabu hii ya Bugando Fitness ilianzishwa rasmi Julai 19, 2023 ikiwa na jumla ya watumishi 15 na leo Julai 27, 2024 imetimiza mwaka huku ikiwa na wanachama 107.
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO YAFANYA KIKAO NA WAZABUNI WAKE.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amefanya kikao na wazabuni wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo likiwa ni kujadili mikakati mbalimbali na kuimarisha mahusiano Mazuri
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amefanya kikao na wazabuni wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo likiwa ni kujadili mikakati mbalimbali na kuimarisha mahusiano Mazuri baina ya wazabuni na Hospitali ya Bugando.
Akizungumza katika kikao hicho Dkt.Massaga amewashukuru wazabuni hao kwa ushirikiano mkubwa wanaotoa kwa Hospitali na kuwaeleza wazabuni hao namna Hospitali inavyozidi kuboresha na kutoa huduma za kibingwa na Bingwa bobezi pamoja na mipango ya baadae ya Hospitali. Aidha, Mkurugenzi Mkuu ameomba wazabuni kuleta vifaa mbalimbali vinavyokuwa vimeombwa na Hospitali na kuwaomba kutojiingiza kwenye udanganyifu wa aina yoyote.
Pamoja na hayo Mkurugenzi Mkuu amewaomba kuwa waangalifu hasa pale baadhi ya Watumishi wanapotumia jina lake kuomba au kujipatia pesa.Pia Mkurugenzi mkuu ameshughulikia changamoto zote ambazo wazabuni hao wamekuwa wakizipata. Dkt.Massaga amewaomba wazabuni kumuunga mkono katika suala zima la mbio za hisani za Bugando Health Marathon kwaajili ya kusaidia watoto wenye saratani ambapo mbio hizi kwa mara ya kwanza zitafanyika Tarehe 31/08/2024.
Hata hivyo baadhi ya wazabuni wamepata wasaa wa kutoa hoja zao ikiwemo kupongeza huduma za uendeshaji wa Hospitali ya Bugando kuwaeleza changamoto ambazo Mkurugenzi Mkuu ameanza kuzitatua. Wazabuni wamemuunga mkono Mkurugenzi mkuu kwa kuchangia fedha kwaajili ya mbio za hisani za Bugando Health Marathon.
BUGANDO KUANZA KUTUMIA SINDANO MAALUM NA UPASUAJI WA MATUNDU MADOGO KUTIBU MGONGO.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kuanza kutumia teknolojia mpya na ya kisasa katika matibabu na upasuaji wa mgongo na uti wa mgongo kwa kutumia sindano pamoja na upasuaji wa kisasa wa matundu madogo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kuanza kutumia teknolojia mpya na ya kisasa katika matibabu na upasuaji wa mgongo na uti wa mgongo kwa kutumia sindano pamoja na upasuaji wa kisasa wa matundu madogo.
Haya yamebainishwa na Daktari Bingwa bobezi wa Mifupa, Andrew Nkirijiwa wakati wa kambi maalum ya upasuaji wa mgongo na uti wa mgongo inayoendelea Bugando ikihusisha Wataalam wa Mifupa kutoka Bugando na Chuo cha Kikatoliki cha Valencia - Hispania.
“Sasa Hospitali ya Bugando inatoa huduma ya uchomaji sindano maalumu na upasuaji wa kisasa wa matundu madogo kwa watu wenye matatizo na maumivu ya mgongo badala ya kufanya upasuaji wa kufungua mgongo. Huduma hii ni endelevu na hapa ni wasihi wenye changamoto za maumivu ya mgongo kujitokeza kupata huduma hii hapa Bugando” Dkt. Andrew.
Aidha Dkt. Andrew Nkirijiwa ameshukuru wageni kutoka Valencia kwa ushirikiano, msaada na jitahada zao walizofanya kwani wamesaidia sana katika huduma hii hapa Hospitalini Bugando. Pia bila kusahau uongozi wa Hospitali ya Bugando pamoja na chuo kikuu cha CUHAS kuweza kushirikiana kufanikisha kambi hii.
MWANZILISHI WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA ICAP ATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
Dkt. Wafaa El-Sadr (MD,MPH,MPA) ambaye ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Shirika la kimataifa la ICAP na mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza na elimu ya Afya kwa jamii kutokea Nchini Marekani ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Dkt. Wafaa El-Sadr (MD,MPH,MPA) ambaye ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Shirika la kimataifa la ICAP na mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza na elimu ya Afya kwa jamii kutokea Nchini Marekani ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo likiwa ni kuangalia mchango unaotolewa na shirika la kimataifa la ICAP katika utoaji huduma za tiba na matunzo, Maabara ya upimaji wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa za Virusi vya UKIMWI pamoja na upimaji wa ueneaji wa Virusi vya UKIMWI na maambukuzi ya Virusi vya UKIMWI kwa watoto waliopo kwenye hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Akizungumza katika ujio huo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amewakaribisha na kuwashukuru viongozi wa shirika la ICAP kwa ushirikiano mkubwa wanaouonyesha katika utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za maabara na CTC katika Hospitali ya Bugando ambayo inahudumia takribani Mikoa nane ya Kanda ya Ziwa na hata nje ya Kanda ya ziwa.
"sisi kama shirika la ICAP tunayo furaha na shauku kuendelea kufanya kazi na Hospitali ya Bugando kwa kuwa tunaona jinsi ambavyo Hospitali hii inatoa huduma bora na nzuri kwa wagonjwa jambo ambalo linatuonyesha kuwa tunafikia malengo yetu" amesema Dkt. Wafaa El-Sadr.
Naye Dkt. Linda P. Fried ambae ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Columbia lrying Medical Center amempongeza Dkt. Massaga kwa utendaji wake wa kazi pamoja na wafanyakazi kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa.
MKURUGENZI MKUU TUME YA NGUVU ZA KIATOMU TANZANIA (TAEC) ATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Kiatomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed mapema leo Julai 5, 2024 amefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Kiatomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed mapema leo Julai 5, 2024 amefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kujitambulisha na kufahamu maeneo ya mashirikiano na miradi ambayo TAEC inashirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Prof. Najma amebainisha kuwa, anafanya ziara katika Taasisi zenye mashirikiano na TAEC kujua maeneo ambayo TAEC inahusika
" Nina wiki moja tangu nimeteuliwa, nikaona nipitie maeneo ambayo TAEC ina mashirikiano na kupitia wasilisho la Bugando kuna mambo TAEC inaweza kusaidia ikiwemo upungufu wa wafanyakazi na mafunzo, tuna mfuko wa Mama Samia Scholarship tunaomba muwasisitize watumishi waombe" Prof. Najat.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amempongeza Mkurugenzi mpya wa TAEC kwa kuteuliwa na Mhe. Rais na kuishukuru TAEC kwa kuendelea kuwezesha Hospitali ya Bugando kwa Vifaa na mafunzo katika eneo hilo na msaada wa kiufundi katika eneo hilo la matibabu kwa kutumia mionzi na kueleza kuwa uhitaji bado ni mkubwa kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa saratani wanaohudumiwa na Hospitali ya Bugando
" Hospitali ya Bugando ni ya pili kwa ukubwa na kwa huduma ya saratani inafuatia baada ya Ocean Road, tunahudumia wagonjwa wa saratani 120 kwa siku na tuna uhaba wa mashine za matibabu ya mionzi ya nje na ndani hali inayopelekea kubebesha mzigo mkubwa mashine zilizopo badala ya kuhudumia wagonjwa 80 kwa siku na inapotokea changamoto kwa mashine hizi wagonjwa wanapata shida kubwa na kama tunavojua unapochelewa matibabu ndivyo na tatizo linazidi" amesisitiza Dkt. Massaga.
Dkt. Massaga pia ameendelea kwa kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha huduma ya saratani Bugando kwa kuwekeza katika vifaa na wataalamu wa tiba mionzi.
PROF. PASCHALIS RUGARABAMU AAGWA BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE KAMA MAKAMU MKUU WA CHUO CHA CUHAS - BUGANDO
PROF. ERASMUS KAMUGISHA AKARIBISHWA KUWA MAKAMU MKUU WA CHUO CHA CUHAS - BUGANDO.
Mhashamu Baba Askofu
Severine Niwemugizi Askofu wa Jimbo kuu Katoliki Rulenge Ngara ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Kikatoliki Cha Afya ya Sayansi Shirikishi (CUHAS) amewakilisha Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) kuadhimisha ibada ya misa takatifu ameungana na Waumini wa Jumuiya ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Chuo Kikuu cha CUHAS na MWACHAS kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo cha CUHAS Prof. Paschalis Rugarabamu aliyemaliza muda wake na kumkaribisha Makamu Mkuu mpya wa chuo cha CUHAS Prof. Erasmus Kamugisha hii leo tarehe 28 June 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Wolfgang Pisa, Askofu. Severine Niwemugizi amempongeza Prof. Rugarabamu kwa utendaji bora na wa mfano kwa muda wote wa miaka 10.
"Kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, tunamshukuru Profesa Rugarabamu kwa kazi kubwa sana ambayo amefanya kwa Chuo chetu, tunamshukuru sana. Ulikuwa na Taasisi hii moyoni mwako ukitaka ikue na itoe matunda mazuri na kwa kweli jamii imekwishapokea hayo matunda kutoka hapa CUHAS wako huko wanahudumia jamii, ni lazima tukushukuru kabisa na Baraza linatambua, linathamini kazi nzuri uliyoifanya hapa, haswa ukiwa mnyenyekevu, mwadilifu, unayejituma bila kujihurumia, hilo tunajifunza kwako"
"Prof Kamugisha Asante kwa kukubali kubeba jukumu hili zito na karibu sana, naamini jamii ya CUHAS inakupokea Kwa moyo wa dhati kabisa na itakupa ushirikiano, Mungu akubariki uweze kutenda kazi yako kwa uadilifu na wengine wote Mungu awabariki" Amesema Askofu Severine Niwemugizi.
MAADHIMISHO YA SIKU YA SIKO SELI (SELI MUNDU) DUNIANI 19 JUNI, 2024.
Jamii yatakiwa kujenga utamaduni wa kupima na kuchunguza afya ili kutambua mapema hali ya maambukizi ya Siko Seli na kuchukua hatua za haraka.
Jamii yatakiwa kujenga utamaduni wa kupima na kuchunguza afya ili kutambua mapema hali ya maambukizi ya Siko Seli na kuchukua hatua za haraka za kuhudhuria Kliniki na kupata huduma stahiki.
Rai hii imetolewa mapema leo Juni 19, 2024 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt. Fabian A. Massaga katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Siko Seli akiwa mgeni rasmi wa hafla hii iliyoadhimishwa Hospitali ya Bugando.
Dkt. Bahati wajanga amefafanua
"Ugonjwa huu wa Siko Seli umeathiri zaidi Tanzania huku idadi kubwa ya wagonjwa ikitokea Kanda ya Ziwa karibu robo tatu ambapo kila mwaka wagonjwa 14,000 wanagundulika na miongoni mwao 10,000 wanatokea Kanda ya ziwa na kati ya watu wanne mmoja wao ana vinasaba vya Siko Seli.
Dkt. Wajanga ameendelea kwa kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kuboresha huduma za afya na kununua dawa na vifaa tiba stahiki kwa jamii ya wagonjwa wa Siko Seli.
Kwa upande wake mwakilishi wa Jamii ya watu wenye Siko Seli Bi. Vivian Kazembe ameiomba Serikali kuimarisha matibabu ya Siko Seli kwa watu wazima kama ilivyo kwa watoto na kuitaka jamii kujitokeza kupima na kutambua hali zao.
HOSPITALI YA BUGANDO YAWAJENGEA UWEZO WATAALAMU WA MASHINE ZA UCHUNGUZI WA MAGONJWA KWA NJIA YA MIONZI.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando yapongezwa kwa kuwajengea uwezo Wataalamu wa mashine za uchunguzi wa magonjwa kwa njia ya Mionzi(CT scan) kutoka Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa nchini Tanzania.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando yapongezwa kwa kuwajengea uwezo Wataalamu wa mashine za uchunguzi wa magonjwa kwa njia ya Mionzi(CT scan) kutoka Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa nchini Tanzania.
Pongezi hizi zimetolewa na Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RNO) Bi. Claudia ambaye amemwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa mapema leo Juni 18, 2024.
Bi. Claudia amesema "Tunajivunia Hospitali ya Bugando Juhudi zenu za kusaidia Hospitali za Rufaa za Mikoa kuboresha huduma hii ya Vipimo vya Tiba Mionzi" na kuwataka washiriki kuwa wasikivu wakati wote wa mafunzo kwa manufaa yao na Taasisi wanazofanyia kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amepongeza waandaji na wafadhili wa mafunzo haya huku akitanabaisha kuwa mafunzo haya ni muhimu si tu kusaidia huduma bora kwa wagonjwa lakini pia inakwenda kusaidia utunzaji wa vifaa kutokana na ujuzi watakaoupata na hii ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ambayo imewekeza katika ununuzi wa vifaa vya tiba Mionzi katika hospitali za Rufaa za Mikoa nchini.
Ndugu Baraka Kajubu ambaye ni Kaimu Meneja wa Kanda TAEC amesisitiza kuwa mafunzo haya yanakwenda kuongeza ujuzi katika utendaji kazi wa siku kwa siku.
Mafunzo haya ya siku tano yanafanywa na Hospitali ya Bugando kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Kiatomu (International Atomic Energy Agency) na yametolewa na Wataalamu wafizikia tiba kutoka Bugando Dkt. Benard Gombanila na Ndg. Bronwin Van Wyk akiambatana na Ndg. Hendrik de Vos kutoka nchini Afrika Kusini.
MHASHAMU BABA ASKOFU RENATUS NKWANDE AFANYA ZIARA HOSPITALI YA BUGANDO.
MHASHAMU BABA ASKOFU RENATUS NKWANDE AFANYA ZIARA HOSPITALI YA BUGANDO.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na Askofu Mkuu Jimbo Katoliki Mkoa wa Mwanza, Mhashamu Baba Askofu Renatus Nkwande, leo June 8, 2024 ametembelea Hospitali ya Bugando na kuongoza Misa Takatifu ya Kipaimara katika kanisa la Mt. Martin De Porres lililopo katika Hospitali hiyo na baadaye kuongea na Watumishi wa Jumuiya Hospitali ya Bugando, CUHAS na MWACHAS ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka kufanya ziara ya kukutana na Jumuiya hizo kukumbukumbushana machache kuhusu majukumu katika utendaji kazi .
Akizungumza mara baada ya Misa Takatifu, Baba Askofu Renatus Nkwande amewasisitizia wanajumuia nzima ya Bugando kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi, kujitoa kwa upendo na huruma wakati wa kuwahudumia wagonjwa huku tukijali miongozo na thamani zetu hasa maeneo yetu ya kazi. Pia, Baba Askofu Renatus Nkwande amewasihi Wafanyakazi kuwa na moyo wa uvumilivu hasa wanapokumbana na changamoto mbalimbali.
Sambamba na ziara hiyo Mhashamu Baba Askofu, amezindua rasmi Jumuiya ya Wafanyakazi Wakatoliki ya Bugando, CUHAS na MWACHA na kupongeza muungano huo, nakuomba umoja huo ukalete tija na manufaa kwa watu tunaowahudumia katika jamii yetu. Pamoja na hayo zawadi mbalimbali zimetolewa kwa Baba Askofu na wanajumuiya ikiwa ni shukrani na majitoleo yao.
Mwisho ameshukuru Uongozi wa Hospitali ya Bugando, CUHAS, na MWACHAS pamoja Wafanyakazi wote kwa majitoleo yao, kujitoa na kufika kwa kuacha shughuli zao.
MAABARA YA UPIMAJI WA USUGU WA DAWA ZA VIRUSI VYA UKIMWI YAZINDULIWA RASMI BUGANDO
MAABARA YA UPIMAJI WA USUGU WA DAWA ZA VIRUSI VYA UKIMWI YAZINDULIWA RASMI BUGANDO
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando yakabidhiwa maabara ya kupima usugu wa dawa za maambukizi ya virusi vya ukimwi yenye ubora na itakayohudumia zaidi ya Mikoa nane ya Kanda ya Ziwa na kuhakikisha upatikanaji wa haraka wa huduma za vipimo.
Maabara hii imekarabatiwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia mfuko wa dharura wa kupambana na Ukimwi (PEPFAR), Center of for Diseases Control and Prevention (CDC ) ikishirikiana na ICAP.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mohammed Mtanda ambaye ni mgeni rasmi ameipongeza Hospitali ya Bugando kwa kuwa kituo bora kinachohudumia Mikoa nane Kanda ya Ziwa na kupongeza jitihada za PEPFAR, CDC na ICAP kwa ushirikiano endelevu na kusema " tunashukuru kwa ushirikiano tunaoupokea kutoka katika Bunge na serikali ya Marekani kupitia CDC tumeweza kuweka mikakati mbalimbali katika tiba na mafunzo ya Ukimwi katika vituo vya Afya ambayo imesaidia kupunguza maambukizi kutoka asilimia 7.2 kwa mwaka 2016-2017 mpaka 4.7 kwa mwaka 2022- 2023" .
Sambamba na hayo Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amesema uwepo wa maabara hii utaleta mazingira rafiki kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na wanasayansi mbalimbali nchini katika kufanya mafunzo na tafiti zitakazoleta mapinduzi chanya katika huduma za Afya.
Dkt Massaga amewapongeza wadau hao kwa kuomba mashirikiano haya yawe endelevu.
MTAALAMU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA NGUVU ZA ATOMU ATEMBELEA BUGANDO.
MTAALAMU WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA NGUVU ZA ATOMU ATEMBELEA BUGANDO.
Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando kupitia Kitengo cha mionzi ya nyuklia na idara ya Saratani imetembelewa na mtaalamu kutoka shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (International Atomic Energy Agency)
kutoka Viena Austria Ndugu Mauro Carrara ambaye ni mshauri wa kitaalamu wa mradi unaotekelezwa kati ya Tanzania na Shirika la *IAEA* ambapo Bugando ni mdau mmojawapo.
Lengo ni kufatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo na kuandaa mipango ya utekelezaji kwa Mwaka 2025.
Bugando imefaidika na mradi huo kwa kupata nafasi za masomo pamoja na vifaa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya Saratani kwa njia ya mionzi.
Akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika kati ya mtaalamu huyo na Uongozi wa Hospitali ya Bugando, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dkt. Fabian A. Massaga amemshukuru na kumkaribisha mtaalamu huyo huku akibainisha kuwa Mradi huu umeinufaisha na unaendelea kuinufaisha Hospitali ya Bugando kwa kuwezesha mafunzo kwa wataalamu wa Bugando na ununuzi wa vifaa tiba jambo ambalo linasaidia kuongeza na kuboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa wa saratani na kutimiza adhma ya serikali ya kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora ya afya. Kwa Kanda ya Ziwa ni Hospitali ya Bugando ndio imechaguliwa na Serikali kusimamia matibabu ya saratani na inahudumia takribani wananchi Millioni 22 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na Magharibi ambao ni theruthi ya wananchi wote wa Tanzania.
Kwa upande wake Mtaalamu kutoka IAEA Ndugu Mauro mbali na kuipongeza hospitali ya Bugando kwa huduma wanayoitoa amesisitiza kupanga bajeti ya matengenezo kinga ya mashine za mionzi ili kuondoa adha ya mashine kuharibika na kusitishwa kwa huduma mara kwa mara.
Aidha ameahidi kuwa shirika la IAEA litaendelea kushirikiana kwa ukaribu na Bugando ili kuhakikisha huduma za tiba ya Saratani kwa njia ya mionzi zinaboreka na kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imewaaga madaktari watatu kutoka nchini Cuba waliofanya kazi na Hospitali ya Bugando kwa takribani miaka sita, hii leo terehe 15 Julai 2024.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imewaaga madaktari watatu kutoka nchini Cuba waliofanya kazi na Hospitali ya Bugando kwa takribani miaka sita, hii leo terehe 15 Julai 2024.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imewaaga madaktari watatu kutoka nchini Cuba waliofanya kazi na Hospitali ya Bugando kwa takribani miaka sita, hii leo terehe 15 Julai 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A.Massaga amewashukuru Madaktari hao kwa utumishi na utendaji mzuri wa kazi na kusema kuwa anatamani waendelee kuwepo katika Hospitali hii lakini kutokana na utaratibu wa nchi yao hana budi kuwaaga na pia anawakaribisha sana wakati mwingine.
Hata hivyo madaktari kutoka Cuba wamesema kuwa wamefurahishwa sana na ukarimu wa Tanzania hasa Hospitali ya Bugando na kusema kuwa Bugando ni nyumbani hivyo wataikumbuka na kuwa mabalozi wazuri huko waendako.
Zoezi hili la kuwaaga madaktari limeambatana na ugawaji wa vyeti vya shukrani kwa Madaktari hao wageni.
Kikundi cha Divine women (DW) kinachoundwa na wanachama kutoka mashirika mbalimbali wametembelea Hospitali ya Bugando
Kikundi cha Divine women (DW) kinachoundwa na wanachama kutoka mashirika mbalimbali wametembelea Hospitali ya Bugando
Kikundi cha Divine women (DW) kinachoundwa na wanachama kutoka mashirika mbalimbali wametembelea Hospitali ya Bugando katika Idara ya Saratani pamoja na kituo cha watoto wenye saratani katika Hospitali ya Rufaa Ya Kanda Bugando lengo likiwa ni kusaidia wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji hasa wagonjwa wenye saratani ambapo imekua desturi ya chama hicho kwa kila mwaka kusaidia watu wenye uhitaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt.Fabian A. Massaga amewapongeza na kuwashukuru wanachama wa Divine Women kwa majitoleo yao na kuwaeleza kuwa Hospitali inahudumia wagonjwa wengi ikiwemo wagonjwa wa saratani ambao wengi wao wanakumbana na changamoto za gharama za matibabu ya Saratani pamoja na gharama za kijamii wanapokuwa Hospitalini, jambo ambalo linasababisha asilimia 80% ya wagonjwa kufika Hospitalini wakiwa wamechelewa kuanza kupatiwa matibabu.Dkt Massaga ametoa wito kwa wanachama hao kuwa mabalozi kwa jamii inayowazunguka katika masuala ya Saratani.
Naye Pendo Shindo ambae ni Mwenyekiti msaidizi wa kikundi ameushukuru uongozi wa Hospitali kwa kuwapatia nafasi ya kuweza kuwaona wagonjwa wa saratani na kuahidi kuwa wataendelea kutoa majitoleo mara kwa mara kwa wagonjwa hao.
KIKUNDI CHA FAITH GROUP CHATOA MISAADA KWA WAGONJWA WA SARATANI BUGANDO
KIKUNDI CHA FAITH GROUP CHATOA MISAADA KWA WAGONJWA WA SARATANI BUGANDO
KIKUNDI CHA FAITH GROUP CHATOA MISAADA KWA WAGONJWA WA SARATANI BUGANDO
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea ugeni kutoka kikundi cha Wanawake cha FAITH GROUP cha Jijini Mwanza kwa lengo la kuwatembelea, kuwapa moyo na kutoa misaada mbalimbali kwa Wagonjwa wa Saratani hii leo tarehe 29 June 2024.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitu mbalimbali ikiwemo taulo za kike, pampasi, dawa za meno, miswaki, mafuta, vitambaa na sabuni, Mwenyekiti wa FAITH GROUP Kudra Nyahonge amesema kuwa ujio wao umesukumwa na uhitaji mkubwa wa Wagonjwa wa Saratani na hivyo kutoa kile walichobarikiwa katika kusaidia na kuwatia moyo wahitaji.
"Tumelenga Wanawake na Watoto kwa sababu kwa kipindi cha hivi karibuni tumepata taarifa saratani imekuwa kubwa kwa Wanawake na sisi tunatamani kuwa mabalozi wa kusaidia wengine kuamka kwenye hilo, tunaamini kuna watu wapo hapa hawana uwezo, hatutaweza kumaliza mahitaji yao yote lakini tutapunguza kwa namna Moja ama nyingine, hii ni sadaka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwajali wengine na kuonyesha huruma na upendo miongoni mwetu" Kudra Nyahonge.
Kwa upande wa Muuguzi Mussa Peter akiwamuwakilisha Mkuu wa Idara ya Saratani, amewapongeza FAITH GROUP kwa majitoleo hayo kwenda kugusa wahitaji wa Saratani kwani ni kweli uhitaji ni mkubwa na msaada huo utaenda kusaidia kuwapunguzia Wagonjwa na Ndugu ugumu wa kuuguza.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Juni 22,2024 imefaya kikao cha baraza la wafanyakazi na wajumbe
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Juni 22,2024 imefaya kikao cha baraza la wafanyakazi na wajumbe
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Juni 22,2024 imefaya kikao cha baraza la wafanyakazi na wajumbe wa baraza hilo wamepata nafasi ya kusomewa taarifa ya Hospitali na kujadili changamoto na dondoo mbalimbali za watumishi. Hata hivyo, Dkt Massaga amejibu hoja zote na dondoo za watumishi wa Bugando kwa kushirikiana na wakurugenzi wengine wa Hospitali hiyo.
Dkt.Fabian A Massaga ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando amewashukuru wajumbe kwa kuwa huru na kutoa mawazo ya kujenga.Amewaomba watumishi na wakuu wa idara kufanya kazi kwa weledi na kujikita katika utoaji wa huduma bora na zenye ubingwa bobezi
Naye makamu wa chuo cha CUHAS Prof.Paschalis Rugarabamu amepongeza uongozi wa Hospitali kwa maandalizi ya kikao na wajumbe kwa kutoa hoja zenye muelekeo mzuri ma kusema kuwa amepokea hoja zote zilizotolewa kwa upande wa Chuo cha CUHAS na kusema kuwa zipo katika utekelezaji.
Naye Prof. Hyasinta Jaka ambae ni Mkuu wa Chuo cha MWACHAS ameshukuru
Uongozi wa Hospitali kwa kuendelea kusaidia chuo cha MWACHAS na kuomba
Kuwe na kikao cha pamoja cha Idara za kudhibiti ubora (Quality Assurance) za BMC, CUHAS na MWACHAS.
Katibu wa Tughe Mkoa wa Mwanza Bw. Cleophace Butahe amepongeza uongozi wa Bugando na baraza la wafanyakazi kwa kusema kuwa baraza hili limekuwa zuri kwasababu wajumbe wamekuwa huru kwa kutoa hoja na si malalamiko na hii ni katika kuendeleza huduma bora.
Pia Bw. Cleophace amewataka wajumbe wa baraza la wafanyakazi kuwa mfano katika kuendesha taasisi kwa kujiepusha na tabia zisizo faa na kuwa waadilifu mahala pa kazi na kuwahudumia wateja kwa bidii ili kuongeza mapato katika Hospitali, hivyo amewaomba watumishi kufanya kazi kwa bidii.
WAUGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO WAPONGEZWA.
WAUGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO WAPONGEZWA.
WAUGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO WAPONGEZWA.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt Bahati Wajanga akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga ameungana na Chama cha Wauguzi tawi la Bugando (TANNA) kuadhimisha siku ya Wauguzi Duniani leo terehe 14 Juni 2024.
Katika hafla hiyo Dkt Bahati Wajanga amekipongeza Chama cha TANNA kwa kuwa na ushawishi mkubwa kwa kuwa na Wanachama zaidi ya 440 sambamba na kuwa kiungo muhimu kwenye maendeleo ya Hospitali ya Bugando;
"Kwanza nianze kuwapongenza sana kwa tendo hili la sherehe hongereni sana, Kuna mengi ambayo mmeyafanya, niwapongeze kwa mafanikio mengi mliyoyaeleza, mmekuwa mstari wa mbele hata kuwalipia Wanachama wenu ada ya leseni, nyie ni watumishi wa kuigwa,
"Niendelee kuwasisitiza, kuishi katika kiapo ambacho leo hii tumekirejea, mambo yaliyo kwenye kiapo yanaakisi maendeleo makubwa ya Hospitali yetu na mmekuwa sehemu kubwa ya maendeleo hayo na muendelee kuonesha upendo kwa Wagonjwa wetu kama ilivyo desturi yetu na niwatakie maadhimisho mema" amesema Dkt Bahati Wajanga.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr Salome Marando amepongeza Wauguzi wa Bugando kwa kazi kubwa wanayofanya usiku na mchana katika kuhudumia Wagonjwa na kuwakumbusha kuendelea kusimamia misingi ya taaluma zao katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Aidha, Mwenyekiti wa TANNA tawi la Bugando James Bhilananiye ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kuwa pamoja nao na kuwatimizia mahitaji mbalimbali kama Wauguzi na kuwaridhia kuungana na Dunia kuadhimisha siku yao kwa kutoa misaada kwa wahitaji na kuandaa tafrija kubwa jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt Bahati Wajanga akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A Massaga amepokea majitoleo mbalimbali
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt Bahati Wajanga akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A Massaga amepokea majitoleo mbalimbali
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt Bahati Wajanga akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A Massaga amepokea majitoleo mbalimbali kutoka kwa Wanachama wa Chama Cha Wauguzi tawi la Bugando(TANNA) katika kuadhimisha siku ya Wauguzi duniani kwa leo terehe 14, Juni 2024.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Dkt Bahati amesema;
"Kwanza niwapongeze sana TANNA wakati mnaadhimisha siku yenu mnafanya na matendo mema kwa kuwagusa wahitaji, tunawashukuru sana kwa haya majitoleo ambayo ni muhimu kwa kuwasaidia Wagonjwa na kuwapunguzia makali wanaowauguza, niwaombe tu muendelee na moyo huu kwani mahitaji haya ni endelevu na niwatakie kila la kheri kwenye sherehe yenu"
Kwa upande wa Mwenyekiti TANNA tawi la Bugando James Bhilananiye ameushukuru Uongozi wa Bugando kwa kuwapa fursa ya kutoa walichobarikiwa kwa kuwashika mkono wahitaji kwa kuwapatia sabuni, mafuta, pampas, dawa za meno na miswaki wakati wanadhimisha siku yao muhimu ya Wauguzi Duniani.
Chama cha Wauguzi tawi la Bugando kimeungana na Dunia kuadhimisha siku yao kwa kutoa majitoleo mbalimbali kwa Wagonjwa wa Saratani, watoto na watu wenye changamoto ya Magonjwa ya Afya ya akili na kuhitimishwa kwa tafrija kubwa jijini Mwanza.
MKURUGENZI MKUU WA HOSPITALI YA BUGANDO AWAPONGEZA WAUGUZI NA WAHUDUMU WA AFYA.
MKURUGENZI MKUU WA HOSPITALI YA BUGANDO AWAPONGEZA WAUGUZI NA WAHUDUMU WA AFYA.
MKURUGENZI MKUU WA HOSPITALI YA BUGANDO AWAPONGEZA WAUGUZI NA WAHUDUMU WA AFYA.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga na Viongozi wengine wa Hospitali wamefanya kikao cha Wauguzi na Wahudumu wa Afya lengo likiwa ni kuwakumbusha juu ya utendaji kazi, kusikiliza hoja zao ili kuzidi kuboresha huduma za Afya na Mazingira ya Kazi kwa Watumishi hao.
Akizungumza katika Kikao hicho Dkt. Massaga amewapongeza Wauguzi na Wahudumu wa Afya kwa kazi nzuri wanayofanya na kusema,
"Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya, sisi kama menejimenti tunafahamu mchango wenu,
katika Hospitali Wauguzi ndiyo shina la Hospitali, kazi yenu ni ngumu na ni kazi ya wito wengi wenu mnatimiza majukumu yenu ipasavyo hongereni sana.
Dkt.Massaga amewaomba wauguzi na wahudumu wa Afya kuendelea kuzingatia kauli nzuri na kutoa huduma bora kwa wagonjwa na kuongeza kwa kusema,
"wateja wetu hawajui mgawanyo wa idara na vitengo, hivyo ukimpokea mgonjwa msikilize na kumsaidia kufika sehemu anayoenda kupata huduma"
Aidha, Wauguzi na Wahudumu wa Afya wamepata fursa na kutoa maoni, ushauri na kuuliza maswali yaliyojibiwa na kutatuliwa huku wakiushukuru Uongozi kwa kutenga muda kuwasikiliza ikiwa katika kuboresha mazingira ya kazi na huduma za Afya kiujumla.
Wataalamu wa famasi na Radiolojia wa Hospitali ya Bugando wamekumbushwa kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya kazi,weledi wa hali ya juu
Wataalamu wa famasi na Radiolojia wa Hospitali ya Bugando wamekumbushwa kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya kazi,weledi wa hali ya juu
Wataalamu wa famasi na Radiolojia wa Hospitali ya Bugando wamekumbushwa kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya kazi,weledi wa hali ya juu,uaminifu na uadilifu na kutatua changamoto mara tu zinapotokea pindi wanapokuwa katika utoaji huduma.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt.Fabian Massaga ameyasema hayo katika kikao kazi na wataalamu hao akiwa ameambatana na wakurugenzi na viongozi wengine wa hospitali ya Bugando lengo likiwa ni kujadili na kusikiliza hoja mbalimbali za wafanyakazi ili kuboresha huduma zitolewazo hospitalini hapa.
Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Massaga amewapongeza wataalamu hao kwa ushirikiano na bidii wanayoionyesha kazini katika kuhakikisha matibabu ya mgonjwa yanakamilika na kusema " hospitali inatambua mchango, jitihada na bidii mnazozionesha katika utendaji kazi wenu, niahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa kuzitatua changamoto mlizoziwakilisha hapa”. Amesema Dkt. Massaga
Pia watumishi wameushukuru uongozi wa Bugando kwa kutoa nafasi ya kikao hiki na kusikiliza hoja na changamoto zao na kusema kikao hiki kitaongeza ufanisi na ushirikiano katika kazi
Wanawake wa kikundi cha SWIYAAM wametembelea Wagonjwa wa Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kutoa msaada,
Wanawake wa kikundi cha SWIYAAM wametembelea Wagonjwa wa Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kutoa msaada,
Wanawake wa kikundi cha SWIYAAM wametembelea Wagonjwa wa Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la kutoa msaada, kuwafariji wagonjwa na kupata elimu juu ya ugonjwa wa Saratani Mei 26, 2024.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Muuguzi wa Wagonjwa wa Saratani Dativa Zelamla akimuwakilisha Mkuu wa Idara ya Saratani amesema;
"Mgonjwa wa Saratani anatumia muda mwingi kwenye matibabu hivyo hata familia inapoteza rasilimali fedha na wanakuwa na uhitaji mkubwa, mmefanya jambo jema kwani msaada huu utasaidia kupunguza gharama kwa wagonjwa, tunawakaribisha muendelee na moyo huo huo wa kuwapa faraja watu wenye uhitaji"
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Wanawake Swaumu Yusuph ameushukuru Uongozi wa Bugando kwa kuwapokea kwani wamepata funzo kubwa kiimani kutembelea Wagonjwa wa Saratani ambapo itawakumbusha kuendelea kutenda matendo mema na kuacha alama nzuri kwenye jamii na wataenda kuwa mabalozi wazuri kupitia elimu ya Saratani waliyoipata.
Kikundi cha SWIYAAM chenye Wanachama 270 kimetoa pampasi, taulo za Kike, mafuta, sabuni na soksi kwa Wagonjwa wa Saratani huku wakipewa elimu juu ya ugonjwa wa huo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Magonjwa ya Dharura imemaliza kambi ya siku mbili ya utoaji wa huduma za Afya
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Magonjwa ya Dharura imemaliza kambi ya siku mbili ya utoaji wa huduma za Afya
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Magonjwa ya Dharura imemaliza kambi ya siku mbili ya utoaji wa huduma za Afya kwa upimaji wa Magonjwa mbalimbali kwa Wananchi bure ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya huduma za Dharura duniani ambapo kilele chake ni Juni 3, 2024.
Kambi hiyo ya siku mbili iliyoendeshwa na Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Idara ya Magonjwa ya Dharura kwenye eneo la Bugando Specialized Polyclinic (NERA) imefanya upimaji wa Sukari, upimaji wa Shinikizo la damu, upimaji wa uwiano wa uzito na urefu, ushauri wa lishe, upimaji na Virusi vya Ukimwi(VVU) na ushauri nasaha bure.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha utoaji huo wa huduma za Afya, Muuguzi Erick Mosses kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura amesema
"Kwa ujumla muitikio umekuwa mzuri kama tulivyotarajia na hii imetufurahisha kama Idara na Hospitali kuweza kufikia jamii, hivyo tunaamini kwa muitikio huu mkubwa tutakuwa tumetoa mwanga kwa Wananchi kutambua viashiria vya awali vya Magonjwa mbalimbali kwani wananchi wengi hawapati fursa hiyo na wataenda kuwa Mabalozi wazuri kupitia ushauri walioupata"
Kwa upande wa Wananchi waliohudhuria kupata huduma hizo wameishukuru Hospitali ya Bugando kwa kuwasogezea huduma hizo za Afya karibu yao na kuzitoa bure, jambo ambalo limewasadia kujua Afya zao ambayo ni nguzo katika shughuli zao za kila siku na ujenzi wa Taifa.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando itaadhimisha siku ya Magonjwa ya Dharura Duniani siku ya jumatatu ya 03 June 2024, maadhimisho yanayokwenda kwa kaulimbiu ya "Mabadiliko ya Tabia Nchi ni Dharura ya Kiafya pia"
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Dharura imeungana na Dunia nzima katika kuadhimisha wiki ya huduma za dharura duniani leo Juni 03,2024
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Dharura imeungana na Dunia nzima katika kuadhimisha wiki ya huduma za dharura duniani leo Juni 03,2024
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia Idara ya Dharura imeungana na Dunia nzima katika kuadhimisha wiki ya huduma za dharura duniani leo Juni 03,2024 iliyoambatana na kampeni ya kupambana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi yenye kauli mbiu isemayo "Mabadiliko ya Tabia ya Nchi ni Dharura ya Kiafya pia".
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando na Mgeni Rasmi wa maadhimisho hayo Dkt. Fabian A. Massaga amepongeza Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa ukarabati wa vyumba vya wagonjwa wa dharula na kuweka vifaa tiba vya kisasa ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
"Mabadiliko ya tabia ya Nchi ni tishio kubwa kwa wanadamu Duniani ambapo watu billioni 3.6 wanaishi katika mazingira hatarishi ya magonjwa ya kuambukiza ambapo hii ina maana kubwa katika utoaji wa huduma za dharura hivyo nitoe rai kwa wananchi na wafanyakazi kuchukua tahadhari kudhibiti mabadiliko haya ya Tabia Nchi kwa kupanda miti ili tuwe na mazingira rafiki kwa Afya zetu".
Dkt.Massaga amemaliza kwa kuipongeza Idara ya dharura na wadau mbalimbali kwa kutoa elimu na huduma ya uchunguzi wa Afya bure kwa wananchi wa Mwanza na viunga vyake, pia amewaasa kuendelea kufanya kazi kwa moyo huku wakizingatia miongozo na taratibu za kazi.
Aidha Dkt. Shazhmah Suleman ambaye ni Mkuu wa Idara ya Dharura ameishukuru uongozi wa Hospitali kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika idara kutoa ushauri na elimu wanayotoa katika kuendelea kuboresha huduma za dharura kwani huduma hii ni muhimu sana kwa wananchi.
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wamepata fursa ya kushiriki mafuzo ya ugonjwa wa kiharusi (stroke)
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wamepata fursa ya kushiriki mafuzo ya ugonjwa wa kiharusi (stroke)
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wamepata fursa ya kushiriki mafuzo ya ugonjwa wa kiharusi (stroke) yanayotolewa kwa njia ya mtandao kwa udhamini wa Hospitali ya Bugando na WORLD STROKE ORGANISATION, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo Watumishi wa kada mbalimbali pamoja na uanzishwaji rasmi wa stroke unit hapa bugando kama ambavyo Wizara ya Afya inaelekeza.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea mtambo wa kufua na kuzalisha hewa safi ya Oxygen (CYROGENIC PLANT)
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea mtambo wa kufua na kuzalisha hewa safi ya Oxygen (CYROGENIC PLANT)
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea mtambo wa kufua na kuzalisha hewa safi ya Oxygen (CYROGENIC PLANT) mtambo wenye uwezo wa kuzalisha mitungi 400 yenye ukubwa wa 6m3 kwa mda wa masaa 24 ukiondoa masaa 8 ya maandalizi.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospiatali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amepongeza wakurugenzi wote, Mhandisi Bwn Abhimanyu Kumar, Idara ya uhandisi kwa kazi kubwa ya kusimamia na kuhakikisha mradi huu umefanikiwa kwa kiwango kikubwa na kusema
"Ujuzi mlioupata kupitia mradi huu ukawe kipaumbele na fursa katika uzalishaji na ubora katika kazi pia mkawe walimu kwa wengine"
Aidha Dkt.Massaga amesisitiza watumishi wa uhandisi kufanya kazi kwa uadilifu hasa katika uzalishaji wa hewa safi. Hospitali ya Bugando inatumia mitungi takribani 100 kwa siku, hivyo Hospitali za Nje zitanufika na mtambo huu.
Aidha Bw.Abhimanyu Kumar Singh kutoka kampuni ya Universal Industrial Plant MFG Co L.T.D Delhi, India amesema "Mtambo huu ni salama na unauwezo wa kufua hewa safi yenye ubora wa kiwango cha juu na kwa wakati sahihi"
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Cde. Joel Kaminyonge akiambatana na viongozi wa TUGHE Mkoa wa Mwanza
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Cde. Joel Kaminyonge akiambatana na viongozi wa TUGHE Mkoa wa Mwanza
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Cde. Joel Kaminyonge akiambatana na viongozi wa TUGHE Mkoa wa Mwanza wamefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo likiwa ni kuwakumbusha Wanachama na Wafanyakazi umuhimu wa wajibu na haki zao mahala pa kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga amemshukuru Mwenyekiti na Uongozi wa TUGHE kwa kutembelea Hospitali ya Bugando na kusema
"TUGHE inaendelea kuwajali Wafanyakazi na sisi Bugando tutaendelea kushiriki katika kuboresha maslahi ya Wafanyakazi na kuendelea kutekeleza yale yote ambayo TUGHE inayasimamia na kusisitiza katika maeneo ya kazi ikiwemo uwajibikaji kwa wanachama wake kupitia kauli mbiu yao isemayo - Huduma bora, maslahi zaidi"
Bw. Joel Kaminyonge amefanya majadiliano ya pamoja na kujibu hoja mbalimbali za Wafanyakazi ikiwemo suala la kikokotoo kwa Wastaafu na Bima ya Afya, pia amesisitiza suala la uadilifu na uaminifu kwa Wafanyakazi na kuwataka viongozi kusimamia miongozo na taratibu za uongozi hasa katika kipindi cha uchaguzi wa mfanyakazi bora.
Cde.Joel amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga kwa kuwa Mfanyakazi bora Taifa wa mwaka 2023 na kuendelea kuwa mlezi wa Chama cha TUGHE pia ameshukuru Uongozi wa TUGHE Bugando chini ya Mwenyekiti wake Bwn. Daudi Makumcha kwa kuendelea kulea chama hiki kwa kufuata misingi na taratibu za Chama.
Kikao hiki kilimalizika kwa ugawaji wa Vyeti kwa Wafanyakazi bora wa Idara mbalimbali katika Hospitali ya Bugando.
MATENDO YA HURUMA KWA WAGONJWA
MATENDO YA HURUMA KWA WAGONJWA
MATENDO YA HURUMA KWA WAGONJWA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Mei 2, 2024 imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani zaidi ya shillingi laki saba ambavyo ni pampasi, sabuni na mafuta ya kupaka kutoka kwa Bi. Loura Evance mkazi wa kata ya Isamilo Jijini Mwanza.
Msaada huu umetolewa mahususi kwaajili ya watoto waliozaliwa na changamoto za vichwa vikubwa na mgongo wazi (spine bifida) pamoja na watoto waliofanyiwa pasuaji mbalimbali kwa lengo la kurudisha tumaini kwa jamii yenye uhitaji
Akizungumza katika makabidhiano hayo,
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Hospitali ya Bugando Sr. Sarome Marando kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali yaBugando amemshukuru Bi. Loura kwa majitoleo yake kwa wahitaji hususani watoto wanaopitia changamoto za kiafya
“Tunakushukuru kwa mchango wako na kwa kujali kipekee tunathamini na kutambua mchango wako, Mwenyezi Mungu akubariki sana kwa sadaka yako hii ulioitoa” amesema Sr. Salome Marado
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Bugando
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Bugando
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Bugando katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) Mkoani Mwanza yaliyofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katika maadhimisho hayo ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Saidi Mtanda amewapongeza Watumishi na kuwaomba kuendelea kufanya kazi kwa bidii na akiwataka kuendelea kuchapa kazi na kujiepusha na vitendo vinavyoenda kinyume na maadili ya umma ikiwemo kujihusisha na vitendo vya rushwa na ukosefu wa maadili ya utumishi.
Aidha, Mh Saidi Mtanda amesema amesikia na kupokea jumbe za Wafanyakazi walizotoa za maoni, ushauri na changamoto na atazifikisha sehemu husika ili ziwezw kufanyiwa kazi.
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani(Mei Mosi) kwa Mkoa wa Mwanza yameadhimishwa katika viwanja vya CCM Kirumba huku kitaifa yakifanyika Jijini Arusha.
Madaktari mbalimbali wa Hospitali na Vituo vya Afya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza
Madaktari mbalimbali wa Hospitali na Vituo vya Afya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza
Madaktari mbalimbali wa Hospitali na Vituo vya Afya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wakufunzi wa mafunzo ya matibabu ya Masikio na Usikivu yaliyoendeshwa na kuhitimishwa katika Hospitali ya Bugando leo Aprili 24, 2024.
Akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo hayo na kukabidhi vyeti kwa washiriki Dkt Pastory Mondea akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu Dkt Fabian A. Massaga amesema "Hospitali ya Bugando imebeba jukumu kubwa la kuwa Mlezi wa Hospitali na Vituo vya Afya Kanda ya Ziwa, mafunzo haya ni moja ya sehemu ya kuendelea kuboresha utoaji huduma katika Hospitali zetu hususani utoaji huduma wa matibabu ya Masikio na Usikivu ambayo imekuwa tatizo kwa wananchi, mkatumie mafunzo haya vizuri na mkawafundishe wengine"
Kwa upande wake Dkt Rodgers Machimu, Kaimu Mkuu wa Idara ya Pua, Koo na Masikio wa Hospitali ya Bugando amesema ili kuboresha matibabu ya Masikio na Usikivu Kanda ya Ziwa idara ya ENT imeona ni vema kutoa mafunzo kwa Madaktari na na Wauguzi wa Vituo vya Afya ili watu wapate huduma hiyo kwenye ngazi ya Vituo vya Afya na urahisi.
Aidha, washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Hospitali ya Bugando kwa mafunzo ambayo watayafanyia kazi na yatawasaidia kwenye utoaji wa huduma bora zaidi na kutatua tatizo la Masikio na Usikivu kwa Wananchi wanaowahudumia kwenye Vituo vyao kwa ubora zaidi kwani wamepata maarifa ambayo hawakuwa nayo kabla ya mafunzo.
Jumla ya Madaktari 23 wa Hospitali na Vituo vya Afya Wilaya Nyamagana wamepata mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia idara ya Pua, Koo na Masikio (ENT) kwa kushirikiana na Chuo cha San Francisco (Marekani) na Chuo cha Melbourne (Australia).
Madaktari mbalimbali toka Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya ya Nyamagana wamepata mafunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Madaktari mbalimbali toka Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya ya Nyamagana wamepata mafunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Madaktari mbalimbali toka Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya ya Nyamagana wamepata mafunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kupitia idara ya Pua, Koo na Masikio(ENT) kwa kushirikiana na Chuo cha San Francisco (Marekani) na Chuo cha Melbourne (Australia) ambapo mafunzo haya yamehusisha Madaktari 23 yakiwa na lengo la kuimarisha huduma na matibabu ya Masikio na Usikivu kwa Watu wa Kanda ya Ziwa.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo Aprili 23, 2024 na yatahitimishwa Aprili 24, 2024 katika Hospitali ya Bugando.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwapeleka watoto wa kike wenye umri wa Miaka 9 - 14 kupata chanjo ya saratani ya mlango wa Kizazi
Wazazi na walezi wametakiwa kuwapeleka watoto wa kike wenye umri wa Miaka 9 - 14 kupata chanjo ya saratani ya mlango wa Kizazi
Wazazi na walezi wametakiwa kuwapeleka watoto wa kike wenye umri wa Miaka 9 - 14 kupata chanjo ya saratani ya mlango wa Kizazi kwa madhumuni ya kuwalinda na kuwakinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya saratani hii.
Rai hii imetolewa mapema leo Aprili 22, 2024 na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na kuongozwa na kauli mbiu isemayo "Jamii iliyopata chanjo, jamii yenye Afya"
"Chanjo huokoa maisha, natoa wito kwa wazazi na walezi wote nchini kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo hii, chanjo hii ni salama na majaribio yamefanyika kimataifa na kitaifa kupitia Taasisi yetu ya utafiti ya NIMRI ikihusisha pia Mkoa wa Mwanza, tukumbuke matibabu ya saratani yanagharimu takribani Milioni.8 kwa mwaka wakati chanjo ni elfu 10, na hapa ndio tunasema kinga ni bora kuliko tiba" amesema Mhe. Ummy.
Mhe. Ummy ameongeza kuwa, hapo awali chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi imekua inatolewa mara mbili lakini walio wengi walikua wanaishia kuchoma chanjo moja na hawarudi kwa chanjo ya pili na hivyo kupelekea wataalamu kuja na chanjo itakayochomwa mara moja baada ya kujiridhisha.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Amina Makiragi amewapongeza na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya huku akiahidi kuwa wao kama Mkoa watalisimamia na kuhakikisha wanavuka lengo kwa kuhakikisha chanjo inawafikia wote wanaostahili kupata. Mhe. Makiragi pia amepongeza hatua ya Wizara kuuchagua Mkoa wa Mwanza kuzindua maadhimisho haya na kuahidi ushirikiano.
Saratani ya mlango wa kizazi inaambukizwa na virusi vilivyoko kwa jinsia ya kiume kupitia kujamiiana na ndio maana chanjo hii inatolewa kwa mabinti wa umri wa miaka 9 - 14 tukiamini hawajaanza kushiriki vitendo vya ngono.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba saidizi Dkt. Cosmas Mbulwa akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba saidizi Dkt. Cosmas Mbulwa akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba saidizi Dkt. Cosmas Mbulwa akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amefungua semina ya dawati la jinsia lililopo chini ya usimamizi wa Mwl.Halima Mwaisungu likiwa na usaidizi wa champions pioneer na Wafanyakazi kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, CUHAS na MWACHAS Lengo la semina hii ni kukumbusha na kuwajengea uwezo wafanyakazi kutambua, kuzuia, na kupinga ukatili kwa kufuata miongozo na kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Huduma za Tiba saidizi Dkt.Cosmas Mbulwa amewapongeza wadau, waanzilishi, waratibu na viongozi wa dawati hili na kusema "tunatambua na tunathamini mchango mkubwa wa dawati hili kwa kuwa husaidia jamii kwa kufuata masharti na matakwa ya kazi husika"
Dkt.Cosmas ameongeza kwa kusema kuwa ana imani kubwa na semina hiyo ambayo itaongeza umoja na ufanisi katika maeneo ya kazi.
Naye Prof. Dominica Morona akimwakilisha makamu mkuu wa chuo cha CUHAS Prof. Paschalis Rugarabamu ameshukuru uongozi kwa kutambua na kuthamini uwepo wa dawati hili na kutoa ushauri wa kuwepo kwa ukusanyaji wa taarifa mbalimbali na kufanyiwa tafiti kwa kina.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwekeza katika huduma za matibabu ya Saratani
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwekeza katika huduma za matibabu ya Saratani
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwekeza katika huduma za matibabu ya Saratani kwa kuongeza mashine moja ya kisasa ili wananchi wa Kanda ya Ziwa waweze kusogezewa huduma.
Mhe. Ummy amesema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslau Nyongo (MB), walipotembelea Hospitali ya Bugando leo Machi 14, 2024 lengo likiwa ni kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amesema Bugando imeendelea kuwekeza kwenye jamii yenye Afya na kuboresha huduma za jamii Kanda ya Ziwa, ambapo kupitia fedha za Uviko 19 ambazo zilitolewa na Serikali na kwa kutumia mapato ya ndani zimewezesha upatikanaji wa vifaa tiba kwa wagonjwa wa dharura, tiba mkoba, uboreshwaji wa miundombinu kama ujenzi wa jengo la saratani na macho pamoja na upanuzi wa ICU, hivyo kuhimili utoaji wa huduma za Afya kwa zaidi ya watu million 22 Kanda ya Ziwa.
Ziara hii imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bugando Mhashamu Baba Askofu Renatus Nkwande ambaye amesema Uongozi wa Bugando utaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha huduma za afya zinasonga mbele Kanda ya Ziwa na kupokea ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge pamoja na Waziri wa Afya.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa utoaji wa huduma bora unaozingatia teknolojia ya kisasa
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa utoaji wa huduma bora unaozingatia teknolojia ya kisasa
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa utoaji wa huduma bora unaozingatia teknolojia ya kisasa ikiwemo utumiaji wa mfumo wa TEHAMA katika utoaji huduma huku akizitaka Hospitali nyingine za Rufaa na Mikoa kuiga mfano wa Hospitali ya Bugando amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwekeza katika huduma za matibabu ya Saratani kwa kuongeza mashine moja ya kisasa ili wananchi wa Kanda ya Ziwa waweze kusogezewa huduma.
Pongezi hizi zimetolewa wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslau Nyongo (MB), walipotembelea Hospitali ya Bugando leo Machi 14, 2024 lengo likiwa ni kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amesema Bugando imeendelea kuwekeza kwenye jamii yenye Afya na kuboresha huduma za jamii Kanda ya Ziwa, ambapo kupitia fedha za Uviko 19 ambazo zilitolewa na Serikali na kwa kutumia mapato ya ndani zimewezesha upatikanaji wa vifaa tiba kwa wagonjwa wa dharura, tiba mkoba, uboreshwaji wa miundombinu kama ujenzi wa jengo la saratani na macho pamoja na upanuzi wa ICU, hivyo kuhimili utoaji wa huduma za Afya kwa zaidi ya watu million 22 Kanda ya Ziwa.
Kwa upande mwingine Dkt. Massaga amesema Bugando imepiga hatua kubwa kwenye matumizi ya TEHAMA ambayo inarahisisha utoaji wa huduma na uadilifu kwa watumishi. Pia, ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiipatia Bugando ikiwemo kuajiri watumishi, kulipa mishahara, uboreshwaji wa miundombinu sambamba na utoaji wa ufadhili wa elimu kupitia program ya Mama Samia Tuvushe.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa utoaji wa huduma bora unaozingatia teknolojia ya kisasa ikiwemo utumiaji wa mfumo wa TEHAMA katika utoaji huduma huku akizitaka Hospitali nyingine za Rufaa na Mikoa kuiga mfano wa Hospitali ya Bugando amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwekeza katika huduma za matibabu ya Saratani kwa kuongeza mashine moja ya kisasa ili wananchi wa Kanda ya Ziwa waweze kusogezewa huduma.
Pongezi hizi zimetolewa wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslau Nyongo (MB), walipotembelea Hospitali ya Bugando leo Machi 14, 2024 lengo likiwa ni kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amesema Bugando imeendelea kuwekeza kwenye jamii yenye Afya na kuboresha huduma za jamii Kanda ya Ziwa, ambapo kupitia fedha za Uviko 19 ambazo zilitolewa na Serikali na kwa kutumia mapato ya ndani zimewezesha upatikanaji wa vifaa tiba kwa wagonjwa wa dharura, tiba mkoba, uboreshwaji wa miundombinu kama ujenzi wa jengo la saratani na macho pamoja na upanuzi wa ICU, hivyo kuhimili utoaji wa huduma za Afya kwa zaidi ya watu million 22 Kanda ya Ziwa.
Kwa upande mwingine Dkt. Massaga amesema Bugando imepiga hatua kubwa kwenye matumizi ya TEHAMA ambayo inarahisisha utoaji wa huduma na uadilifu kwa watumishi. Pia, ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiipatia Bugando ikiwemo kuajiri watumishi, kulipa mishahara, uboreshwaji wa miundombinu sambamba na utoaji wa ufadhili wa elimu kupitia program ya Mama Samia Tuvushe.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Dkt Fabian A. Massaga
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Dkt Fabian A. Massaga
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Dkt Fabian A. Massaga ameendesha kikao kazi na Madaktari, kilichobeba ajenda mbalimbali ikiwemo ombi la Madaktari kuanzisha umoja wao, motisha, wajibu, mashirikiano sambamba na utatuaji wa changamoto za madaktari na namna ya uboreshwaji wa huduma za afya.
Dkt Massaga amewashukuru Viongozi wake waandamizi kwa kujibu hoja na kuwapongeza Madaktari kwa huduma nzuri wanazozitoa na kuwa wakweli na wawazi katika kufikisha hoja zao kwa uongozi ambazo zitaleta maboresho mazuri na chanya zaidi kwa taasisi na kusema ni matumaini kwamba umoja huu utaleta michango mizuri zaidi itakayofanya tufikie malengo tunayotamani kuyafikia, pia amewakumbusha kuwa na mahusiano mazuri baina yao na kada nyingine na kusisitiza kuendelea kutoa mawazo yao yanayowezesha maendeleo ya Hospitali.
Aidha Dr Massaga amewakumbusha madakitari kuhusu kitita kipya cha NHIF kilichoanza kutumika hapa Hospitalini tangu tarehe 1 March 2024 na kusema Hospitali ya Bugando inahudumia wagonjwa wote kwa wakati, nawasihi muendelee kutekeleza majukumu yenu bila kubagua mgonjwa.
Kwa upande wao Madaktari wameupongeza Uongozi wa Bugando kwa kusikiliza na kutatua hoja zao ili waweze kuendelea kutoa huduma kwenye mazingira rafiki na kuwawezesha kutoa huduma bora zaidi.
Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, tarehe 8 Machi ,2024
Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, tarehe 8 Machi ,2024
Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, tarehe 8 Machi ,2024 Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha huduma ya upimaji na uchunguzi wa Magonjwa ya Macho, masikio, saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza lengo likiwa ni kuwafikia wananchi ambao wanashindwa kufika hospitali kwa sababu mbalimbali.
Huduma hii ambayo inaratibiwa na Wanawake wa Bugando ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inafanyika kwa siku tatu mfululizo, tarehe 04 - 06, Machi 2024 katika maeneo ya Bujingwa Shule ya Sekondari, Buswelu round about na Mabatini. Akizungumzia huduma hii, Mwenyekiti wa Wanawake Bugando Bi. Eunice Kitula amesema "wanawake wa Bugando kwa kutambua kuwa jamii hususani wanawake wanakabiliwa na magonjwa mbalimbal ikiwemo kansa ya mlango wa kizazi na Kansa ya matiti na kwa bahati mbaya wengi wetu hatuna utaratibu wa kuchunguza afya zetu mara kwa mara, hali hii imetusukuma kuendesha huduma hii ili kubaini changamoto zozote za kiafya mapema na kuzipatia ufumbuzi kwa kuzitibu na kutoa ushauri wa kitaalamu na ndicho tunachokifanya " amesema Bi. Eunice Kitula na kuwakaribisha wananchi kujitokeza na kutumia fursa hii adhimu.
Kwa upande wake mtaalamu wa uoni Idara ya Macho Bw. Justice Daffa ametanabaisha kuwa sehemu kubwa kubwa ya wagonjwa waliowaona wana tatizo la uoni hafifu unaotokana na kurithi na wengine wachache umetokana na kujiumiza na vitu mbalimbali ikiwemo vijiti au peni. Bw. Daffa amesiaitiza Wazazi na Walimu kushirikiana kutambua tatizo la uoni hafifu mapema na kalipatia ufumbuzi mapema ili kuepukana na upofu unaoweza kuzuilika na kuongeza kuwa ni rahisi Mwalimu kugundua tatizo la uoni kwa kumwangalia Mwanafunzi kushindwa kuona ubaoni akiwa mbali au akiwa karibu.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata ugeni kutoka makao makuu ya ICAP New York
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata ugeni kutoka makao makuu ya ICAP New York
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata ugeni kutoka makao makuu ya ICAP New York nchini Marekani ukiongonzwa na Mkurugenzi mtendaji Bw. Mark Schnellbaeches aliyeambatana na timu kutoka ICAP Tanzania, ikiongonzwa na Mkurugenzi mkazi Dr. Haruka Maruyama. Ugeni huu umekuwa ni mwendelezo wa mashirikiano kati ya pande zote mbili katika vipimo na matibabu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt Fabian A.Massaga amewashukuru ICAP kwa mashirikiano yaliyopo na kwa namna wanavyoongeza nguvu katika kuwasaidia wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya Ukimwi,kuwezesha watumishi, vifaa tiba na vitendanishi katika maabara yetu ya vinasaba (Molecular Laboratory) na kitengo cha CTC,PMCTC na THIS. Pia Dkt Massaga amewaomba ICAP kuendelea kuisaidia Bugando HIV Pediatric Clinic kwa watoto wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Wananchi wa Mkoa wa Mwanza na viunga vyake wameshauriwa kujenga
Wananchi wa Mkoa wa Mwanza na viunga vyake wameshauriwa kujenga
Wananchi wa Mkoa wa Mwanza na viunga vyake wameshauriwa kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kugundua changamoto zinazowakabili na kuzitibu kabla ya kufikia hatua mbaya.
Wito huu umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wakati wa hafla ya kuhitimisha huduma ya uchunguzi uliyofanyika mapema Februari 29, 2024 katika Wilaya tatu za Busega, Simiyu, Nyamagana na Sengerema Mkoa wa Mwanza na umehusisha magonjwa ya Ini, Figo, mfuko wa nyongo na Tezi dume. Dkt. Massaga amesisitiza kuwa "Tuwe na nafasi ya kufanya uchunguzi wa afya zetu tusisubili kuugua, tupate elimu kutoka kwa wataalamu wa afya na sisi kama wataalamu tuwaelekeze wananchi wetu wanapopata changamoto wafike vituo vya afya" amesema Dkt. Massaga. Aidha Dkt. Massaga amewakumbusha wananchi kuzingatia suala la lishe na kujenga tabia ya kufanya mazoezi "Tufanye mazoezi, sisi Bugando tumekua mfano kila Jumanne na Ijumaa tunafanya mazoezi. tunawahamasisha wananchi kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora" Dkt. Massaga Pia ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Afya chini ya Waziri Mhe. Ummy Mwalimu inafanya vizuri sana, kuna uwekezaji mkubwa umefanyika kuanzia ngazi za vituo vya afya, tuliopo hapa tuyaone haya yaliyofanyika na Serikali kwa ajili ya Afya zetu.
kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mionzi Dkt. Magreth Magambo akitoa taarifa ya huduma hii, ametaarifu kuwa huduma hii imewanufaisha zaidi ya wananchi 500 ambapo kati yao asilimia 22% wamekutwa na magonjwa mbalimbali na wengi wao wameandikiwa Rufaa kuja Bugando kwa uchunguzi zaidi.
Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, ambayo hufanyika Machi 8
Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, ambayo hufanyika Machi 8
Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, ambayo hufanyika Machi 8 , Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imendelea kutoa huduma za upimaji na uchunguzi wa Magonjwa ya Macho, Masikio, Saratani ya matiti , Saratani ya mlango wa kizazi pamoja na magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu. Huduma hizi ni muendelezo zikiwa na lengo la kuwafikishia huduma wananchi wanaoshindwa kufika Hospitalini kutokana na sababu mbalimbali. Zoezi hili limeratibiwa na Wanawake Watumishi wa Bugando.
Wananchi wa Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu waimwagia sifa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Wananchi wa Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu waimwagia sifa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Wananchi wa Wilaya ya Busega wameipongeza Hospitali ya Bugando kwa mkakati wake ambao umekua endelevu wa kuwafuata na kuwasogezea wananchi huduma za kibingwa na bingwa bobezi lengo likiwa ni kuwafikia Wananchi wengi ambao wanashindwa kufika Bugando kutokana na sababu mbalimbali.]
pongezi hizi zimetolewa na wananchi wa Kata ya Igalukilo, wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa zoezi la uchunguzi na upimaji lililofanyika Februari 26, 2024 katika Kituo cha Afya Igalukilo kwa magonjwa ya homa ya ini, figo, tezi dume, Saratani ya Mlango wa kizazi na mfuko wa nyongo wamesema
" Tunashukuru sana wataalamu wa Hospitali ya Bugando kwa kuendelea kutujali kwa kutuletea huduma hii muhimu ya upimaji na uchunguzi bure kabisa, uhitaji ni mkubwa tunatamani huduma hii ifanyike hata kila mwezi ili kuwafikia wengi zaidi, wamama sisi tuna changamoto nyingi katika uzazi kwa huduma hii tuliyopata leo ya kipimo cha ultra sound imetusaidia kutambua mapema kama kuna tatizo na kuchukua hatua mapema za matibabu. amesema Bi. Suzana Kahabi Mkazi wa kijiji cha Manala - wela, Wilaya ya Busega.
kwa upande wake Diwani wa Kata ya Igalukilo Mhe. Lukale John Charles hakusita kumtaja na kumshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga kwa ushirikiano wake ambao amekua akiwapatia ikiwa pamoja nakuwezesha huduma hii ya uchunguzi kuendeshwa bure kwa wananchi wake na kuongeza kuwa huduma hizi zimewapunguzia gharama wananchi kwenda vituo vingine ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Busega ambayo ipo mbali.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeanzisha kituo maalumu cha matibabu ya vidonda kwa wagonjwa wa nje ( Outpatient Specialized Wound Care Center).
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeanzisha kituo maalumu cha matibabu ya vidonda kwa wagonjwa wa nje ( Outpatient Specialized Wound Care Center).
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeanzisha kituo maalumu cha matibabu ya vidonda kwa wagonjwa wa nje ( Outpatient Specialized Wound Care Center).
Kituo hiki kitatoa matibabu jumuishi kwa wagonjwa wote wenye changamoto za vidonda. Sambamba na hayo kituo kitatoa Huduma ya Tiba lishe, mazoezi tiba,huduma ya makovu baada ya kupona ikiwemo vidonda sugu ( chronic ulcers), vidonda vinavyotokana na kisukari ( Diabetic Ulcers), vidonda na ajali za moto ( Burn Wounds), vidonda vinavyotokana na ajali (Traumatic Wounds), huduma za vidonda vilivyotokana na upasuaji ( post surgery wounds) vidonda vilivyo katika mishipa ya damu na vidonda vinavyotokana na saratani ( Malignant Ulcers).
Akizungumza katika tukio hili, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian Massaga ameipongeza Kurugenzi ya upasuaji pamoja na idara ya upasuaji sanifu kwa kuwa wabunifu na kuanzisha kituo hiki muhimu, “ Kitu mlichoanzisha ni kikubwa na chenye tija na sisi kama menejimenti tutawapa ushirikiano mkubwa sana katika utekelezaji wa huduma hii, kitu hiki mlichoanzisha hakifanyiki katika hospitali nyingi hivyo niwapongeze sana kwa ubunifu huu na niwakumbushe kutoa huduma kwa huruma na upendo kama ilivyokauli mbiu yetu.” Amesema Dkt. Massaga
Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya njia mbadala ya upumuaji (Tracheostomy Care ) kwa muda wa siku mbili.
Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya njia mbadala ya upumuaji (Tracheostomy Care ) kwa muda wa siku mbili.
Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya njia mbadala ya upumuaji (Tracheostomy Care ) kwa muda wa siku mbili.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Bugando Dkt. Bahati Wajanga akiwaamemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian A. Massaga, amewapongeza wauguzi wahitimu wa mafunzo hayo, kwa kushiriki mafunzo haya muhimu katika kuwasaidia wagonjwa wenye changamoto za kupumua kwa kutumia njia mbadala kwa ufanisi zaidi na kuwataka kuandaa mpango kazi mzuri wa utekelezaji sahihi kwa vitendo kwa waliyojifunza katika mafunzo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr. Salome Marandu amesema Wauguzi wana umuhimu mkubwa kwenye matibabu, hivyo maarifa waliyoyapata kwenye mafunzo hayo wakawape na wengine katika utekelezaji bora wa majukumu yao ya uuguzi katika kuwahuduma wagonjwa.
Aidha, Mkuu wa Idara ya Pua, Koo na Masikio, Dkt. Rogers Machimu amesema, mafunzo hayo kwa Kiasi kikubwa yanaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Wauguzi hao kwenye majukumu yao kwani wameweza kupata maarifa mapya ya kusaidia wagonjwa wenye changamoto za upumuaji kupitia njia mbadala jambo ambalo linaungwa mkono na wauguzi waliopatiwa mafunzo hayo wakiahidi kwenda kufanyia kazi kwa vitendo yote waliyofundishwa.
Sambamba na hayo Dkt. Rogers pamoja na Wauguzi waliohitimu mafunzo haya wameushukuru uongozi kwa kuwapatia fursa yakuweza kushiriki katika mafunzo hayo na wameomba mafunzo hayo yawe endelevu ila yawe msaada kwa wengine pia.
Idara ya Mifupa ya hospitali ya Bugando imepokea vifaa tiba kutoka Kampuni ya Sign Fracture International
Idara ya Mifupa ya hospitali ya Bugando imepokea vifaa tiba kutoka Kampuni ya Sign Fracture International
Idara ya Mifupa ya hosptali ya Bugando imepokea vifaa tiba kutoka Kampuni ya Sign Fracture International ya nchini Marekani ikiwa ni muendelezo wa mashirikiano baina ya kampuni hii na hospitali ya Bugando katika maeneo mbalimbali ya kubadilishana uzoefu, mafunzo na utafiti tangu mwaka 2001.
Makabidhiano haya yamefanyika mapema leo Februari 20, 2024, na kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga na imejumuisha vifaa tiba maalum vya kisasa vya upasuaji kwaajili ya kutibu mivunjiko ya mifupa mirefu.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Dkt. Fabian A. Massaga ameshukuru kwa msaada
wa vifaa hivi huku akiwapongeza madaktari wa idara ya mifupa kwa jitihada kubwa wanazofanya kufanikisha maendeleo ya idara na taasisi kwa ujumla.
Pamoja na hayo Dkt. Massaga amewasisitiza madaktari wa idara hii kutumia fursa ya ushirikiano huu kufanya tafiti mbalimbali na kuongeza ujuzi zaidi katika kada yao. Vile vile amewahasa watumiaji wa vifaa hivi kuvitumia kwa uangalifu na kuvitunza ili viweze kuwa msaada kwa matibabu ya wagonjwa wetu.
Mbali ya kupokea vifaa hiyo, Mkurugenzi Mkuu amekabidhi vyeti vya shukrani kwa Kampuni ya Sign fracture International na kwa
Dkt. Wilson Masanja Daktari bingwa wa mifupa kwa kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivi.
Naye Dkt. Inyasi Akaro Mkuu wa Idara ya Mifupa ameushukuru uongozi wa Bugando kwa kuendelea kuwawezesha idara hiyo kufanikisha maendeleo mbalimbali ya idara ya mifupa ikiwemo upatikanaji wa vifaa hivi.
ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA BUGANDO
ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA BUGANDO
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe atembelea hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Mwanza, Dkt. Magembe ameambatana na timu kutoka wizara ya afya pamoja na timu ya mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza .
Dkt. Magembe na amewahimiza watumishi kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi , “ serikali imeendelea kuwekeza na kufanya maboresho mbali mbali hivyo imebaki sisi kutimiza wajibu wetu, tubadilike kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kwakuwa kila taaluma inayo miiko hivyo ni lazima tuzingatie miiko na weledi wa taaluma zetu, vile vile tuwe wabunifu tuendane na mabadiliko ya teknolojia/ tehama mabadiliko kama telemedicine (Tiba mtandao) “ Amesema Dkt. Magembe.
Sambamba na hayo naibu Katibu Mkuu ameupongeza uongozi wa Bugando kwa maboresho ya miundo na huduma yaliyofanyika vile vile amesema amepokea changamoto zilizowasilishwa na bugando na kusisitiza kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto hizi.
Dkt. Magembe amewahimiza vyuo vya Afya vilivyopo bugando vinawajibu wa kuwajengea uwezo watumishi wa kada ya afya ndani ya mikoa ya Kanda ya ziwa ili kuendelea kukuza sekta hii. Vile vile amesisitiza kuwa serikali inaendelea kutafuta wadau mbali mbali ambao wapo tayari kushirikiana na serikali katika matibabu ya saratani ambapo moja ya taasisi zitazonufaika ni hospitali ya Bugando.
Sambamba na hayo Dkt. Massaga ameendelea kuishukuru serikali kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa pesa za uviko 19 zilizoleta matengenezo na maboresho ya ICU, pamoja na Idara ya dharula, vile vile serikali imeisaidia taasisi kwa kuendelea kutoa ajira kwa watumishi pamoja na kutoa ufadhili wa masomo wa baadhi ya watumishi wa Bugando
Idara ya saratani Bugando imeadhimisha siku ya saratani za watoto duniani leo Februari 15,2024
Idara ya saratani Bugando imeadhimisha siku ya saratani za watoto duniani leo Februari 15,2024 kwa kutoa elimu kwa wazazi wa watoto wenye Saratani, maadhimisho haya yameambatana na kauli “ Kuongeza ufahamu wa saratani za watoto”.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Desk and Chair foundation
Bw. Sibtain Maghjee ambae ni Mgeni rasmi amesema takwimu zimeonesha ukubwa wa tatizo hili katika jamii yetu "Watoto 400,000 chini ya miaka 18 Duniani wanagundilika na Saratani kila mwaka" ili kukabiliana na tatizo hili serikali yetu kupitia Wizara ya Afya imeendelea kujenga miundombinu, Kufundisha wataalamu na kutoa vifaa tiba ili kusaidia wagonjwa wa saratani, pia amelipongeza Baraza la Maaskofu ( TEC),Wadau mbalimbali kwa uwezeshaji mkubwa uliofanikisha uanzishwaji na uboreshwaji wa huduma za matibabu ya Saratani kwa watanzania wote na hasa kwa watoto wetu, pamoja na hayo amesema elimu imeendelea kutolewa kwa jamii ili kujiepusha na vichocheo vya saratani, Ufahamu wa kugundua dalili za awali za saratani na kwenda kuchunguzwa mapema. Aidha ameiomba hospitali kuanzisha radio ambayo itasambaza elimu za afya kwa jamii kwa haraka ili wananchi waweze kupata uelewa juu ya magonjwa mbalimbali kwani radio inasaidia kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi.
Nae Mkurugenzi wa huduma saidizi Dkt. Cosmas Mbulwa amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dkt Fabian A. Massaga ameishukuru na kuipongeza serikali kwa kushirikiana na hospitali katika kuhakikisha watoto wanapata matibabu stahiki pia amewapongeza Idara ya Saratani ambao wanafanya kazi kwa juhudi kubwa ili kuhakikisha watoto hawa wanafikia ndoto zao kwa kupata matibabu stahiki na kusema Hospitali inaendelea kutoa elimu juu ya magonjwa ya saratani hasa maeneo ya vijijini.
Sambmba na hayo Daktari Bingwa Bobezi wa Magonjwa ya saratani za watoto Dkt. Heronima Joas amesema "Siku ya Saratani za watoto hutukumbusha ujasiri na uthubutu wa watoto katika kupambana na changamoto za Saratani mbalimbali. " Akihamasisha wananchi waliohudhuria katika maadhimisho haya kuwamabalozi kwa Wengine kwa elimu waliyoipata.
BALOZI WA CUBA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
BALOZI WA CUBA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
BALOZI WA CUBA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA HOSPITALI YA BUGANDO.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea ugeni wa muheshimiwa balozi Yodenis Despaigne Vera wa Cuba nchini Tanzania aliyeambatana na mke wake Bi. Anaisa Castellenaos Blanco pamoja na watendaji wa ubalozi wa Cuba nchini Tanzania ambao wapo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza na moja ya maeneo ambayo wametembelea ni hospitali ya rufaa ya kanda Bugando. Mhe. Balozi Yodenis amefurahishwa sana na maboresho makubwa yaliyofikiwa na hospitali ya Bugando na kuahidi kuendeleza ushirikiano kati ya Bugando kupitia Wizara ya Afya nchini Tanzania na Wizara ya Afya nchini Cuba, amesema wapo tayari kupokea maombi ya madaktari wapya ambao Bugando itahitaji na kuwaongezea muda madaktari waliopo. Sambasamba na hayo Mhe. Balozi Yodenis ameipongeza serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya nchini Tanzania kwa jitihada kubwa zinazofanyika za kuboresha sekta ya afya nchini, pia ameishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa ushirikiano waliopewa katika ziara hii, pamoja na uongozi wa Bugando kwa kuwapokea vizuri na yupo tayari kutoa ushirikiano katika maeneo ya kimkakati ambayo hospitali ya Bugando inatarajia kuyaimarisha ikiwemo ujenzi wa jengo la mama na mtoto, taasisi ya moyo, huduma za upandikizaji figo, taasisi ya matibabu ya mfumo wa chakula, pamoja na taasisi ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.
Kwa muda mrefu hospitali ya rufaa ya kanda Bugando imekuwa na ushirikiano katika maeneo mbali mbali na nchi ya Cuba, ikiwemo upande wa mafunzo na matibabu.
WATAALAMU WA MAABARA WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA HUDUMA ZA MAABARA.
WATAALAMU WA MAABARA WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA HUDUMA ZA MAABARA.
Mkurugenzi Mkuu wa Bugando Dkt. Fabian A Massaga ahitimisha kikao kazi cha wataalamu wa maabara kanda ya ziwa. Kikao hiki kimekutanisha wataalamu mbalimbali wa maabara wa ngazi ya mkoa na halmashauri pamoja na wadau wa kada hii wakiwa na lengo la kutoa mrejesho, mafanikio na changamoto zinazojitokeza katika kazi kwa kipindi cha mwaka mzima.
Akihitimisha kikao hicho Dkt. Massaga na amewapongeza viongozi mbalimbali kwa kuratibu kikao hicho Wakurugenzi, Wakuu wa Idara pamoja na waratibu wote ngazi ya Mkoa na halmashauri ikiwemo wadau mbalimbali na kuwahasa walioyajadili yakawe chachu na kuongeza weledi katika nafasi zao za kazi, Pia amewasisitiza wataalamu hao kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa jamii.
Naye Bw. Regan Kessy Mratibu wa huduma za maabara Mkoa wa Mwanza, ameipongeza Bugando kwa kuendelea kuwa na Maabara bora Kanda ya ziwa na Tanzania na kusema kikao hiki kimewakutanisha wataalamu mbali mbali na kuwapa nafasi ya kujadili mafanikio, changamoto na michango mbalimbali ambayo itasaidia katika uboreshwaji wa huduma zetu za maabara na kujifunza kwa namna gani Bugando imeweza kuwa na maabara bora zaidi kanda ya ziwa.
Pamoja na hayo Bw. John Daffi Meneja wa Maabara ya Hospitali ya Bugando amewashukuru wadau kwa kuweza kuhudhuria kikao kazi hiki kwa kuwa kitaenda kuhakikisha tunafanya kazi katika ubora na kutoa majibu sahihi na kwa wakati sahihi hivyo tukafanyie kazi tuliyoyapata hapa yakaongeze ubora zaidi katika nafasi zetu za kazi.
Benki ya NMB Kanda ya Ziwa imesherehekea siku ya wapendanao kwa kutoa misaada mbalimbali kwa watoto wanye mahitaji maalum waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Benki ya NMB Kanda ya Ziwa imesherehekea siku ya wapendanao kwa kutoa misaada mbalimbali kwa watoto wanye mahitaji maalum waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Watumishi hawa wa NMB wamefika katika wodi ya watoto walio katika uangalizi maalum na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Idara ya watoto Bi. Sophia Kassim kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu na ameushukuru uongozi wa NMB Kanda ya Ziwa kwa moyo wao wa kujitoa kuwasaidia watoto.
“Tunashukuru sana hii ni sehemu ya sadaka yenu mmeamua kuifanyia hapa na tunawaombea Mungu awazidishie pale mlipotoa na nawahakikishia kuwa msaada huu utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa, niombe taasisi nyingine kuiga mfano kwa NMB ” amesema bi. Sophia.
Kwa upande wake mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Ziwa Bw. Hamadan Sillia ametanabaisha lengo la Benki ya NMB kufanya zoezi hili kuwa
“Tumechagua kuja Hospitali ya Bugando kuonesha upendo na kusherehekea na watoto wenye mahitaji maalum kutokana na ukweli kua hii ni Hospitali ya Rufaa inayopokea watoto wenye changamoto zilizokosa usaidizi na utatuzi kwingine kwani Bugando ina idadi kubwa ya watoto wenye mahitaji maalum hivyo tumeona ni vema kusharekea siku kwa kujitoa kusaidia watoto hawa”. Amesema Bw. Hamadan
akizungumza kwa niaba ya wazazi wa wototo wenye mahitaji maalum, Bi. Happiness Astariko mbali na kupongeza huduma nzuri wanazopatiwa na wataalamu wa bugando , amewapongeza watumishi wa NMB kwa moyo wao wa majitoleo na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huo kwani bado wana uhitaji mkubwa ikiwa ni pamoja na wengi wa nashindwa kumudu gharama za matibabu.
TIMU YA KUZUIA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YAIPONGEZA BUGANDO
Timu ya kuzuia na kudhibiti maambukizi iliyokua ikifanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya hospitali ya Bugando,
TIMU YA KUZUIA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YAIPONGEZA BUGANDO
Timu ya kuzuia na kudhibiti maambukizi iliyokua ikifanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya hospitali ya Bugando, imeipongeza hospitali hii kwa kuweka juhudi katika kusimamia miongozo ya utoaji huduma na ubora wa maeneo ya kutolea huduma.
Kiongozi wa timu hiyo ya ukaguzi Dkt. Redempta Bahegwa ambaye ni Afisa uimarishaji ubora kitengo cha uhakiki ubora kutoka wizara ya afya, amepongeza maeneo ya wodi ya VIP, chumba cha uangalizi maalumu cha watoto (NICU) , chumba cha wagonjwa mahututi upande wa tiba ( Medical ICU) pamoja na wodi ya wagonjwa wa afya ya akili kwa kuwa nyenzo bora za kutolea huduma na mazingira bora vile vile ametoa mapendekezo ya maeneo ya kuboresha zaidi ili kuendelea kutoa huduma bora zinazofuata miongozo ya utoaji huduma.
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameipongeza timu hii kwa ukaguzi wenye tija uliolenga kuboresha utoaji wa huduma bora. Huku akielekeza wakuu wa idara kufanyia kazi maeneo yenye changamoto katika kuhakikisha huduma zinazidi kuimarika.
WARSHA KWA MADEREVA WA BMC, CUHAS, NA MWACHAS.
WARSHA KWA MADEREVA WA BMC, CUHAS, NA MWACHAS.
WARSHA KWA MADEREVA WA BMC, CUHAS, NA MWACHAS.
Madereva kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Chuo Kikuu cha kikatoliki cha Sayansi za afya shirikishi , na Chuo cha Mafunzo cha Sayansi na tiba ( MWACHAS) wamehudhuria Warsha iliyoandaliwa na dawati la jinsia kuhusiana mahusiano mahala pa kazi na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika maeneo ya kazi.
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amesema, agenda kubwa ni uadilifu na mahusiano mahala pa kazi ambayo yameambatana na (Gender based violence and harassment) na changamoto wanazokutana nazo katika kazi ambazo hupelekea misuguano mbalimbali . Dkt. Massaga amewahasa madereva wazingatie haya mafunzo na wakawe mabalozi kwa wengine. Aidha ameipongeza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa kuendelea kutoa na kusimamia miongozo.
Afisa mchunguzi mkuu wa TAKUKURU- Mkoa wa Mwanza Bi Maua Ally amewasisitiza watumishi hawa kuzingatia maadili na usiri katika kazi. Vile vile watoa mafunzo wengine akiwemo daktari bingwa wa afya ya Akili kutoka Bugando Dkt. Kiyeti Hauli amewahasa madereva kuweza kuweka uwiano kati ya maisha yao binafsi na maisha ya kazi haswa kupata muda wa kupumzika na kuepukana na ulevi na kuzingatia muda wa kufanya mazoezi ili kulinda afya zao za mwili na akili ili kuleta ufanisi zaidi katika kazi.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha CUHAS, Prof. Paschalis Rugarabamu akifunga mafunzo haya ameshukuru na kutoa wito kwa waandaaji wa mafunzo yasiishie kwa kundi la madereva bali yafanyike kwa makundi mengine ya watumishi.
Kanisa katoliki nchini limeungana na serikali kupitia Wizara ya afya na mpango wa taifa wa damu salama kuadhimisha kilele cha siku hii
Kanisa katoliki nchini limeungana na serikali kupitia Wizara ya afya na mpango wa taifa wa damu salama kuadhimisha kilele cha siku hii katika parokia ya Kristu Mfalme -Kiseke jimbo kuu la Mwanza.
Kanisa katoliki nchini limeungana na serikali kupitia Wizara ya afya na mpango wa taifa wa damu salama kuadhimisha kilele cha siku hii katika parokia ya Kristu Mfalme -Kiseke jimbo kuu la Mwanza. Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyoambatana na zoezi la uchangiaji damu, Mgeni Rasmi, Dkt. Abdu Juma Bhombo meneja mpango wa taifa wa damu salama ameeleza “Mpango umeweka lengo la kukusanya chupa za damu 23,618 katika Parokia zote nchini na kauli mbiu katika kampeni hii ni “Onesha Upendo kwa Wagonjwa, Changia Damu Okoa Maisha” iliyolenga kuonesha wajibu wa waumini wa kwa jamii na kudhihirisha moyo wa umoja, utu, upendo, huruma na kuwa mfano wa utumishi kwa jamii kwa kuwafikiria wagonjwa wenye uhitaji wa damu. Ushirikiano huu utawezesha serikali kufikia malengo yake mahsusi ya kuboresha huduma za damu salama nchini kwa kufikia mahitaji ya damu kwa asilimia 100% , wizara ya Afya inaahidi kutoa ushirikiano na kufanikisha adhima ya kanisa ya kuboresha huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na kuendeleza kampeni ya kuhamasisha na kukusanya damu nchi nzima kila Mwaka.” Amesema Dkt. Bhombo.
Aidha , Askofu Mkuu jimbo kuu la Mwanza Mhashamu Baba Askofu Renatus Nkwande ameeleza nia ya Kanisa ya kuadhimisha siku ya wagonjwa duniani, iwe ni siku ya kuchangia damu kitaifa “Baraza liliona ni vyema kila tunapoadhimisha siku hii tushiriki kuchangia damu, ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na wagonjwa na sisi kama kanisa lazima tuwasaidie wagonjwa kiroho na kimwili, mwaka huu tumeanza rasmi kwa kuhamasisha kila Parokia kushiriki zoezi hili endelevu , nawaomba sana haswa vijana ambao bado wana nguvu na afya njema kuendelea kuchangia damu ili wenzetu waendelee kupona” Amesema Askofu Nkwande.
MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI 04.02.2024
MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI 04.02.2024
MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI 04.02.2024
Elimu pamoja na Huduma za uchunguzi zimeendelea kutolewa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya saratani Duniani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa
ambaye ni Mgeni rasmi wa Maadhimisho hayo ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Bugando na Watumishi wote wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian A. Massaga kwa kuendelea kuisimamia vyema idara hii ya Saratani inayotoa Huduma katika kanda yaziwa na mikoa ya pembezoni. Pia akimshukuru Mkuu wa idara ya Saratani Dkt. Nestory Masalu kwa kuendelea kuwahudumia wagonjwa wa Saratani bila kuchoka.
Sambamba na hayo amewapongeza Mashujaa wa Saratani kwa kuwatia moyo wananchi na kwa namna wanavyojitoa ili kupigania Afya za watanzania kwa ujumla.
Pia amempongeza Bi. Stella Herman kwa kutoa elimu ,motisha na kurudisha fadhila kwa Hospitali ya Bugando akisema ugonjwa wa saratani bado ni changamoto kwa dunia na Serikali inaendelea kuimarisha huduma katika vituo vya Afya. "Serikali imesambaza mashine za Ultrasound na kuwajengea uwezo Watumishi namna ya kuhudumia wagonjwa wa saratani".
Dkt. Rutachunzibwa amesisitiza uzingatiaji wa kufanya mazoezi,kutokuvuta sigara,Ulaji wa chakula bora,chanjo ya Mlango wa kizazi,homa ya ini, kuacha pombe na Pia kuwa wasafi katika maeneo ya kazi,sehemu za uzalishaji ili kuweza kujikinga na magonjwa mbalimbali.
Pia ameendelea kuishukuru hospitali ya Bugando, Chuo cha CUHAS, na MWACHAS kwa kuwekeza nguvu zaidi katika kampeni ya udhibiti wa ugonjwa wa kichocho ambapo kwa asilimia ishirini na tano (25% ) kichocho kimeonekana kuchangia saratani ya kibofu.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, imepokea vifaa tiba ikiwemo
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, imepokea vifaa tiba ikiwemo
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, imepokea vifaa tiba ikiwemo (Thermometer, negulizer,stethoscope) kutoka katika chama cha Ushirika cha akiba na mikopo (SACCOS), Lengo likiwa ni kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa wa Idara ya saratani na ikiwa ni moja ya misingi na kanuni za chama pindi wanapotengeneza faida kurudisha katika jamii inayoizunguka. Akipokea vifaa tiba hivyo Dkt. Fabian A. Massaga, Mkurugenzi Mkuu wa Bugando, ameushukuru uongozi wa SACCOS, katika ngazi zote za Mkoa pamoja na wilaya ikiwemo Bugando SACCOS na kuupongeza uongozi huo kwa kuendelea kusimamia misingi na kanuni ya chama na kutanabaisha kuwa, kupitia majitoleo hayo yataenda kuhudumia wagonjwa na kuendelea kuboresha huduma za Hospitali. "Sisi kama menejimenti tumepokea na tunathamini mchango wa majitoleo katika huduma zetu za Afya na vifaa hivi vitatumika kama ilivyokusudiwa “. amesema Dkt. Massaga. Nae msimamizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Mwanza Bw. Saguda Yohana ameushukuru uongozi wa hospitali ya Bugando na wamefurahi kuona chama kinaendelea kutimiza moja ya kanuni na misingi ya chama. Bw.Richard Masunga Mwenyekiti wa chama cha Bugando SACCOS amesema chama hiki kimekuwa msaada mkubwa na kuondoa msongo wa mawazo kwa wafanyakazi wa Bugando, pale wanapopata matatizo mbalimbali. Pia amempongeza Mkurugenzi Mkuu kwa usimamamizi mzuri wa Saccos hii, akiongeza kuwa "Majitoleo haya yataenda kusaidia wauguzi wetu kwa ajili ya kuona wagonjwa katika jengo la saratani"
BUGANDO YAKABIDHIWA GARI YA KUBEBA WAGONJWA (AMBULANCE)
BUGANDO YAKABIDHIWA GARI YA KUBEBA WAGONJWA (AMBULANCE)
BUGANDO YAKABIDHIWA GARI YA KUBEBA WAGONJWA (AMBULANCE)
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula, amekabidhi gari la kubeba wagonjwa mahututi ( ambulance) kwa Hospitali ya rufaa ya kanda Bugando iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kubeba wagonjwa.
Mhe. Mabula amesema gari hilo ni sehemu ya yale yaliyotolewa na Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika juhudi za kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananachi,ikiwa ni kipaumbele cha kutoa huduma bora kwa watanzania wote.
Katika hatua nyingine Mhe. Mabula ameipongeza menejimenti ya Hospitali ya rufaa ya kanda Bugando chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian A. Massaga kutokana na kazi kubwa iliyofanyika ya kuboresha huduma na miundombinu ya utoaji wa huduma hizo pamoja na uwajibikaji wa watumishi katika kuwahudumia wananchi.
“Nampongeza sana Mkurugenzi Mkuu kwa uongozi imara, kwa sasa huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Bugando hazina tofauti na zile zinazotolewa katika nchi kubwa zilizoendelea, pia watumishi wanafanyakazi kwa kujitoa sana na hii inadhihirisha kuwa wananchi wa Kanda ya ziwa wanapata huduma stahiki. Mimi kama Mbunge wa jimbo la Nyamagana ntahakikisha nazidi kuwawakilisha vyema kwa kuhakikisha tunapata gari nyingine kwa ajili ya kubeba wagonjwa pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba mbali mbali amesema”. Mhe. Mabula
Awali akipokea gari hilo, Dkt. Massaga amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya katika sekta ya Afya kwa ujumla ikiwemo uboreshaji wa miundo mbinu na upatikanaji wa vifaa tiba ikiwemo gari hii, Pili amemshukuru Waziri wa Afya Mhe. Ummy A Mwalimu( Mb) kwa usimamizi mzuri wa wizara ya afya. Pia Amemshukuru Mhe. Stanslaus Mabula kwa ushirikiano mkubwa anaoutoa Bugando katika utekelezaji wa majukumu yake akiahidi kulitunza gari hilo.
MAFUNZO YA UONGOZI KWA WAUGUZI VIONGOZI-BUGANDO
MAFUNZO YA UONGOZI KWA WAUGUZI VIONGOZI-BUGANDO
MAFUNZO YA UONGOZI KWA WAUGUZI VIONGOZI-BUGANDO
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha Mafunzo ya Uongozi na Utawala kwa wauguzi viongozi na Wauguzi wasaidizi wa Bugando. Mafunzo Haya yamefunguliwa rasmi leo Januari 31,2024 na Mkurugenzi Mkuu wa hosptali ya Bugando Dkt.Fabian A.Massaga.
Akizungumza katika ufunguzi huu Dkt. Massaga, ameishukuru Wizara ya Afya na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ushirikiano wao wa moja kwa moja na Bugando katika kuhakikisha hospitali inaendelea kutoa huduma bora kwa kuzingatia kanuni na taratibu za Afya, pia amempongeza Mkurugenzi wa huduma za wauguzi Bugando Sr. Salome Marandu kwa usimamizi bora katika kuhakikisha wauguzi hawa wanapata mafunzo stahiki.
Aidha amewasisitiza wauguzi kutoa huduma bora, kujiendeleza kimasomo na pia kuonyesha umahili zaidi katika maeneo yao ya kazi kwa kuhudumia wagonjwa kwa huruma na upendo.
Nae Bw. Edwin Damas Mkufunzi kutoka Wizara ya Afya amempongeza Mkurugenzi Mkuu kwa kutoa Kibali na kuwezesha mafunzo haya ambayo yana mchango mkubwa katika uendeshaji wa taasisi hasa za Afya na kusema ataendelea kufanya kazi kwa karibu na kurugenzi ya uuguzi ili kuhakikisha huduma zinatolewa katika viwango vinavyostahili.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea wataalamu wa upandikizaji wa figo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa. itali ya
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea wataalamu wa upandikizaji wa figo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Katika kuendelea kuboresha huduma za Kibigwa na Bigwa Bobezi, Hospitali ya Rufaa Ya Kanda Bugando leo Desemba 5, 2023, imepokea wataalamu wa upandikizaji wa figo kutoka katika Hospitali ya Benjamin Mkapa lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wataalamu katika mpango wa upandikizaji figo na kuingia makubaliano na ushirikiano baina ya Hospitali hizi mbili katika nyanja mbalimbali za mafunzo na ubadilishanaji wa wataalamu na vifaa tiba.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameushukuru Uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kutoa wataalamu hawa na kusema ujio huu utaleta tija kubwa katika safari ya kuanzishwa kwa huduma za upandikizaji wa figo( Renal Transplant) katika Hospitali ya Bugando.
MAADHIMISHO YA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI.
MAADHIMISHO YA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeungana na Dunia kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu kwa kuendesha huduma ya uchunguzi wa kibingwa na kibingwa bobezi kwa watu wenye matatizo ya viungo vya mwili ikiwa ni pamoja na macho, mikono, miguu na masikio kwa siku mbili mfululizo bure.
Akizungumza wakati wa hitimisho la huduma hii ya uchunguzi iliyohitimishwa mapema Disemba 05, 2023, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameiasa jamii ihakikishe inawafikisha wagonjwa wenye changamoto mbalimbali zinazoweza kupelekea ulemavu kwa wataalamu ili kupata huduma za ushauri na matibabu kwa wakati ili kuwapunguzia athari ya ulemavu ukubwani.
"Hospitali ya Bugando imeboresha na inaendelea kuboresha miundo mbinu ikiwemo uboreshaji wa kituo cha huduma kwa wateja, utumiaji wa lugha ya alama na viti maalum vya wagonjwa, tunayazingatia haya ili kuhakikisha wateja wetu wote wanapata huduma sawa" amesisitiza Dkt. Massaga.
Dkt. Massaga pia ametanabaisha kuwa tatizo la ulemavu linaathiri maendeleo ya mtu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla huku ikikadiliwa kuwa takribani watu bilioni moja nukta tatu (1.3) sawa na asilimia 16% na kwa Tanzania watu wenye tatizo la ulemavu ni takribani millioni tatu nukta tatu (3.3) sawa na asilimia 9%.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mifupa, Daktari Bingwa Inyasi Akaro, ametoa wito kwa jamii, ndugu, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha matatizo yanayopelekea ulemavu yanashughulikiwa kwa wakati kwa kuwafikisha wagonjwa katika vituo vya Afya kupata huduma stahiki na kueleza kuwa katika huduma hii ya uchunguzi wamefanikiwa kuhudumia wagonjwa wenye changamoto za viungo vya mwili ikiwemo macho, masikio, mikono na miguu 160 kwa siku moja huku kati yao 80 wamepewa rufaa kwa vipimo zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga, leo Desemba 1, 2023
kurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga, leo Desemba 1, 2023 amezindua rasmi Chama cha wahudumu wa Afya katika Hospitali ya Bugando (UWAABU)
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga, leo Desemba 1, 2023 amezindua rasmi Chama cha wahudumu wa Afya katika Hospitali ya Bugando (UWAABU) na kuwaaga watumishi waliostaafu mwaka huu 2023.
Akizungumza katika tafrija hiyo Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian A. Massaga amepongeza Kurugenzi ya huduma za Uuguzi Hospitalini hapo kwa kuanzisha umoja huo ambazo utaleta chachu na tija kwa watumishi ambao ni wahudumu wa Afya
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mkuu ametoa pongezi kwa Watumishi Wastaafu Watano (5) kwa utumishi wao na kutoa huduma kwa wagonjwa kwa huruma na Upendo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga, leo Novemba 30, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga, leo Novemba 30, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga, leo Novemba 30, 2023 amepokea ugeni ya Supportive Supervision kutoka Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ambukizi Kibong’oto (KDH) ikiongozwa na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dkt. Leonard Subi, Mratibu wa MDn-TB Dkt. Happines Mvungi, mwakilishi wa hospitali, Muuguzi Sara Matoyi, mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Gabriel Mashauri.
Lengo la ugeni huu ni kujadili namna ya kuboresha huduma za kifua kikuu na kifua kikuu sugu katika Hospitali ya Bugando na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Sambamba na hayo Dkt. Massaga ameshukuru kwa ujio wa ugeni huo wa supportive supervision nakuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kupambana na tatizo la TB huku akiwataka Wataalamu wa Kitengo cha TB kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Taasisi hiyo ili kufikia malengo ya kutokomeza ugonjwa huo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Novemba 29, 2023, imepokea msaada wa portable ultrasound
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Novemba 29, 2023, imepokea msaada wa portable ultrasound yenye thamani ya shilingi milioni tano (Tshs. 5,000,000/=) kutoka kwa Watumishi wa NMB
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Novemba 29, 2023, imepokea msaada wa portable ultrasound yenye thamani ya shilingi milioni tano (Tshs. 5,000,000/=) kutoka kwa Watumishi wa NMB, ultrasound hiyo imetolewa kwa wagonjwa wa saratani katika Hospitali ya Bugando, pia itakuwa ikitumiwa na wataalamu wakati wa kutoa huduma za tiba mkoba.
Dkt. Fabian A. Massaga, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando amewashukuru NMB kwa kusema, "tukio hili limetukutanisha kwaajili ya kukuza uhusiano baina ya Bugando na NMB kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa wetu, naahidi kuendelea kukuza mashirikiano haya."
Akizungumza katika makabidhiano hayo Ndg. Hamadi Suria kwa upande wa NMB, amesema, “ Ni utaratibu wa watumishi wa NMB kujichangisha kila mwaka kwa ajili ya kurudisha fadhila kwa wateja wao hususani makundi yenye uhitaji ikiwemo wagonjwa kama ilivyofanyika”.
HOSPITALI YA BUGANDO IMEPOKEA TUZO YA HOSPITALI BORA KATIKA UTOAJI WA TAARIFA ZA UFUATILIAJI KUHUSU USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA DHIDI YA DAWA.
TUZO YA HOSPITALI BORA YA UFUATILIAJI WA VIMELEA VYA MAGONJWA DHIDI YA DAWA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepewa tuzo ya kuwa Hospitali Bora katika utoaji wa taarifa za Ufuatiliaji kuhusu usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (National AMR Surveillance Champion). Tuzo hii imekabidhiwa na Mh. Ummy Mwalimu Waziri wa Afya katika Kongamano la tatu la Kuongeza Uelewa kuhusu Usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa jijini Arusha.
Katika kongamano hili Prof. Jeremiah Seni na Prof. Stephen E. Mshana wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi ya Afya Bugando (CUHAS) wamekabidhiwa pia tuzo za vinara wa kitaifa wa mapambano ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.
Pichani Prof. Jeremiah Seni (Mwenyekiti wa Kamati ya AMR Surveillance BMC) akikabidhi tuzo ya hospitali kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian Massaga.
Naye Dkt. Fabian A. Massaga ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wa Bugando na Chuo cha Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi ya Afya (CUHAS) katika suala hili, na kuwashukuru wafanyakazi wote kwa ushiriki wao. Pia, amesisitiza zoezi hili kuwa endelevu ili taarifa hizi zichangie katika utengenezaji wa miongozo ya matibabu Hospitalini hapa.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa kushirikiana na Shirika la Global hope la nchini Marekani
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa kushirikiana na Shirika la Global hope la nchini Marekani
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa kushirikiana na Shirika la Global hope la nchini Marekani linalojihusisha na matibabu ya saratani kwa watoto wameendesha mafunzo kwa wauguzi wa magonjwa ya saratani kwa watoto lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kitabibu wa kujua viashiria,sababu, matibabu na hata matokeo baada ya mgonjwa kupata matibabu husika.
Mafunzo haya yatafanyika ndani ya siku 6 yakiongozwa na Tadala Mulemba ambae ni Msaidizi wa huduma za tiba kwa wauguzi kutokea nchini malawi pamoja na Aisha Ndege ambae ni Mkufunzi wa wauguzi kutokea nchini Uganda.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr. Salome Malandu ameushukuru uongozi wa Global hope kwa mafunzo hayo na kusema mafunzo hayo yataongeza chachu na kuboresha huduma kwa wagonjwa hasa kwa watoto wenye saratani.
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya (CUHAS-Bugando) na Askofu wa jimbo kuu la mbeya Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya (CUHAS-Bugando) na Askofu wa jimbo kuu la mbeya Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga amewaasa Wahitimu wa Chuo kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya Bugando katika mahafali ya 16 ya Chuo hicho kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili na ubinadamu bila kujali kipato na kuepuka tamaa za vyeo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt.Fabian Massaga amehudhuria misa takatifu ya mahafali ya 16 ya Chuo kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt.Fabian Massaga amehudhuria misa takatifu ya mahafali ya 16 ya Chuo kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt.Fabian Massaga amehudhuria misa takatifu ya mahafali ya 16 ya Chuo kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha zoezi la uchunguzi wa awali kwa magonjwa ya henia
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha zoezi la uchunguzi wa awali kwa magonjwa ya henia
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha zoezi la uchunguzi wa awali kwa magonjwa ya henia, Kisukari na shinikizo la damu ikiwa ni maandalizi ya kambi maalumu ya upasuaji ya ugonjwa wa henia inayotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo Novemba 12 mpaka 17.
Akizungumza katika zoezi hilo la uchunguzi Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ametoa wito kwa jamii kutumia fursa zinazotolewa bure na kusisitiza huduma hii itakuwa endelevu.
Sambamba na hayo, Mkurugenzi Mkuu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha Muswada wa Bima ya Afya kwa wote na kuwaomba Wananchi na kuwahamasisha kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ili kujiepusha na gharama kubwa za matibabu.
Kwa upande wake
Dkt. Ahmed Binde bingwa wa Upasuaji wa ugonjwa wa Henia amesema, tatizo hili linaweza kuwapata watu wa jinsia zote nakutoa wito kwa Jamii kujitokeza kufanya uchunguzi mapema na kuacha dhana potofu kuwa tatizo la ugonjwa wa Henia huwapata wanaume pekee.
Nawapongeza sana na kuwatia moyo mkafanye kazi kwa bidii huku mkifuata maadili
Nawapongeza sana na kuwatia moyo mkafanye kazi kwa bidii huku mkifuata maadili na miiko ya kazi zetu "
"Nawapongeza sana na kuwatia moyo mkafanye kazi kwa bidii huku mkifuata maadili na miiko ya kazi zetu " amesema haya Dkt. Cosmas Mbulwa Mkurugenzi wa huduma za Afya saidizi katika hafla
ya kuhitimu mafunzo ya chumba cha kuhifadhia miili( mortuary) ambapo amekabidhi vyeti kwa wahitimu 23.
Aidha Dkt.Jackson Kahima mkuu wa huduma za maabara (CPL) amewapongeza wahitimu hao na kuwaomba wakafanyie kazi yale yote waliyojifunza kwa kipindi chote cha mafunzo yao.
Hospitali ya Bugando ni Hospitali pekee inayotoa mafunzo haya kwa muda mrefu (Miezi mitatu) kwa ngazi ya cheti hapa nchini.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendelea kuunga Mkono juhudi za Serikali
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendelea kuunga Mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita katika kujenga na kuboresha mahusiano na mashirikiano ya kimataifa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendelea kuunga Mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita katika kujenga na kuboresha mahusiano na mashirikiano ya kimataifa kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali zikiwemo za huduma ya Afya, tiba na matibabu kwa ujumla wake.
Mapema leo, Oktoba 27, 2023, Hospitali kupitia Idara ya Fiziotherapia imepokea ugeni wa Wanafunzi 7 na Walimu wao wawili kutoka Chuo Kikuu cha Carroll cha nchini Marekani kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu.
Akizungumza katika mapokezi ya ugeni huu, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Bahati Wajanga akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dkt. Fabian A. Masaga amewakaribisha wageni na kushukuru ujio wao huku akibainisha kuwa kwa ujio wao Hospitali kupitia Idara ya Fisiotherapia itapiga hatua kutoka pale ilipo kwa kujifunza na kuboresha huduma zinazotolewa na Idara.
Kwa upande wa wageni wameushukuru uongozi wa Hospitali kwa kuwapokea huku wakitanabaisha kuwa kwa wanafunzi ni mara yao ya kwanza kufika Bugando lakini kwa Walimu ni mara ya pili na ya tatu kuitembelea Hospitali.
Wageni hawa kutoka Chuo Kikuu cha Carrol wanatarajia kuwepo Hospitali ya Bugando katika Idara ya Fiziotherapia kwa muda wa siku 45.
UPANDIKIZAJI WA KOO BANDIA
UPANDIKIZAJI WA KOO BANDIA
Kwa mara ya kwanza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanya huduma ya upandikizaji wa koo bandia kwa mgonjwa wa saratani ya koo ambaye anashindwa kula au kumeza chakula.
Mkuu wa kitengo cha Magonjwa ya mfumo wa chakula Dkt.David Majinge ameiasa jamii na watanzania kuwa na desturi ya kufanya uchunguzi pindi wanapohisi kupata changamoto ya kumeza chakula kwani hiyo inaweza kuwa ni dalili ya awali ya saratani ya koo la chakula.
Dkt Ahmed Binde daktari bingwa wa upasuaji na mfumo wa chakula amesema kuwa madaktari wametumia mbinu ya kuweka koo bandia ambayo imekuwa na matokeo mazuri kwa mgonjwa huyo.
"Nilipata shida ya kutokumeza chakula tangu mwezi Agosti jambo lililonipelekea kuja katika Hospitali ya Bugando nikagundulika kuwa na Saratani ya koo na njia pekee ya kupona ilikuwa ni kuwekewa koo bandia.Baada ya njia hiyo kufanyika kwasasa nimepona na ninaweza kula vizuri".Amesema Bw.Boniphace Warioba.
Bugando Mpya yenye huruma na Upendo, tumepiga hatua, tunathamini Afya yako, Kazi iendelee.
Kila Alhamis ya pili ya mwezi wa Kumi, Dunia huadhimisha siku ya Afya ya macho,
ila Alhamis ya pili ya mwezi wa Kumi, Dunia huadhimisha siku ya Afya ya macho, Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando
Kila Alhamis ya pili ya mwezi wa Kumi, Dunia huadhimisha siku ya Afya ya macho, Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando imehitimisha maadhimisho hayo kwa kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi. Maadhimisho haya yalianza kwa kutoa huduma za uchunguzi wa afya ya macho bure, utoaji wa miwani na huduma za upasuaji kwa gharama nafuu kwa muda wa siku nne.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amehitimisha zoezi hili kwa kuzungumza na wananchi waliofika kupata huduma kwa kuwahimiza kufuata kanuni za afya ili kuendelea kutunza afya za macho ikiwemo kula chakula chenye kurutubisha afya ya macho,kuacha matumizi ya dawa na uvaaji miwani bila ushauri wa wataalamu pamoja na kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yenye madhara katika macho ikiwemo kisukari na shinikizo la damu. Dkt. Massaga amesema “Penda macho yako Mahala pa Kazi”, Kauli mbiu ya mwaka huu inatuhimiza wote tuwe makini na afya ya macho yetu tuwapo mahala pa kazi.
Kazi ni uhai, hivyo basi kumekuwa na kujisahau kwa baadhi ya watumishi Kwenda kupima afya ya macho hadi pale wanapopata changamoto. Zipo kazi ambazo moja kwa moja ni hatarishi kwa afya ya macho hivyo wakati mkiwa mnazifanya ni lazima muwe mmevaa vifaa maalum kwa ajili ya kukinga macho yenu, mfano, Wachomeleaji wa vifaa vya chuma (welders), Wafanyakazi wa kwenye viwanda vya madawa na vinywaji, madawa hayo huwa ni hatari kwa afya ya macho endapo yataingia machoni moja kwa moja, kwa ujumla kazi zote za viwandani, maofisini, mashambani, kazi za nje zina hatari ya kuathiri afya ya macho yetu hivyo tujitahidi kuzingatia kanuni na taratibu za kulinda afya ya macho yetu makazini.” Amesema Dkt. Massaga Sambamba na utoaji huduma kwa wananchi,
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga amehitimisha mafunzo kwa wauguzi wa chumba cha upasuaji leo Oktoba 6, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga amehitimisha mafunzo kwa wauguzi wa chumba cha upasuaji leo Oktoba 6, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Dkt Fabian A. Massaga amehitimisha mafunzo kwa wauguzi wa chumba cha upasuaji leo Oktoba 6, 2023
ambapo mafunzo haya yamefanyika kwa muda wa wiki mbili yakitolewa na wakufunzi kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt . Massaga amewapongeza wakufunzi kwa kazi nzuri wanazofanya na kuongeza kuwa mafunzo haya yalilenga katika maandalizi wakati wa upasuaji, uandaaji wa vifaa vya upasuaji, uandaaji wa nguo na gozi za kufanyia upasuaji katika chumba cha kutakasia( Central Sterilization Service Department) pamoja na maandalizi ya mgonjwa kabla na baada ya upasuaji(Pre and Post operation preparation)
Mafunzo haya yatakuwa msaada mkubwa kwa Taasisi na pia yataleta mabadiliko makubwa katika chumba cha upasuaji, amesema Dkt.Massaga.
Kwa upande wake Sr.Salome Kassanga muuguzi mbobezi katika chumba cha upasuaji na mkufunzi kutoka baraza la uuguzi na ukunga Tanzania, amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Hospitali ya Bugando katika utoaji wa huduma za afya ikiwemo upasuaji.
Sr.Kassanga ameongeza kwa kusema kuwa Pamoja na mapungufu machache tuliyoyaona, mafunzo haya yataenda kuondoa changamoto nyingi na kushauri mpango wa kufufua vyuo vinavyotoa mafunzo ya huduma za uuguzi katika vyumba vya upasuaji kwani mpango huu unaweza kuwa suluhisho la changamoto hizi
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha semina iliyohudhuriwa na zaidi ya wanafunzi 500
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha semina iliyohudhuriwa na zaidi ya wanafunzi 500 wa shule za msingi jijini Mwanza
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha semina iliyohudhuriwa na zaidi ya wanafunzi 500 wa shule za msingi jijini Mwanza inayohusu namna ya kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kuchangia matatizo ya afya ya akili.
Akizungumza katika Semina hiyo
Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi, Mwalimu Maenda M Chambuko amewataka watoto kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kusababisha matatizo ya afya akili ikiwemo ulevi na matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha Daktari Bingwa wa magonjwa ya Afya ya Akili na Mkuu wa Idara hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, DKt.Catherine Magwiza amesema Hospitali ya Bugando inahudumia wastani wa watu 3,000 kwa mwaka wenye matatizo ya afya ya akili na wagonjwa 500 kati yao huhitaji uangalizi maalumu jambo linalosababisha wagonjwa hao kuwekwa katika uangalizi maalum wa wataalam wa hospitali hiyo.
Hata hivyo Dkt.Catherine ametoa wito kwa jamii kuwa waonapo dalili au viashiria vya magonjwa ya Akili wafike hospitali ili wapate huduma hiyo na kuomba jamii kutowanyanyapaa au kuwatenga wagonjwa wa afya ya akili kwani kufanya hivyo kutawafanya wagonjwa hao wakate tamaa ya kwenda Hospitali na kupata matibabu kwa kuhofia jamii itakavyowachulia.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando umefanya makabidhiano ya mifuko 35 ya simenti
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando umefanya makabidhiano ya mifuko 35 ya simenti pamoja na madirisha 10 ya aluminiamu kwa uongozi wa kijiji cha Mapilinga
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando umefanya makabidhiano ya mifuko 35 ya simenti pamoja na madirisha 10 ya aluminiamu kwa uongozi wa kijiji cha Mapilinga lengo likiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii na kudumisha ushirikiano baina ya Bugando na jamii ili kufanikisha ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho.
Fr.Cornelius H. Ntunguweli Mwanasheria wa Hospitali akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bugando Dkt.Fabian A. Massaga ameomba uongozi wa kijiji hicho kutumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa ili kukamilisha ujenzi wa zahanati ambayo itakua msaada mkubwa kwa jamii inayozunguka eneo hilo.
Aidha Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapilinga Bw.Sospeter Semeni ameushukuru uongozi wa Hospitali kwa ushirikiano mkubwa wanaouonyesha na kusema vifaa hivyo vitasaidia sehemu kubwa ya ujenzi wa zahanati hiyo pia ameuomba uongozi wa Hospitali usichoke kutoa msaada ili kufanikisha ujenzi wa Zahanati.
Ungana nasi kila siku ya jumanne na ijumaa ya kila wiki katika mazoezi ya kuimarisha Afya ya miili yetu. Bugando Medical centre tunajali Afya yako.
Ungana nasi kila siku ya jumanne na ijumaa ya kila wiki katika mazoezi ya kuimarisha Afya ya miili yetu. Bugando Medical centre tunajali Afya yako.
Ungana nasi kila siku ya jumanne na ijumaa ya kila wiki katika mazoezi ya kuimarisha Afya ya miili yetu. Bugando Medical centre tunajali Afya yako.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameendesha kikao
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameendesha kikao kazi cha madaktari bingwa na bingwa bobezi wa Hospitali hiyo lengo likiwa ni kuboresha na kujadili mipango ya Taasisi katika kukuza huduma za kibigwa na bigwa bobezi. Amewakumbusha madaktari bingwa na bingwa bobezi kuzidi kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi ya taaluma zao na kwa ubobezi katika maeneo husika na kutoa huduma kwa huruma na upendo kwa wagonjwa wote kwa wakati sahihi na Kuzingatia kauli nzuri kwa wagonjwa. Dkt. Massaga amewapongeza madaktari hao kwa kazi nzuri wanayoifanya na ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika Taasisi .”Sisi kama viongozi tunatambua na tunathamini mchango wenu katika Taasisi na tumetenga bajeti kwa ajili ya kuendeleza madaktari wetu kitaaluma” Hata hivyo, Dkt.Massaga amewataka Wakurugenzi, wakuu wa idara na madaktari kwa ujumla kufanya kazi kwa ushirikiano,uaminifu na uadilifu katika maeneo yao ya kazi ili kuboresha huduma za kibingwa na bigwa bobezi katika Taasisi.
TATHIMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO KATIKA MIKOA YA GEITA, SHINYANGA NA KAGERA.
TATHIMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO KATIKA MIKOA YA GEITA, SHINYANGA NA KAGERA.
TATHIMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO KATIKA MIKOA YA GEITA, SHINYANGA NA KAGERA.
Kutoka Mkoani Geita..
Mhe. Helman Matemu Katibu Tawala Mkoa wa Geita akimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita amefungua kikao kazi cha tathimini ya Afya ya uzazi ya mama na mtoto, Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika mikoa ya Geita, Shinyanga na Kagera.
Mhe. Matemu pamoja na mambo mengine amewaelekeza wadau kuwa na mikakati mahususi ya kuboresha huduma za Afya ya uzazi na mtoto
"Ninawaelekeza muainishe mikakati itakayolenga kuboresha huduma za uzazi kabla ya kujifungua, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua hakikisheni kuwa miundombinu na vifaa tiba kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma ya mama na mtoto vinaboreshwa, aidha watumishi wajengewe uwezo na kupewa motisha ili kuwajengea hamasa ya kujituma zaidi waelimisheni watumishi kujiepusha na lugha mbaya na vitendo vya rushwa kwa wajawazito na ndugu wanapofika katika vituo." Amesema Mhe. Temu
Akiongea katika kikao icho Mwenyekiti wa kamati ya Afya ya uzazi ya mama na mtoto Kanda ya Ziwa ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga amesema lengo la kikao kazi hiki ni kujadili na kutathimini huduma za Afya ya uzazi na mtoto, kubadilishana na kupeana uzoefu wa namna na mbinu za kuboresha huduma na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga na mwisho kutoka na mikakati ya kuboresha na kupunguza vifo vitokanvyo na uzazi.
Sambamba na hayo Dkt. Massaga ameishukuru Serikali kupitia Wizara zake kwa kuboresha huduma za Afya
"Nichukue nafasi hii kuishukuru Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kuandaa kikao hiki kikubwa chenye kikao mbiu "Uongozi na uwajibikaji ni chachu katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga".
UZINDUZI WA BUGANDO FUN RUN 2023.
Katika kuadhimisha miaka 20 ya Chuo kikuu cha kikatoliki cha Sayansi za Afya na Tiba Shirikishi (CUHAS)
UZINDUZI WA BUGANDO FUN RUN 2023.
Katika kuadhimisha miaka 20 ya Chuo kikuu cha kikatoliki cha Sayansi za Afya na Tiba Shirikishi (CUHAS), Taasisi za Bugando zimeungana kwa pamoja kuanzisha mbio za hisani zenye lengo la kuchangia wanafunzi wanaoshindwa kulipa pesa ya kugharamia masomo hivyo kupelekea kukwama kuendelea na masomo yao. Mbio hizi za hisani zimezinduliwa na Mhe. Stanslaus Mabula mbunge wa jimbo la Nyamagana ambae ameiomba jamii kuwa na utaratibu wa kuchangia katika masuala ya elimu, “Nimefurahishwa na mbio hizi za hisani ambazo zimebeba kauli mbiu inayosema“Kimbia kwa ajili ya Wanafunzi Wahitaji”
Sisi kama Jamii tunawajibu wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji wa ada katika vyuo vyetu, natumia nafasi hii kuwaalika wadau mbalimbali kujenga utamaduni wa kuchangia elimu, mimi na ofisi yangu tutachangia na kushiriki katika mbio hizi hapo tarehe 5, novemba 2023.
Amesema Mhe. Mabula.
Naibu makamu Mkuu wa Chuo cha CUHAS- Profesa Peter Rambau ameeleza kwa upana wa idadi ya wanafunzi wanaopata changamoto ya kukosa mahitaji ikiwemo pesa za kugharamia masomo.
“Takwimu zinaonesha kwa sasa tuna wanafunzi takribani 152 ambao wanapata changamoto mbalimbali za mahitaji na kukosa pesa ya ada hivyo kupelekea wanafunzi wengi kuacha Chuo au kuahirisha masomo yao.
Kipekee, tunapenda kupongeza juhudi za serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, mikopo ya elimu ya juu kupitia mfuko wa SAMIA SCHOLARSHIP, Chama cha wanafunzi CUHASSO, TANNA, TNMC, kwa juhudi kubwa za uchangiaji wanafunzi wanaokumbana na changamoto za malipo ya ada” Amesema Prof.Ramba
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bugando Dkt. Fabian A Massaga amesema, “Mbio hizi za hisani ni mwanzo wa maandalizi ya mbio za BUGANDO MARATHON"
Idara ya Saratani kutoka Hospitali Rufaa ya Kanda Bugando
Idara ya Saratani kutoka Hospitali Rufaa ya Kanda Bugando imeadhimisha siku ya uelewa wa magonjwa ya Saratani duniani
Idara ya Saratani kutoka Hospitali Rufaa ya Kanda Bugando imeadhimisha siku ya uelewa wa magonjwa ya Saratani duniani amabayo hufanyika kila mwaka tarehe 15 Septemba ikiwa na kaulimbiu “KILA MTOTO MWENYE SARATANI ANASTAHILI FURSA YA TIBA” Madhimisho hayo yamefanyika kwa kutoa elimu kwa magonjwa ya saratani, Uchangiaji damu pamoja na uchunguzi wa magonjwa ya macho katika viwanja vya Hospitali ya wilaya Magu.
Aidha daktari bingwa wa magonjwa ya saratani ya watoto Dkt Heronima Kashaigili amewashukuru wanachi kwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo na kufanya uchunguzi wa magonjwa ya saratani na kuwaomba wananchi wote kuwa mabalozi kwa wengine kwani Saratani ikigundulika mapema inatibika.
Hata hivyo, Hospitali ya Bugando inafanya juhudi kubwa kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kufanya tiba mkoba(Outreach) katika mkoa wa Mwanza na viunga vyake pamoja na kufanya mazoezi ambapo mazoezi haya huwahusisha watumishi wote wa Hospitali ya Bugando
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando wakiongozwa na mkurugenzi mkuu Dkt Fabian .A. Massaga wameshiriki katika mazoezi ya viungo ya pamoja yaliyo fanyika leo
Septemba 12 ,2023 katika viwanja vya maegesho ya magari.
Mazoezi haya hufanyika mara mbili kwa wiki kwa siku za Jumanne na Ijumaa ikiwa na lengo la kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza.
UZALISHAJI MAJI TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO.
UZALISHAJI MAJI TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO.
UZALISHAJI MAJI TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO. Idara ya famasi imefanya maboresho makubwa kupitia kitengo cha uzalishaji maji tiba, ( Infusion Unit) Akizungumza katika makabidhiano Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian Massaga amewapongeza idara ya Famasi kwa Jitahida kubwa wanazofanya ili kuongeza uzalishaji na kuipunguzia Hospitali gharama za kuagiza maji tiba nje kwa gharama kubwa, Dkt. Massaga ametoa wito kwa viongozi na wanaidara kwa ujumla kutunza mitambo mipya pamoja na sehemu zilizofanyiwa ukarabati bila kusahau kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya nchi.
Dkt. Massaga ameeleza adhima ya taasisi hapo baadae kuwa na kiwanda kikubwa cha uzalishaji maji tiba kwa kutumia teknolojia mpya “ sisi kama Hospitali ya Rufaa ya Kanda, tunaowajibu wa kuhakikisha wagonjwa wanapata tiba stahiki na kwa wakati pia kuokoa gharama za matibabu kwa wananchi, kitengo hiki cha maji tiba kinazalisha kwa asilimia 90, ya mahitaji ya maji tiba ndani ya hospitali, kwakuwa tunaendelea na maboresho mbali mbali niombe wadau kushirikiana nasi tuweze kutumia teknolojia mpya ili kuongeza uzalishaji zaidi “.
Pia Dkt. Massaga ameishukuru Serikali kupitia wizara ya Afya kwa kutupa kibali cha kufanya ubunifu wenye tija katika uboreshaji wa huduma za afya katika taasisi zetu, kwani ubunifu huu utaipunguzia serikali mzigo wa kununua dawa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi, lakini pia itapunguza gharama za matibabu kwa mwananchi.
ZOEZI LA UZINDUZI WA MAABARA YA UCHUGUZI WA MAGONJWA YA BINADAMU
UZINDUZI WA MAABARA YA UCHUGUZI WA MAGONJWA YA BINADAMU
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando Dkt.Fabian A. Massaga ameongoza zoezi la uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi wa magonjwa ya binadamu (vivimbe, saratani na sababu za vifo (histopatholojia) ambao umefanyika mapema leo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.Lengo la uzinduzi wa Maabara hiyo ya uchunguzi ni kuhakikisha huduma hii inapatikana katika Hospitali nyingine na majibu ya vipimo yanatoka haraka ndani ya wiki moja ili kuwasaidia na kuwarahisishia wagonjwa katika kupata huduma za kibingwa na bingwa bobezi
Aidha Dkt Massaga amewaomba watumishi wa Histopatholojia kuendelea kuwa wabunifu na kuzidi kutoa na kufanya huduma kwa uharaka na majibu sahihi.
Naye Dkt Jackson Kahima mkuu wa Huduma za Maabara( CPL ) ameshukuru uongozi wa Hospitali kwa kujitoa katika ukarabati wa maabara ya Histopatholojia kwani ukarabati huo utazidisha upatikanaji wa majibu kwa wakati.
Aidha Dkt Fabian A. Massaga ametembelea na kukagua mradi wa warehouse na Oxygen plant ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni lakini pia katika ukaguzi huo amefanikiwa kutembelea na kuzindua mradi wa Ultrasound ambao utahudumia akina Mama wajawazito na wazee ili kupunguza msongamano wa wateja na yote haya ni katika kutimiza malengo ya serikali ya kuwajali kina mama wajawazito pamoja na wazee.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando Dkt. Fabiani A. Massaga leo Septemba 1, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando Dkt. Fabiani A. Massaga leo Septemba 1, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando Dkt. Fabiani A. Massaga leo Septemba 1, 2023 amehitimisha mafunzo ya lugha ya alama kwa Watumishi 15 ambayo yametolewa kwa wiki tatu mfululizo kutoka Hospitali ya Bugando wakiwemo Wataalam kutoka kitengo cha usikivu pamoja na Watumishi kutoka Chuo cha Afya cha MWACHAS (Mwanza college of health allied science), akizungumza katika zoezi hilo Dkt.Massaga amefurahishwa na Watumishi hao kuwa na utayari wa kukubali kujifunza lugha ya alama ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa Taasisi na Taifa kwa ujumla.
Lengo la mafunzo haya ni kurahisisha mawasiliano baina ya Wataalam na Wagonjwa wenye changamoto za usikivu ili kuleta uelewano katika kutoa huduma na kuifanya hospitali ya Bugando kuwa kituo cha kutolea mafunzo ya lugha ya alama kwa Taasisi nyingine ili kuwasaidia wagonjwa wenye tatizo la usikivu.
Sambamba na hilo Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabiani A. Massaga amewapongeza Wahitimu na kuwashukuru Wakufunzi kutoka Chuo cha Sauti Tabora na shule ya msingi Kirumba Jijini Mwanza kwa jitihada walizofanya katika kufundisha na kuhakikisha wanafunzi wao wanaelewa.
Leo Agosti 29, 2023 Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanya makabidhiano ya Transformer
Leo Agosti 29, 2023 Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanya makabidhiano ya Transformer na (AFRICAB)
Leo Agosti 29, 2023 Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanya makabidhiano ya Transformer na (AFRICAB), Taasisi ya uzalishaji wa vifaa vya umeme viwandani na majumbani, chini ya Mhandisi Hamis Rajabu Said ambapo lengo la mradi huu ni kubadili mfumo wa umeme wa Trasnformer 500KVA kwenda Transformer 1MVA, hii ni katika kukabiliana na
mahitaji makubwa ya umeme yaliopo na yatakayokuwepo ndani ya Taasisi ikiwemo kuongezeka kwa mashine na majengo mapya katika Taasisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ametoa shukrani za dhati kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kutupatia transformer na kuwaomba Viongozi wa Hospitali, Wakuu wa Idara na watumishi kwa ujumla kulinda na kuthamini vifaa vya Taasisi kwa masilahi ya Taasisi na jamii .
Naye mhandisi Hamis Rajab, ametoa shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian A. Massaga, Idara ya uhandisi na Hospitali kwa ujumla kwa ushirikiano walioonyesha wa hali na mali katika mradi huu tangu mwanzo hadi tamati.
Ikiwa katika maandalizi ya kuelekea siku ya Bugando (Bugando Day)
Ikiwa katika maandalizi ya kuelekea siku ya Bugando (Bugando Day) ambayo hufanyika kila mwaka Novemba 3
Ikiwa katika maandalizi ya kuelekea siku ya Bugando (Bugando Day) ambayo hufanyika kila mwaka Novemba 3, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Agosti 29, 2023 imetembelea shule msingi Mkuyuni iliyopo Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza. Lengo likiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii na kutoa huduma za upimaji na uchunguzi wa magonjwa homa ya ini, meno, macho na shinikizo la damu bure kwa Wanafunzi na Walimu wa shule ya msingi Mkuyuni C. Uongozi washule hiyo umepongeza na kushukuru Uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa kuridhia kutoa huduma hizo bure.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inawakaribisha watumishi wote
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inawakaribisha watumishi wote
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inawakaribisha watumishi wote katika mazoezi kila siku ya Jumanne na Ijumaa saa 12:45 mpaka saa 1:20 Asubuhi katika eneo la maegesho ya magari ya watumishi. Wote mnakaribishwa.
KAMBI YA UPASUAJI SANIFU- (PLASTIC SURGERY)
HOSPITALI YA BUGANDO
KAMBI YA UPASUAJI SANIFU- (PLASTIC SURGERY) BUGANDO
Timu ya madaktari Bingwa Bobezi, Bingwa na madaktari walio mafunzoni kutoka Chuo kikuu cha Duke kwa kushirikiana na Taasisi mbali mbali za Afya za nchini Marekani wanaendesha kambi ya matibabu, upasuaji pamoja na mafunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa muda wa wiki moja.
Timu hii inashirikiana na kurugenzi ya upasuaji kupitia idara ya upasuaji sanifu, pua , koo na masikio, katika kutoa huduma za matibabu, na upasuaji kwa wagonjwa pamoja na mafunzo kwa madaktari.
Akiwakaribisha wageni hao, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Dkt. Fabian A Massaga, amesema hospitali ipo tayari kudumisha mahusiano mazuri kati ya taasisi hizi katika maeneo mbali mbali ya hospitali pia na kuhimiza kambi hizi ziwe endelevu kwa maana zinatija katika uboreshaji wa Huduma.
Naye kiongozi wa timu hiyo Dkt. P Manor Abraham ambaye ni daktari Bingwa wa upasuaji sanifu ametoa pongezi kwa uongozi wa Hospitali kwa maboresho makubwa yaliyofanyika ikiwemo kuwa na kitengo cha mtaalamu wa matamshi
( Speech therapist), uwepo wa vyumba vizuri vya upasuaji, mashine kubwa za radiolojia pamoja na mazingira ya Hospitali kwa ujumla.
Pamoja na ujio wa madaktari bingwa hawa, Hospitali ya Bugando kwa muda mrefu imekuwa na ushirikiano mzuri na Chuo kikuu cha Duke kupitia idara ya Saratani katika upande wa tafiti za magonjwa ya Saratani.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Desk and Chair Foundation Bw. Sibtain Meghjee
Mkurugenzi wa Taasisi ya Desk and Chair Foundation Bw. Sibtain Meghjee amekabidhi viti vya magurudumu kumi (wheel chair) na cherehani tano
Mkurugenzi wa Taasisi ya Desk and Chair Foundation Bw. Sibtain Meghjee amekabidhi viti vya magurudumu kumi (wheel chair) na cherehani tano kwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwaajili ya kuboresha huduma kwa wagonjwa hasa wale wenye uhitaji.
Aidha viti hivi vya magurudumu vimekabidhiwa ikiwa ni katika kuadhimisha miaka ishirini toka Taasisi hiyo kuanzishwa kwake. Akimuwakilisha Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Bahati Wajanga Mkurugenzi wa huduma za tiba ameushukuru Uongozi wa Taasisis ya Desk and Chair Foundation kwa majitoleo hayo ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa na wenye uhitaji.
Pia ameomba ushirikiano uliopo wa muda mrefu baina ya pande zote mbili uzidi kuendelea.
Kamati ya Fedha na Mipango ya Hospitali ya Bugando
Kamati ya Fedha na Mipango ya Hospitali ya Bugando ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhashimu Baba Askofu Beatus Kinyaiya wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma
Kamati ya Fedha na Mipango ya Hospitali ya Bugando ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhashimu Baba Askofu Beatus Kinyaiya wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma pamoja na Katibu wa kamati hiyo Dkt. Fabian A.Massaga ambaye ndiye Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wamepata fursa ya kutembelea geti la kuingilia magari baada ya kufanyiwa maboresho pamoja na kukagua ujenzi wa jengo la Bugando hoteli.
Mradi wa ujenzi wa Bugando Hoteli unategemea kukamilika Disemba mwaka huu, ambapo ujenzi wa hoteli hii umefikia asilimia 45% na utakua na msaada mkubwa kwa wagonjwa pamoja na wageni wa ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo Muhashamu Baba Askofu Beatus Kinyaiya ametoa pongezi nyingi juu ya maendeleo ya mradi huu na kuomba ujenzi huu umalizike salama.
Aidha MkurugenzI Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameishukuru Kamati ya fedha na mipango kwa kuweza kutembelea mradi huo na kuahidi kuusimamia vyema ili ujenzi wa Bugando Hoteli umalizike kwa wakati.
UGENI WA WATAALAMU NA VIFAA TIBA.
UGENI WA WATAALAMU NA VIFAA TIBA.
UGENI WA WATAALAMU NA VIFAA TIBA.
Mkuu wa Huduma za ufundi wa vifaa na vifaa tiba kutoka wizara ya afya Mhandisi Saniva Haule ameambatana na mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI) na Mhandisi Anna Worm kutoka Shirika la Kimataifa la UNICEF, Wametembelea karakana ya Vifaa na vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa Lengo la kujifunza na kufanya tathimini ya kuboresha mashirikiano katika uratibu wa utengenezaji vifaa tiba katika karakana za Hospitali za Rufaa za kanda Na vituo vya Afya katika ngazi za msingi. Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A Massaga ameeleza namna Hospitali inavyotunza na kukarabati vifaa tiba kwa kupitia idara ya uhandisi Pia ameeleza Hospitali inatazamia kutoa mafunzo kwa ngazi ya cheti na stashahada ya uhandisi wa vifaa tiba. Nae mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la UNICEF Mhandisi Anna worm amesema Shirika la UNICEF linalenga kuboresha Huduma za vifaa tiba sio tu vinavyotumika kutoa Huduma za mama na mtoto ila vifaa tiba vinavyolenga kutoa Huduma kwa watu wote.
UBORESHWAJI WA MATIBABU YA SARATANI KWA WATOTO
UBORESHWAJI WA MATIBABU YA SARATANI KWA WATOTO
UBORESHWAJI WA MATIBABU YA SARATANI KWA WATOTO.
Shirika la Global hope kutoka nchini marekani linalojihusisha Na matibabu ya Saratani za watoto limetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa lengo la Kuimarisha matibabu ya Saratani kwa watoto. Ugeni huu umeongozwa na Dkt. Anne Akullo Mkurugenzi msaidizi , Huduma za Tiba katika Shirika la Global hope kanda,pamoja na viongozi wengine wa shirika hilo.
Pia amefurahishwa na jitihada zinazofanyika latika Hospitali ya Bugando katika uimarishaji na upatikanaji wa huduma za saratani, ikiwemo uwepo wa jengo kubwa linalotoa matibabu jumuishi , uwepo wa vifaa tiba, mashine za miozi na wataalamu waliobobea kutoa huduma hizo.
Sambamba na hayo, Dkt. Fabian Massaga Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando amewashukuru viongozi wa Global hope kwa kuweza kuanzisha mashirikiano hayo yenye tija katika kutoa matibabu ya Saratani kwa watoto, pia ameahidi kuendeleza umoja huu katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma stahiki kwa wagonjwa.
Katika kuboresha Huduma za Upasuaji za kibingwa na kibingwa bobezi
Katika kuboresha Huduma za Upasuaji za kibingwa na kibingwa bobezi
Katika kuboresha Huduma za Upasuaji za kibingwa na kibingwa bobezi, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian A. Massaga imezindua rasmi chumba cha Upasuaji ambacho kitakuwa maalum kwaajili ya huduma za Upasuaji wa uzazi na kizazi. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu amesisitiza utunzaji wa vifaa vyote vinavyopokelewa nakutumiwa kwaajili ya huduma za Upasuaji.
KIKAO KAZI KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI BUGANDO.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt. Fabian A. Massaga ameendesha kikao kazi kwa watumishi wa Kliniki ya madaktari bingwa na bingwa bobezi (Bugando Specialized Polyclinic) inayopatikana mtaa wa Nera jijini Mwanza.
KIKAO KAZI KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA NA BINGWA BOBEZI BUGANDO.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt. Fabian A. Massaga ameendesha kikao kazi kwa watumishi wa Kliniki ya madaktari bingwa na bingwa bobezi (Bugando Specialized Polyclinic) inayopatikana mtaa wa Nera jijini Mwanza.
Kikao hiki kimelenga kufanya maboresho zaidi ili kuendeleza kutoa huduma stahiki na zenye ubora wa hali ya juu kwa wagonjwa.
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Massaga amewapongeza watumishi kwa huduma nzuri wanazozitoa , pia amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kuboresha mazingira ya huduma kwa wagonjwa wanaofika hapo bila kusahau kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na miongozo ya Taasisi.
Pamoja na hayo Meneja wa Kliniki hii
Dkt. Samson Kichiba ametaja huduma mbali zinazotolewa hapa ikiwemo huduma za ushauri zinazotolewa na madaktari bingwa na bingwa bobezi, Huduma za dawa ( pharmacy), na huduma za vipimo za Maabara na radiolojia kama ultra sound na kwa sasa huduma za matibabu ya meno na viuongo tiba ( physiotherapy).
Kliniki hii ya madaktari bingwa na bingwa bobezi ipo wazi kila siku ya Jumatatu mpaka Jumapili kuzia Saa moja kamili Asubuhi (1:00), Mpaka saa Moja na nusu Jioni (1:30)
Ugeni kutoka kwa Padri Brian Musoke pamoja na wazazi kutoka parokia mbalimbali za jimbo kuu la Mwanza
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea ugeni kutoka kwa Padri Fabian Musoke pamoja na wazazi kutoka parokia mbalimbali za jimbo kuu la Mwanza
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea ugeni kutoka kwa Padri Brian Musoke pamoja na wazazi kutoka parokia mbalimbali za jimbo kuu la Mwanza wakiwa na lengo la kutoa msaada kwa watoto wenye uhitaji katika Hospitali ya Bugando.
Hata hivyo Padri Brain Musoke ameelezea furaha yake kwa kikundi hicho kuweza kufikia lengo kubwa la kuweza kuwafikia watoto wenye uhitaji huo.
Aidha Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt.Fabian Massaga amemshukuru Padri Brian kwa majitoleo hayo kwani ni msaada mkubwa kwa watoto wenye uhitaji katika Hospitali.
Uzinduzi Rasmi wa Mradi wa PRESHA
Uzinduzi Rasmi wa Mradi wa PRESHA
PIMA PRESHA ZUIA KIFAFA CHA MIMBA.
Chuo kikuu cha kikatoliki cha Sayansi za Afya Shirikishi (CUHAS-BUGANDO) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Chuo kikuu cha Oslo ( Norway), Chuo kikuu cha Utrecht (Uholanzi) na Baraza la utafiti la Nchini Norway wamezindua Rasmi mradi wa “PRESHA “ wa kuzuia kifafa cha mimba kwa wakina mama wajawazito katika mikoa ya Kanda ya ziwa.
Mradi huu umezinduliwa rasmi na Dkt. Pima Sebastian Mganga mkuu wa wilaya ya Nyamagana ( Akimuwakilisha Mganga Mkuu wa Mko wa Mwanza), Dkt. Pima ameeleza jinsi gani serikali ilivyotayari kishirikiana na wadau kupunguza vifo vya mama na mtoto na vinayotokana na sababu mbali mbali ikiwemo presha,
Akitoa wasilisho lake katika uzinduzi huu, Dkt. Richard Kiritha ( Daktari Bingwa wa Magonjwa ya uzazi na kina mama-Bugando) ambae pia ni muasisi wa mradi amesema “ Tumelenga kupunguza vifo vya mama na mtoto haswa vinavyotokana na kifafa cha mimba kwanza kwa kufanya upimaji Wa mara kwa mara kwa wajawazito na kugundua mapema kama kuna viashiria vya kifafa cha mimba na kuendelea kuzuia kwa kutoa matibabu stahiki na kuwafatilia kwa ukaribu wajawazito wenye changamoto hii, Pili kuwezesha ( capacity building) watoa Huduma katika Hospitali za wilaya na vituo vya Afya ili kutambua viashiria vya tatizo hili na kuwapa rufaa mapema na kufika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa matibabu zaidi.” Amesema Dkt. Kiritha Akihitimisha hafla ya uzinduzi wa mradi huu,
Dkt. Fabian Massaga ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na Mwenyekiti wa Afya ya uzazi na mtoto Kanda ya ziwa, amewashukuru wadau walioona umuhimu wa changamoto ya kina mama wajawazito na kuja na mradi wa kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Tuugane kwa pamoja katika kuimarisha Afya ya Viungo vya Mwili na kutokomeza Magonjwa yasioambukiza.
Tuugane kwa pamoja katika kuimarisha Afya ya Viungo vya Mwili na kutokomeza Magonjwa yasioambukiza.
Tuugane kwa pamoja katika kuimarisha Afya ya Viungo vya Mwili
na kutokomeza Magonjwa yasioambukiza.
Wataalamu wa ugonjwa wa Himofilia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili
Wataalamu wa ugonjwa wa Himofilia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili leo,Julai 4, 2023 wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Wataalamu wa ugonjwa wa Himofilia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili leo,Julai 4, 2023 wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando lengo hasa likiwa ni kufuatilia na kufanya tathimini ya wagonjwa wa Himofilia na kuwajengea uwezo wa kujihudumia kabla ya kufika katika vituo vya afya, kuelimisha wataalamu wa afya kuhusu wagonjwa wenye tatizo hilo na kubaini changamoto wanazokumbana nazo wagonjwa hao.
Akizungumza na baadhi ya wanachama wa magonjwa ya Himofilia kanda ya ziwa Dkt. Stella Rwezaula ambae ni Daktari bingwa wa magonjwa ya damu Muhimbili na Raisi wa chama cha magonjwa ya Himofilia Tanzania amewaomba wagonjwa wa Himofilia kuwa mabalozi kwa wagonjwa wengine na jamii kwa ujumla kama kauli mbiu inavyosema, “ Uvujaji damu, ulemavu na vifo vitokanavyo na haemophilia sasa basi pima sasa ujue hali yako”.
Aidha Daktari bingwa wa magonjwa ya damu (Himofilia) Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dkt.Tecla Mtobesya , ameshukuru ujio wa wageni hao na kusema ujio huu umeonesha ushirikiano mkubwa baina ya Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando na Muhimbili lakini pia umeongeza chachu na uelewa mkubwa kwa wagonjwa na wataalamu kwa ujumla juu ya ugonjwa huo.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala ( Akimuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makala) amekabidhi hundi ya shilingi millioni tano
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala ( Akimuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makala) amekabidhi hundi ya shilingi millioni tano
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala ( Akimuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makala) amekabidhi hundi ya shilingi millioni tano (5,000,000/=) fedha zilizotolewa na Kampuni ya Transec Lake Victoria Marathon, kwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ili kusaidia matibabu ya watoto wenye Saratani kupitia mbio za marathon zilizofanyika jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A Massaga ameushukuru uongozi wa Transec Lake Victoria marathon kwanza kwa kuandaa mbio hizi ikiwa ni sehemu ya kuimarisha afya kwa njia ya mazoezi, pili kwa kuona umuhimu Wa kusaidia matibabu kwa watoto weye Saratani, “ Nimefarijika na nipende kuwa Shukuru kwa kuona umuhimu wa mchango huu kwa watoto wenye Changamoto ya Saratani, sisi tumepokea mchango huu na utatumika ipasavyo”.
Sambamba na hayo Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando inaendelea kutimiza hazima ya kutokomeza magonjwa yasiyoambukizi na Kuimarisha afya kupitia ufanyaji wa Mazoezi ya mwili kwa kuweka utaratibu wa kila siku ya ijumaa kabla ya muda wa kazi, watumishi wote wanakutana pamoja na kufanya Mazoezi.
Katika kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza
Katika kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Katika kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameanzisha utaratibu wa kufanya mazoezi ya viungo vya mwili ambapo mazoezi hayo ni endelevu yatakua yakifanyika kila Ijumaa kwa watumishi wote wa Hospitali.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata fursa ya kutembelewa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata fursa ya kutembelewa na Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya magonjwa ambukizi-Kibong’oto
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepata fursa ya kutembelewa na Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya magonjwa ambukizi-Kibong’oto ili kujadili maendeleo, utendaji kazi na changamoto katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa Kifua kikuu sugu (MDR-TB).
Sambamba na majadiliano hayo Mkurugenzi wa Hospitali ya Kibong’oto Dkt. Leonard Subi ametoa msaada wa kijamii kwa wagonjwa wenye TB sugu (MDR-TB) waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Bugando, Dkt. Bahati Wajanga ( Mkurugenzi wa Huduma za Tiba) ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Kibong’oto kwa jitihada kubwa wanazozifanya kupambana na magonjwa ambukizi nchini Tanzania haswa katika ufanyaji wa tafiti za magonjwa yasiyo ambukizi.
Hospitali Rufaa ya kanda Bugando ina klinki na wodi maalumu kwaajili ya wagonjwa wa kifua kikuu sugu.
Uzinduzi wa Huduma za Kliniki ya kinywa na meno
Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando leo June 20, 2023 imezindua Huduma za Kliniki ya kinywa na meno katika ngazi ya kibingwa
Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando leo June 20, 2023 imezindua Huduma za Kliniki ya kinywa na meno katika ngazi ya kibingwa, ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ambaye ameambatana na viongozi wengine wa Hospitali hiyo.
Akizungumza katika zoezi hilo la uzinduzi Mkurugenzi Mkuu amesema huduma zinazopatikana kwasasa katika Idara ya Meno ni za kibingwa na bozezi, hivyo basi ametoa wito kwa wananchi kufanya uchunguzi au kliniki za mara kwa mara ambapo ameeleza kwamba Chuo Kikuu cha kikatoliki cha Afya (CUHAS) Kilichopo Bugando Kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, inatarajia kuanzisha fani ya matibabu ya kinywa na meno katika ngazi ya shahada ya kwanza. Pia wanafunzi watakaopata fursa ya kujifunza katika chuo hicho watapata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo katika kitengo cha meno kilichozinduliwa leo hii na kusaidia kupata wataalam wengi katika ngazi mbalimbali ikiwemo Hospitali za Mikoa pamoja na za Wilaya.
Pamoja na hayo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameendesha zoezi la uzinduzi wa ghala ambalo litatumika kuhifadhia dawa ambazo zitatumika kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa katika hali ya usalama.
Sambamba na hayo Dkt. Fabian A. Massaga ametoa wito kwa wafanyakazi kuhusu kutunza vifaa hivyo, lakini pia kufanya kazi kwa uadilifu na uweledi wa hali ya juu, ikiwemo kuwajali wateja wetu. Pia amemshukuru Mkurugenzi wa Upasuaji, Mkuu wa Idara ya Meno pamoja na wafanyakazi wote bila kusahau Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wao katika kuunga mkono Huduma za afya kwa hali na mali.
Uzinduzi wa ghala la kuhifadhia dawa za Wagonjwa
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameendesha zoezi la uzinduzi wa ghala la kuhifadhia dawa za Wagonjwa
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando Dkt. Fabian A. Massaga ameendesha zoezi la uzinduzi wa ghala la kuhifadhia dawa za wagonjwa Katika zoezi hilo Dkt.Msssaga ametoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na uweledi wa hali ya juu, ikiwemo kuwajali wateja wetu.
Pia ameshukuru jitihada za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wao katika kuunga mkono Huduma za afya kwa hali na mali.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian A. Massaga, leo Juni 19, 2023 amepokea ugeni kutoka nchini Ubeligiji ambao ni pamoja na Rais wa shirika la Child help International Bw. Pierre Mertens akiwa ameambatana na kamati ya harambee kutoka nchini Ujerumani Bw. Germa Nils na Bi. Luisa Schuster wa CHI (Child Help International).
Aidha wageni hawa wametembelea Kliniki ya upasuaji na wodini ambapo wamekutana na wazazi nakuonana na watoto wenye shida ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Shirika la Child Help International limekuwa likitoa vifaa vya upasuaji kwa watoto wenye shida hizi na kupunguza gharama kwa wazazi wenye watoto hawa.Dhumuni la ziara ni kutembelea watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ili kuona huduma wanazozipata ikiwa na pamoja na kuwasaidia watoto hao wakishirikiana na Hospitali ya Bugando.
Aidha Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian A. Massaga, ameshukuru ujio wa wageni hao kutoka Child Help International kwa kufika katika Hospitali ya Bugando
Katika kutekeleza agizo la Serikali kupitia Wizara ya Afya.
Katika kutekeleza agizo la Serikali kupitia Wizara ya Afya.
Katika kutekeleza agizo la Serikali kupitia Wizara ya Afya, kuwa na mashirikiano baina ya Mataifa mengine katika kukuza na kuboresha Sekta ya Afya (Medical tourism), Wataalam bingwa na bobezi kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando wamefanya kambi ya Upasuaji mkubwa wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kwa wagonjwa wenye shida hiyo, wakishirikiana na jopo la wataalamu kutoka Shirika la Hope Ministry la nchini Marekani.
Aidha upasuaji huo umeanza tarehe 12 Juni, 2023 na unatarajia kumalizika Juni 16, 2023.
Sambamba na upasuaji huo, pia kambi ya Upasuaji wa nyonga na magoti unaendelea katika Hospitali ya Bugando mpaka Juni 17, 2023. Zoezi hili la upasuaji wa nyonga na magoti litakuwa endelevu katika Hospitali ya Bugando, ambapo haya yote ni katika kutoa huduma bora za kibingwa na kibingwa bobezi ili kuboresha afya za wananchi na Taifa kiujumla.
Umoja wa wataalamu wa mafundi simu Kanda ya Ziwa katika Jiji la Mwanza
Umoja wa wataalamu wa mafundi simu Kanda ya Ziwa katika Jiji la Mwanza
Umoja wa wataalamu wa mafundi simu Kanda ya Ziwa katika Jiji la Mwanza, wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Juni 10, 2023 nakujitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa katika Hospitali ya Bugando.
Akizungumza katika zoezi hilo la uchangiaji damu Kiongozi wa Umoja wa mafundi simu kanda ya ziwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Bw. Muguwa Manyanda, amesema; “Lengo kubwa hasa sisi kama Umoja wetu tumeona umuhimu la kuja Hospitali ya Bugando kwaajili ya kuchangia damu na kuokoa maisha ya akina mama na watoto pamoja na wagonjwa wenye uhitaji wa damu hiyo. Pia kiongozi ameendelea kuishauri jamii iguswe na nasadaka ya utoaji wa damu kwa wenye uhitaji ili kuokoa maisha kwani damu huwezi kuipata popote pale bali kupitia sisi. “Damu tumepata bure tuitoe bure kwa wananchi na Tanzania kwa ujumla."
Aidha Kiongozi wa kitengo cha damu Salama Hospitali ya Bugando Sr. Lucia Ng’walu, ameshukuru Umoja wa Wataalamu simu Kanda ya Ziwa kwa wiwa kuja kuwasaidia wagonjwa mbalimbali hasa ambao wanateseka kwa namna ya pekee katika Hospitali yetu ya Bugando amesema; “Nipende kuwashukuru sana kwa moyo wao wa majitoleo kwa kuguswa na habari za wagonjwa, ninaomba na kusisitiza kwa ajili vikundi na umoja mbalimbali wa vyama vya aina yeyote ile viige mfano wa hawa wataalamu wetu wa simu waweze kufika wengine kusaidia wagonjwa, tukielewa na kuamini kwamba binadamu yeyote aliyechangia damu humu duniani ni Yesu Kristu Mwenyewe mtu yeyote anayejitoa kwa sadaka kuwasaidia wagonjwa ni sehemu ya uhai wake akisaidia kama Yesu alivyofanya; “Tone moja la damu linaokoa uhai wa mtu ambaye angefariki dakika chache zilizopo.” Pia ameomba kila mmoja aige mfano wa hawa ndugu zetu ambao wamejolea kutoa damu.
Siku ya Huduma za Magonjwa ya Dharura Duniani
Katika maadhimisho ya siku ya huduma za magonjwa ya dharura duniani.
Katika maadhimisho ya siku ya huduma za magonjwa ya dharura duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 2, Juni, Hospitali ya Rufaa Ya Kanda Bugando imeadhimisha siku hiyo kwa kutoa mafunzo ya huduma za dharura kwa nadharia na vitendo kwa Maaskari Maafisa polisi pamoja na viongozi wa waendesha bodaboda. Lengo la mafunzo hayo ni katika kuzuia ajali za barabarani akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa idara ya huduma za dharura na Dakitari. Bingwa na Bobezi Shahzmah Suleiman amesema ,“wauguzi wa idara ya dharura wamewezeshwa kupata mafunzo ambayo ni muhimu kwa mtoa huduma za dharura yoyote kwa sababu inatuweka katika uwezo wa kimataifa katika kuhudumia mgonjwa wa dharura popote pale” Kama kauli mbiu inavyosema; “usalama wako kipaumbele chetu”. Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando ambaye ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Dkt. Fabian A. Massaga amesema. “ wizara ya afya yenye wajibu mkubwa na dhamana kubwa katika afya.
SHIRIKA LA AMERICARES LAKABIDHI VIFAA TIBA
SHIRIKA LA AMERICARES LAKABIDHI VIFAA TIBA NA UPASUAJI VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILLION 200
SHIRIKA LA AMERICARES LAKABIDHI VIFAA TIBA NA UPASUAJI VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILLION 200. Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imepokea vifaa tiba na vifaa vya Upasuaji kutoka Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Americares Tanzania. Vifaa hivi vimepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos G Makalla pamoja na uongozi wa Hospitali. Akizungumza katika hafla ya makibidhiano Mhe. Amina Makilagi ameupongeza uongozi wa Hospitali pamoja na Shirika la Americares kwa jitihada wanazofanya kutokomeza Ugonjwa wa Fistula nchini, “Nipende kutoa pongezi kwa hospitali ya rufaa ya kanda Bugando, kwa jitihada zake kubwa za kupambana na magonjwa na changamoto za afya kwa wananchi, hususani kwa ugonjwa wa fistula, Nalipongeza shirika la Americares kwa juhudi linazofanya katika kupambana na changamoto za ugonjwa wa fistula nchini Tanzania, hususani katika kanda ya ziwa kwa kushirikiana na hospitali ya rufaa ya kanda Bugando.
Ugeni wa Shirika la OPUS kutokea nchini Marekani
Hospitali ya Kanda Bugando yatembelewa na Shirika la OPUS kutokea nchini Marekani
Shirika la Opus la Nchini Marekani kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha VIllanova kutoka Marekani wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda bugando katika Idara ya Saratani.
Lengo la ujio huu ni kuangalia namna ya uwezeshaji wa Taaasisi zinazotoa matibabu ya Saratani haswa Saratani za Watoto. Akizungumza katika ziara hio ,Kiongozi wa Msafara ameeleza wanavyoshirikiana na Taasisi mbali mbali duniani zinatoa matibabu ya Saratani, na leo wametembelea Bugando ili kuendelea kutimiza adhima yao ya kusaidia matibabu ya Saratani kwa watoto.
Ugeni huu umepokelewa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Fabian Massaga na Kamati Kuu tendaji ya Hospitali .
Mama Maria Nyerere ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Mama Maria Nyerere ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando
Mama Maria Nyerere ambaye ni mke wa Raisi wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ikiwa ni sehemu ya ziara yake binafsi Mkoani Mwanza.Katika ziara hii Mama Nyerere ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi.
Mama Nyerere ameupongeza uongozi kwa jitihada kubwa zinazofanyika kwa kutoa huduma bora na stahiki kwa wagonjwa na wananchi.
Sambamba na hayo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza ametembelea vyumba vya matibabu ya mionzi kwa wagonjwa wa saratani na kujionea uhitaji wa mashine ya ziada kwani mahitaji ya wagonjwa ni makubwa.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt.Fabian A. Massaga amemshukuru
Mama Maria Nyerere kwa kufika Hospitalini hapo. "Umetukumbusha historia ya ujenzi wa Hospitli ya Bugando" Dr Massaga amesema. Hayati Julius Kambarage Nyerere alikuwa muhasisi wa ujenzi wa Hospitali ya Bugando.Wakati huo huo Dkt Massaga amemkabidhi zawadi mama Maria ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wake huo katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kanda ya ziwa.
Maadhimisho ya Sherehe za wafanyakazi
Mei Mosi
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha Mfanyakazi Hodari Dkt.Fabian A. Massaga Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando ikiwa ni katika Maadhimisho ya Sherehe za wafanyakazi Mei mosi ambapo kitaifa zimefanyika Mkoani Morogoro.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (St.Augustine)
.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando leo Mei 6, 2023 imepokea wageni ambao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (St.Augustine) ambao wamewiwa kuja Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando kutembelea na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile :-pampasi, sabuni za unga na miche na dawa za meno, vifaa hivi vimetolewa katika wodi za wagonjwa wa saratani, Mifupa, na watoto wanaozaliwa utumbo wazi.Pia wamejitolea kuchangia damu kwaajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa hasa wenye uhitaji wa damu.
Aidha, wanafunzi hao wameushukuru na kuupongeza uongozi wa Hospitali ya Bugando kwa jitahada kubwa wanazotumia katika kuhudumia wagonjwa na wananchi kwa ujumla.
Latest Events